Mchango wa mh harisson makyembe na samweli sitta katika katika kongamano chuo cha ushirika

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
Mheshimiwa waziri wa afrika mashariki kafungua kongamano Chuo cha Ushirika Moshi 21 may 20011. ''KWANINI TANZANIA NI MASKINI BAADA YA MIAKA 50 YA UHURU'' alianza kwa kutoa historia ya Tanganyika, aelezea kuhusu elimu yake, vyama vya siasa wakati huo kabla ya uhuru vilikua vitatu . Pia alipata bahati ya kusomeshwa nje na serikali ya tanganyika. Baada ya kumaliza elimu yake aliweza kuwa waziri mdogo. Pia aeleza jinsi alivyopewa neno la husia na hayati baba wa taifa mwl j.nyerere alimwambia msichezee misingi ya taifa 1. Uadilifu 2. Umoja 3. Kutopjilimbikizia mali 4. Usawa na uwaibikaji
kuhusu kwanini tanzania ni maskini baada ya miaka 50 ya uhuru amesema tanzania ina rasimali nyingi tukiitumia vizuri tutafika katika kilele cha maisha mazuri tunayoyahitaji, natukiwa na dhamira ya dhati, kuwa wazalendo, tukaacha rushwa tutafika katika hali nzuri ya kimaendeleo. Akasema vijana ndio chachu kubwa ya maendeleo kwahiyo tusikubali kutumiwa vibaya katika siasa za malumbano.
Kasema yeye anaifuata toka alipoingia tanu. Na wala hafikirii kwenda chama chochote kila. Habari za kwenye magazeti kwamba alikua anataka kuanzisha chama ni majungu. Kwani yeye ni mtaji wa urais. Na ujana wake wote amekulia ccm hawezi kukiacha. Na akasema wale wote wanaoipaka matope ccm waondoke ndani ya chama.nk……
na mhehshimiwa dr harisson makyembe amesema tatizo la umaskini tanzania ni ukosefu wa wataalamu hasa katika njanja ya sayansi na teknolojia, tanzania inaitaji wataalamu physical science 837000, wahandishi 2987000, nk
MR A. MANGASINI, KWANINI TANZANIA NI MASKINI BAADA YA MIAKA 50 YA UHURU.
AMESEMA INASHANGAZA MIAKA HAMSINI YA UHURU LAKINI BADO TU MASKINI WAKUTUPWA TUNAAGIZA TISHU NA TOOTHPICK KUTOKA NJE HATA PENCELI, TOILET PAPER.
AKASEMA TANZANIA NA MASKINI KUTOKANA NA
1. KILIMO CHA KUTEGEMEA HURUMA YA MUNGU (MVUA)
2. UCHUMI UNAOTEGEMEA KILIMO ZAIDI BADALA YA VIWANDA
3. KUIGA PROGRAM KAMA MISWADA KUTOKA WB,IMF, MFANO STRUCTURE ADJUSTMENT
4. WANANCHI WAMETENGWA HAWASIKILIZWI.
5. HAKUNA SIASA SAFI
6. WANANCHI HAWANA HAKI YA KUCHAGUA
PIA ALISEMA HUWEZI KUWA NA SIASA SAFI IKIWA UNAMCHAKACHUA SPIKA BY EMPOWER WOMEN BY DISEMPOWER MEN, SHERIA YA UCHAGUZI HAIMRUHUSU MGOMBEA BINAFSI, SHERIA TATA KAMA ''RAIS UKIONA INAFAA'' KUNA SIKU RAISI ATAMCHAGUA MKE WAKE KUWA WAZIRI MKUU KWA VILE AMEONA INAFAA.
PROF CHAMBO ALISEMA USHIRIKA NA MUHIMU SANA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA LETU, AKATOA USHAURI KWAMBA SERIKALI IFUFUE VYAMA VYA YSHIRIKA VILIFILISIKA. PIA KONGAMANO HILO LILIHUDHURIWA NA MRISHO MPOTO MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZENYE KUJENGA FIKRA.
 

Attachments

  • DSC08899.JPG
    DSC08899.JPG
    716.8 KB · Views: 40
  • DSC08879.JPG
    DSC08879.JPG
    552.4 KB · Views: 40
  • DSC08881.JPG
    DSC08881.JPG
    745.1 KB · Views: 45
  • DSC08901.JPG
    DSC08901.JPG
    761.2 KB · Views: 40
Hongera sana Muccobs kwa kuandaa huo mdahalo.Kwa wote tuliokuwa pale Nyerere hall mtakubaliana na mimi kwa yote ambayo yalisemwa.
 
Back
Top Bottom