Mchango wa bint mdogo Malala Yousufzai kwa jamii vs Dr Asha Migiro akiwa UN.

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Ni bint mdogo mno lkn mwenye ujasiri wa pekee,Changamoto aliyoitoa kwa jamii ktk kumtetea mtoto wa kike apateElimu si ya kubezwa hata kidogo,lakini hasa ukizingatia pia mazingira magumu anakoishi.Nimetafakari msimamo na mchango wa mtoto huyu mana hata alipoulizwa akiwa mwenye maumivu makali kuwa ataendelea na harakati zake bila kuogopa kuuawa alijibu ataendelea.Nimemweka kwenye mzani mmoja Malala na na Dr Asharose Migiro(mtanisamehe)Huyu ni mama msomi na mwanamke aliyebahatika kushika nafasi ya juu ktk taasisi nyeti Duniani(UN)Katika utumishi wake sijawahi kufanikiwa kusikia au kusoma mchango chanya juu ya harakati za wazi za kutoachangamoto kwa ulimwengu kuhusiana na nafasi ya mwanamke,achila mbali duniani bali pia ktk serikali ya Nchi yakeambayo ameitumikia,Kuna wanawake mfano Marehemu Prof Wangai walisimama imara wataendelea kuwa mfano wa kuigwa karne na karneNa sasa bint Malala.Dr Migiro tumkumbuke kwa lipi?
 
Asharose ni bodimemba wa WAMA inayoongozwa na kilaza Salma kwa kuiga staili ya msomi AnnaNkapa
 
yule mtoto yuko smart sana..jana nimeangalia documentary moja toka huko kwao wakati wa uhai wake yaani ni mtoto jasiri sana na pia ana akili sana tena sana....

mama migiri kule UN alikuwa anashangaa tu kama jinsi m.kwere alivyokuwa anashangaa jengo huko oman juzi....
 
Dr Migiro alipata wadhifa wa UN akitokea wizara ya mambo ya nje,ambako nako kuna kukumbu tasa za utendaji wake.Tunahitaji wanawake wenye uthubutu angalau kama kina Dr Hellen Kijo,Ananilea.Juzi nimeona anasifiwasiwa na mke wa ****** kwa Sifa za plastic.
 
..kabla hajajiunga na siasa, akiwa bado ni mhadhiri UDSM, Dr.Migiro pamoja na wanasheria wenzake walianzisha kitengo cha msaada wa kisheria kwa wanawake wasiokuwa na uwezo.

..pia alikuwa na mshiriki wa kamati ya maandalizi ya Tanzania kwenda ktk mkutano wa dunia wa kina mama uliofanyika Beijing.

..baada ya hapo alikuwepo kwenye Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Kisanga. sina uhakika kama alikuwa ndiyo katibu wa tume, au mjumbe wa kawaida.
 
nitamkumbuka kwa afro lake zuri ambalo linamfanya aonekene kama mtoto wa shule.
 
Back
Top Bottom