Mchakato wa Mgombea Urais Chadema Uanze Mwaka Kesho, 2013

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Chadema itajijenga vizuri na kushinda kwa urahisi Urais wa mwaka 2015. Mimi napendekeza, Chadema itangaze mwaka kesho wanaotaka urais wajaze fomu. Baada ya hapo hatua ya pili iwe ni wananchi kuchukua kadi za chadema ili waweze kupiga kura ya kumchagua mgombea. Hatua nyingine iwe ni wagombea kuanza kupita kila kata ya Tanzania kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni. Kwa hiyo inahitajika miaka miwili kupita kata zote Tanzania kupigiwa kura. Sasa hii itasaidia sana kwani wakipita kwenye kata wanapiga kampeni ya kukijenga chama, kuandikisha wanachama na kukitambulisha chama na mgombea wake. Hadi uzunguko ukiisha tayari chadema itakuwa imeenea. Hata chama kinaweza kuweka utaratibu kuwa hata siku ya kupiga kura za maoni mtu anaweza kujiunga na chama siku hiyo hiyo na kuruhusiwa kupiga kura,

Itakuwa gharama kubwa lakini itakuwa mbadala wa operesheni sangara. Watu wote hata Shibuda waruhusiwe kugombea ili mradi tu katika kampeni mtu aseme atalifanyia nini taifa na si kupiga vita wagombea wengine
 
hiyo ni nzuri naomba wahusika tumaini makene,john mnyika na zoto kabwe najua mko huku mlichukue wazo la mdau na kulifanyia kazi ili muwape watanzania kitu wanachokitaka ili ikifika uchaguzi mkuuu kazi iwe ni kuidhinisha tu.
 
suala la urais sio muhimu kwa sasa kinachotakiwa ni kukijenga chama mkianza kuwaza mambo ya urais sasa hivi mtaingia kwenye mtego wa ccm badala ya kujenga chama wanajenga mtandao wa kuingia ikulu na kujenga makundi kitu ambacho ni hatari na ndio utakuwa mwanzo wa kusambaratika kwa chadema
 
Nani kakwambia suala la uraisi sio muhimu kwa sasa??? wazo la mdau ni la muhimu sana..kimsingi madhumuni ya chama cha siasa ni kuongoza nchi na msingi wa hilo ni kushinda uraisi. Pia kama ni mfuatiliaji vyama vyote hapa tanzania vimesambaratika ikiwemo ccm kwa mfumo mbovu wa kumchagua mgombea wa uraisi, hivyo mchakato huu unabidi upewe muda usiopungua miaka miwili.
Nachoogopa ni uroho wa madaraka kwa baadhi ya viongozi hasa baada ya kuona kua chama sasa kina wafuasi wengi na kinakubalika hivyo uwezekano wa kushinda upo.Watu hao hawatapenda mchakato mrefu na makini ila watasubili muda mfupi ili kutimiza marengo yao ya kujichagua au kujipendekeza huku wakiitisha vikao vya wazee kuwaonya vijana kwa misingi ya muda wao bado na itasambaratisha chama
mwenye sikio halazimishwi kusikia kwani huu si utabili bali imewahi kutokea
 
Watanzania unapokaribia wakati wa uchaguzi tunanasa kwenye mtego mdogo sana na ndio umetugharimu kuwa maskini tulivo! Huwa tunakimbilia majina na haiba binafsi ya mgombea kama ndio yard stick ya kumpata mgombea! Tunatakiwa kama taifa au chama cha siasa tuanishe matatizo yanayolikabili taifa kwa vipaumbele na tujaribu kukuna vichwa kupata majawabu yake tukishapatana hapo hatua ya pili tuanze kujiuliza ni nani ana qualify kusimamia hiyo dira yetu, tukishampata tumabidhi huo mpango kazi with time limit, ili akishindwa tumtoe kwa hoja! Lakini ilivo sasa watu wanachaguliwa kwa sura kuna mmoja alichaguliwa eti ni handsome that is it!!Tukichagua kwa majina tu na haiba binafsi akishaingia madarakani anafanya atakavo maana hatukumkabidhi majukumu with time limit frame work! Mwambie mgombea mwaka wa kwanza wa urais wako mfano tunataka watoto wetu kukaa chini shuleni mwisho, watu kuishi nyumba za tembe mwisho,mwambie tumia pesa kutokana na utalii, au madini ya tanzanite au dhahabu kutekeleza hayo asipofanya tutambana!
 
{Nani kakwambia suala la uraisi sio muhimu kwa sasa??? wazo la mdau ni la muhimu sana..kimsingi madhumuni ya chama cha siasa ni kuongoza nchi na msingi wa hilo ni kushinda uraisi. Pia kama ni mfuatiliaji vyama vyote hapa tanzania vimesambaratika ikiwemo ccm kwa mfumo mbovu wa kumchagua mgombea wa uraisi, hivyo mchakato huu unabidi upewe muda usiopungua miaka miwili.
Nachoogopa ni uroho wa madaraka kwa baadhi ya viongozi hasa baada ya kuona kua chama sasa kina wafuasi wengi na kinakubalika hivyo uwezekano wa kushinda upo.Watu hao hawatapenda mchakato mrefu na makini ila watasubili muda mfupi ili kutimiza marengo yao ya kujichagua au kujipendekeza huku wakiitisha vikao vya wazee kuwaonya vijana kwa misingi ya muda wao bado na itasambaratisha chama
mwenye sikio halazimishwi kusikia kwani huu si utabili bali imewahi kutokea}
Siasa ni sayansi siyo kukurupuka kama unavyofikiri kama unaamini swala la urais ni muhimu kwa sasa jishugulisheni na urais wakati wenzenu wanaimarisha mtandao wao wa chama
ccm inachowashinda vyama vingine ni mtandao mzuri walionao toka mjini hadi vijijini na mara nyingi ccm wanapokuwa wanakwenda kwenye uchaguzi tayari wanajua wana uhakika wa kupata kura kiasi gani na hata sehemu nyingine wanaposhindwa ni kutokana na kura za hasira ambazo zinatokana na makovu yakura za maonihivyo chadema wanapaswa kujua baadhi ya uchaguzi wanashindwa kutokana na kutokuwa na mtandao wa kutosha wa kuweza kudhibiti kura kura
 
Chadema itajijenga vizuri na kushinda kwa urahisi Urais wa mwaka 2015. Mimi napendekeza, Chadema itangaze mwaka kesho wanaotaka urais wajaze fomu. Baada ya hapo hatua ya pili iwe ni wananchi kuchukua kadi za chadema ili waweze kupiga kura ya kumchagua mgombea. Hatua nyingine iwe ni wagombea kuanza kupita kila kata ya Tanzania kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni. Kwa hiyo inahitajika miaka miwili kupita kata zote Tanzania kupigiwa kura. Sasa hii itasaidia sana kwani wakipita kwenye kata wanapiga kampeni ya kukijenga chama, kuandikisha wanachama na kukitambulisha chama na mgombea wake. Hadi uzunguko ukiisha tayari chadema itakuwa imeenea. Hata chama kinaweza kuweka utaratibu kuwa hata siku ya kupiga kura za maoni mtu anaweza kujiunga na chama siku hiyo hiyo na kuruhusiwa kupiga kura,

Itakuwa gharama kubwa lakini itakuwa mbadala wa operesheni sangara. Watu wote hata Shibuda waruhusiwe kugombea ili mradi tu katika kampeni mtu aseme atalifanyia nini taifa na si kupiga vita wagombea wengine

Ataiuzia chadema fuso mtumba kwa millioni 350.

Atamuweka "mchumba" kuweka software za mahesabu ya chama zinazoonesha mapato "0".

Atahakikisha mshahara wake na wengine haulipiwi kodi.

Atahakikisha kila mwenye jina ndani ya chama ana mtoto au nduguye kwenye viti maalum.

Atahakikisha kuwa kama si Mchagga basi japo uwe na mchumba wa Kichagga ndio uweze kugombea Urais.

Taifa la Tanzania bado sana kuongozwa na chadema, hilo sahauni.
 
Ningekuwa mimi ningemrudisha DR.Kwani mafanikio yaliyopo leo hiiCDM ni baada ya Dr.kupendekezwa kugombea,na bado anakubalika.Ana nafasi moja ya 2015,ikishindikana hiyo ya 2015ndio abadilishwe.CDM kwa sasa haitakiwi focus iwe kwenye uraisi,inatakiwa wapate wabunge wengi.Uwakilishi ukiwa mpana hata huyo raisi akitoka CCM atafanya kazi.Na asipoperform anaondolewa madarakani kwa kutokua na Imani nae.
Focu kubwa iwe Kupata Uwakilishi mpana Bunge ili wawe na nguvu.Wakianza sasa hivi ,vijana ma opportunist,watatumiwa kuanza kukisambaratisha chama.
 
Freeman mbowe ndiye anafaa...siyo kwakuwa anasifa za kuwa rais lahasha...kwakuwa mgombea wa urais wa cdm ni lazima atoke ule upande unaotaka kujitenga....
 
Acha kupoteza muda.cdm ni taasisi makini.hwawezi kuanza huo mchakato mwaka 2013 wakati bado chama hakijajengeka vizuri sehemu zote za nchi.ni ujinga kuandaa mgombea ambaye hamjui atapigiwa kura na nani.
 
Back
Top Bottom