Mchakato wa lami Kimara-U/Ndege waanza

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KATIKA kuhakikisha inapambana na kero ya msongamano wa magari Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni iko katika hatua za mwisho za kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara zake kwa kiwango cha lami, ikiwamo ya Kimara Temboni hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Ilala.

Barabara nyingine zinazotarajiwa kujengwa kwa kiwango hicho ni ile ya Mbezi Loius kwenda
Mbezi Beach.

Hayo yameelezwa kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda aliyesema kwamba, kazi hiyo inaweza kuanza wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

“Kikao cha tathmini ya mwisho kitaketi hivi karibuni ili kujua gharama halisi na umbali utakaojengwa kwa kiwango cha lami katika barabara za pembezoni ndani ya manispaa yetu,” alisema Mwenda.

Alisisitiza kuwa, dhamira kuu ni kuzifanya barabara za Kinondoni kuwa za uhakika na zenye kusaidia kuondoa msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na uchache wa barabara za uhakika.

“Kwa kuanzia, Februari mwaka huu tumetilia mkazo kutengeneza barabara inayotoka Kimara Temboni kuelekea uwanja wa ndege na barabara inayotoka Mbezi Louis kuelekea Mbezi Beach, nina imani zitasaidia sana kupunguza adha hii,” alisema Mwenda.

Na miezi mitano baadaye, yaani kuanzia Julai mwaka huu, halmashauri hiyo imepanga
kutengeneza barabara za pete na kurekebisha madaraja yaliyopo barabara ya zamani ya Bagamoyo.

Sehemu kubwa ya gharama za ujenzi huo inatarajiwa kubebwa na Manispaa ambayo ina vyanzo 34 vya mapato yake na tayari imejiwekea lengo la kuboresha mikakati ya kuongeza mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha.

This nchi is not short of michakato & ahadi. and the gullible will always cheer.

Mambo ya Kikwete hayo!

manispaa na kikwete wapi na wapi? hizo ni kodi za wananchi na hata kama JK asingeshinda bado zingetengenezwa yaonekana we unashabikia tu siasa hujui hata uchumi wa nchi unakwendaje.kweli wewe ni zomba unafuata tu upepo.

KATIKA kuhakikisha inapambana na kero ya msongamano wa magari Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni iko katika hatua za mwisho za kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara zake kwa kiwango cha lami, ikiwamo ya Kimara Temboni hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Ilala.

Barabara nyingine zinazotarajiwa kujengwa kwa kiwango hicho ni ile ya Mbezi Loius kwenda

Mbezi Beach.

Hayo yameelezwa kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda aliyesema kwamba, kazi hiyo inaweza kuanza wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

“Kikao cha tathmini ya mwisho kitaketi hivi karibuni ili kujua gharama halisi na umbali utakaojengwa kwa kiwango cha lami katika barabara za pembezoni ndani ya manispaa yetu,” alisema Mwenda.

Alisisitiza kuwa, dhamira kuu ni kuzifanya barabara za Kinondoni kuwa za uhakika na zenye kusaidia kuondoa msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na uchache wa barabara za uhakika.

“Kwa kuanzia, Februari mwaka huu tumetilia mkazo kutengeneza barabara inayotoka Kimara Temboni kuelekea uwanja wa ndege na barabara inayotoka Mbezi Louis kuelekea Mbezi Beach, nina imani zitasaidia sana kupunguza adha hii,” alisema Mwenda.

Na miezi mitano baadaye, yaani kuanzia Julai mwaka huu, halmashauri hiyo imepanga

kutengeneza barabara za pete na kurekebisha madaraja yaliyopo barabara ya zamani ya Bagamoyo.

Sehemu kubwa ya gharama za ujenzi huo inatarajiwa kubebwa na Manispaa ambayo ina vyanzo 34 vya mapato yake na tayari imejiwekea lengo la kuboresha mikakati ya kuongeza mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha.

Salamu Wana jamii, hii ina someka vizuri lakini kama gharama ya kuweka lami ni ile tunayo soma kwenye vyombo vya habari (takribani milioni 400 kwa kilometa) nikweli tuna haja ya lami kupunguza msongamano wa magari?

Ah! si alikuwa kwenye kikao! hizo ni danganya toto za kuvutia posho! hamna lolote

Hatutaki maneno we need to see some action, we need to see things are being done

Hivi hili neno "mchakato" kama linanitia kichefuchefu vile!

Tutaishi kwa "michakato" mpaka line?

aggggrrrrr!

Mambo ya Kikwete hayo!

Inawezekana hiyo hela ikawa ni % ndogo sana ya bajeti nzima ya manispaa...kiasi kikubwa kikiwa kinapotea kwenye posho na ufisadi. Mfano ni ujenzi wa matundu manne ya choo yaliyojengwa kwa milioni 700 huko bagamoyo na Kikwete kusomewa kama utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2005 - 2010.

Kama hela zetu zikisimamiwa vizuri tunaweza kufanya makubwa zaidi ya hayo yanayosemwa na wewe kupongeza

barabara nyingine ya muhimu ni ile ya kutoka mbezi mpka Kinyerezi kupitia maramba mawili, hiii ni bonge la shortcut

Back
Top Bottom