Ni juzi tu niliwasikia wabunge wa CCM wakiishambulia ITV kwa madai kuwa inafanya uchochezi kwa kurusha vipindi vya makongamano yanayopotosha wananchi yanayohusu upatikanaji wa katiba mpya. Na walienda mbali zaidi kwa kuisifia TBC1 kuwa imekuwa na vipindi vizuri sana....! Leo jioni hapa nyumbani nilikuta wenzangu wakiangalia kipindi cha CHEREKO kinachorushwa na tbc1 kila jumapili, ndipo hapo nikakumbuka zile sifa ambazo tbc1 ilimwagiwa na wabunge wa CCM!
Hivi kipindi kama CHEREKO kina manufaa gani kwa taifa ukizingatia ile ni tv ya taifa? Je, ni vipindi hivi hivi ambavyo wabunge wa CCM walikuwa wanatetea?
m
Hivi kipindi kama CHEREKO kina manufaa gani kwa taifa ukizingatia ile ni tv ya taifa? Je, ni vipindi hivi hivi ambavyo wabunge wa CCM walikuwa wanatetea?
m