Mchakato kupata Katiba Mpya: Hakuna Maandamano, Upinzani kwa hili!

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Jun 9, 2010
1,032
759
Nimetazama upepo unavyokwenda kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Katiba (Katiba Mpya: Masikhara haya), nimeona na kusikia maneno ya JK jana pale PTA, nimesikiliza mahojiano ya Deus Kibamba Channel Ten, Maoni ya Wana CUF na wananchi, wengi wamekata tamaa na kukubaliana na hali halisi, woga, hofu na unyonge umetujaa.

Kwa hali halisi naona kabisa hakuna mabadiliko yatakayotokea, tutakubaliana na Tume itakayoundwa, tutakubaliana na mchakato huo, tutapiga kura za maoni na mwishowe kupata katiba CCM waliyoitaka. Ndio tutapata katiba hiyo na maoni yetu mengi hayatachukuliwa, tutarudi hapa kulalamika kama ilivyo ada yetu, tutarudi hapa tena kusema tulisema sisi ona kilichotokea, hapa tulipojikwaa ndipo patakapotugharimu, UKONDOO wetu ndiyo chumo letu.

Hakika tutarudi hapa tena kulalama. NDIYO TUTARUDI na hakika Tulichokisubiri kwa muda mrefu hatutakipata. Hongereni Watanzania kwa moyo wa uvumilivu na tuendelee kuomba Mwenyezi Mungu aje atusaidie kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu, NDIYO TUOMBE MUNGU huenda atashuka atajumuika nasi na kututia ari thabiti ya kudai haki yetu.

Heri, Mafanikio na Kusubiri Kwema Watanzania ( waliokuwa Watanganyika)!!
 
inauma sana tunapojikubali kuwa sisi ni wadhaifu. inasikitisha kua ule moto na ari tuliokua nao ndo unaendelea kupotea mda unavyoenda.CHADEMA MSITUACHE TUKAKATA TAMAA.TUONGOZENI CHA KUFANYA.
 
ninavyo jua mimi chadema leo wanakutana naamini wao kama chama cha upinzani watakuja na mwongozo...ninacho kiomba kwa watanzania na hasa wana jf, tuwaunge mkono cdm kwa vitendo siyo kwenye kibodi tu..
 
Tulia usiwe na haraka tambua kitu kinachoenda kufanyika ni cha ukombozi na kuleta taifa ambalo limepokonywa na MAGAMBA so Mikakati ni mingi ambayo inasukwa juu ya hilo sio la kwenda faster bila maandalizi ya kitaifa na kimataifa.Wahenga wanasema KAWIA UFIKE.SO nakusihi usipunguze mnkali mwendo ni uleule CDM tunaamini ukombozi waja.
 
CHADEMA MSITUACHE TUKAKATA TAMAA.TUONGOZENI CHA KUFANYA.

Hapa ndio tunapoangukia wanajamii!
Tunaipa CDM kazi ya ziada, afu sisi wenyewe raia MAKONDOO CDM ikiwa inasurubiwa kwa tuhuma za kuanzisha vurugu tunakaa nyuma na kugawanyika na kuanza kuilamu tena CDM eti ni chama cha vurugu na maandamano ili kumpa Mbowe na Slaa umaarufu!
Wapendwa suala la KATIBA sio la chama wala sio la kisiasa pekee...
Wakati tunapaza sauti kuiita CDM, pia tupaze sauti kuitana mtaa kwa mtaa, tupaze sauti kuwaita wakina Mgaya wa TUCTA na vyama vyote vya wafanyakazi, tupaze sauti kuwaita CWT, tupaze sauti kuwaita wakulima na vyama
vyao, tuwaite vyama vyote vya waandishi wa habari na mabaraza yao, tuziite taasisi zote za kidini na wanaharakati wengine wote sio Jukwaa la Katiba tu !
Katika namna ambapo maeneo yote hayo mpaka sasa yapo na yalivyo kimya (nmeanza kuwa nahisia kuwa wamelamba shavu la kuwa wajumbe wa bunge la katiba, ndiyo maana hyo ni dili nyingine katika namna wabongo tunaendesha maisha kwa dili),
Ni wazi kuwa CHADEMA hamna watakachofanya zaidi ya kuonekana wanavurugu na wanaombwe la uongozi kama alivyosema muandishi mmoja (mpuuzi) wa Raia Mwema.
 
ninavyo jua mimi chadema leo wanakutana naamini wao kama chama cha upinzani watakuja na mwongozo...ninacho kiomba kwa watanzania na hasa wana jf, tuwaunge mkono cdm kwa vitendo siyo kwenye kibodi tu..
Hivi kwani Wana JF wote ni CHADEMA?
 
Meking Si mmeshampa siku 100, halafu mkasahau kusema zinaanza lini...


Samahani Meking nahitaji kupata kilichomo kwenye huo waraka kama unao uweke hapa niupitie nijue nini hicho kilichomtisha waziri vuai
 
Hivi kwani Wana JF wote ni CHADEMA?

We ni mwana JF, hebu saidia kujijibu hilo swali.
Afu soma tena hyo post ya Crashwise, soma katikati ya mistari! Usipoelewa soma thread nzima na post za member wote, usipoelewa na hapo itakuwa unahitaji msaada wa ziada...
 
It's a shame that we have a president who has never been, never he is and never will be a role model. he's a complete failure and i wonder if he thinks he is proud of leading this nation.
 
JouneGwalu umesema yote, tatizo tunaipa Chadema mzigo mkubwa wa kutuamulia jambo ambalo hawatakiwi kufanya peke yao bila nguvu ya ziada toka kwa wanaharakati na wananchi kwa ujumla wao. Tuamke
 
katiba ya ccm inakuja na ndiyo itakayo tuongoza.natamani nihamie Juba.Kwel ccm ndo chanzo cha umasikini wa watanzania
 
ninavyo jua mimi chadema leo wanakutana naamini wao kama chama cha upinzani watakuja na mwongozo...ninacho kiomba kwa watanzania na hasa wana jf, tuwaunge mkono cdm kwa vitendo siyo kwenye kibodi tu..
Kuwaunga mkono CHADEMA ndiyo kupata katiba inayokidhi mahitaji yetu? Usiwapotoshe watanzania, suala la katiba halifungamani na itikadi ya chama chochote cha siasa, tusubiri tume itakayoundwa na tuipe ushirikiano.
 
Sisi watanzania tuna kasumba moja mbovu, tusitegemee chama chochote cha siasa kutukomboa pasipo ushiriki wetu, kamwe hili halitatokea vinginevyo labda miujiza itokee kutoka kwa mungu, lakini naye mungu hapendi watu wavivu kama sisi ambao roho zetu zimetulia na kulizika kuwa chadema watatukomboa bila ya sisi kuwa nyuma yao. Ukweli ni kwamba tumeyazidi hata mavuvuzela ya kichina na tunapenda kujilinganisha na vitu tusivyolingana navyo hata kidogo
 
Back
Top Bottom