Mchakamchaka wa CUF hadi 2015 tishio kwa afya ya CDM

Ndiyo mbinu mliyopewa na 'mume' wenu wa ndoa CCM? Endeleeni tu lakini tunawahakiikishia kwamba tunazijua mbinu zenu zote maana Mzee wenu mwenye sura ya ngedere (Wahasira) alishaupasha umma eti CDM itakufa karibuni! CDM haipo hapo ilipofika kutokana na bahati au ridhaa ya CCM bali kwa kazi makini ya makamanda wake. Kama mnabisha ingieni uwanjani kule Rukwa na Igunga mkachumbiwe. CUF ni iCCM B na imeshalewa sumu katika tende na haluwa za fisadi CCM alizowahonga kule
Zanzibar! Sasa wanaweweseka mithil ya wagonjwa wa maruhani.

we kama ni mwanamke hutakaa uolewe ktk maisha yako,utaishia kuzalishwa tu na kuwatia aibu wazazi wako
 
acheni basi kuua wananchi wanaokuja kwenye mikutano yenu ya kampeni kuelekea 2015

Nyie jamaa mwaka 2000 na 2005 si mbali ambapo mlikuwa Chama kikuu cha upinzani na polisi walikua wanatifua karibu mikutano yenu yote. Fujo zote, na damu yote iliyomwagwa na polisi leo mmesahau mnaungana na CCM kuwalaumu CHADEMA kwa fujo ambazo zinaanzishwa na polisi. Ama kweli!! Ukiwa muongo inabidi uwe na kumbukumbu.
 
Ni bora ungeleta hoja kama mchambuzi namna gani hiyo operesheni ya CUF itaimaliza CHADEMA, ila wewe umeleta habari kama umekurupuka. Na hivi adui wa CUF ni CHADEMA?
 
Mbona Hii ya CUF binafsi nimeipenda!! Kwani hata Hata jiwe linahitaji kupata Habari ya Mabadiliko!! Sasa kwa walichokisema jana CUF nadhan nawapongeza sana kwa kusaidia Kuboresha kampeni za M4C. Kama mmewapa hela ili waaribu Ujue Imekula kwenu!!! Pia nataka Kujua lile Zuio la sensa Jana lilikuwa Limekwisha?
CDM tunaongoza wengine wanafuata tu!
 
Chadema ni chama kinachobagua watu kwa dini zao na kina agenda za siri. Mimi binafsi sio mfuasi wa chama chochote but cdm yenyewe inalitambua hilo, tunajua kua cdm wamenunua vyombo vya habari. Wasiojua siri za chadema behind the scene poleni na sisi mnaotaka kutubagua tumejipanga vyakutosha.
 
Mimi nadhani ni wakati muhafaka CUF na CCM kuungana rasmi kupambana na chama tawala CDM kitakacho ingia Ikulu miaka 2 na robo ijayo.
 
Hawa ni magamba wanataka wapinzani wagombane ili wapate unafuu, mmeliwa tuliisha wagundua kabla hamjaanza. Kwanza CUF wenyewe wanalenga mikoa sita tu, CDM inalenga nchi nzima. Kwani hapo tatizo liko wapi? JIFARIJINI MAGAMBA LAKINI KUMBUKA MWISHO WENU UNAKARIBIA

awamu ya kwanza ya mchakamchaka ni mikoa sita
 
Hali imezidi kuwa taabani kwa CDM baada ya CUF kuzindua kauli mbiu ya Mchakamchaka hadi 2015. CDM poleni sana kwani katika kipindi kifupi mtaondokewa na wanachama pamoja na wafuasi wengi. Mara ya CUF kuzindua rasmi harakati zao za kuelekea 2015, makundi ya vijana waume kwa wake, walionekana wakirudisha kadi za CDM kwa vile wamechoshwa na vurugu zinazofanywa na CDM siku hadi siku na hivyo kuharatarisha ustawi wa nchi yetu.

Hiyo ni janja ya CCM kuongeza miruzi mingi ili impoteze mbwa lakini jamii ya sasa ni yenye kujua mbivu na mbichi. Waje tu na siyo wao tu hata ADC nao wazindue kampeni zao ili CDM wakishinda ushindi uwe mtamu, iwe imeshinda kwa halali na kuwashinda wote mke na mume plus watoto.
 
Chadema ni chama kinachobagua watu kwa dini zao na kina agenda za siri. Mimi binafsi sio mfuasi wa chama chochote but cdm yenyewe inalitambua hilo, tunajua kua cdm wamenunua vyombo vya habari. Wasiojua siri za chadema behind the scene poleni na sisi mnaotaka kutubagua tumejipanga vyakutosha.
Hasa magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Daily News, Habari leo, Alnoor, Fahamu, Mtanzania, Tazama na Zanzibar leo.

Pia TBC, Radio Imaan, Radio Uhuru na Bakwata zote hizo zimenunuliwa na CHADEMA.
 
Kuna vitu vingine ni akili ndogoa tuuu...Kama kweli mtoa hoja ni CUF basi kwa aliyoandika hafai kabisa kua mwanachama wa CUF kwani anazidi kukimaliza chama kama ifuatvyo...1>unaposema kuhusu CDM wakati unajua fika CDM si chama kinachotawala inamaanisha ama CUF inatumwa iizoofishe CDM au CUF na chama tawala yaani CCM ni kitu kamoja kama wengi wetu tunavyoamini....2>CUF haina lengo la kuchukua nchi ila kuwashawishi wanachama wa CDM kujiunga kwao ambapo hiyo haitawasaidia kufika popote katika chaguzi zozote....
Anachotakiwa afanye mtoa hoja ni kuwaondolea wananchi zana ya kua CUF imefunga ndoa na CCM kwa maneno na vitendo pia kwani hilo tu peke yake linawamaliza sana CUF na Mtatiro alishakiri hilo.Kubadilisha taswira nzima ya chama kwa kuweka watu ambao wana nguvu ya ushawishi kama ilivyo kwa CDM...Mwisho naamini kua CDM ndo chama cha kuigwa katika kila nyanja...mtumie CDM kama mfano na msione aibu kwa hilo ama sivyo MCHAKAMCHAKA hauta fika popote......Ni yangu binafsi.
 
Chadema ni chama kinachobagua watu kwa dini zao na kina agenda za siri. Mimi binafsi sio mfuasi wa chama chochote but cdm yenyewe inalitambua hilo, tunajua kua cdm wamenunua vyombo vya habari. Wasiojua siri za chadema behind the scene poleni na sisi mnaotaka kutubagua tumejipanga vyakutosha.
Tumeshazisikia hizo CD na sasa zimeshatuchosha masikioni. Tubadilishieni mpya ili angalau masikio yetu yapate kitu kipya. Kwani CUF ni cha dini gani vile na kinafuata itikadi ipi? Kwa taarifa zenu tumeshaelewa si nyinyi mnaojaribu kupambana CDM bali ni mume wenu CCM aliyejificha nyuma ya pazia baada ya kuona amepoteza credibility kabisa sasa anataka kuwachanganya watanzania kupitia mavuvuzela - CUF! Ni aibu kwa chama cha siasa kutumika kama tarumbeta la chama kingine; ndiyo maana mmepoteza ladha miongoni mwa watanzania. Shame on you CCM, CUF.
 
awamu ya kwanza ya mchakamchaka ni mikoa sita
Hata hiyo kaulimbiu yenu ya mchakamchaka mmepewa na CCM kwani kaulimbiu hiyo ingetumika na CDM sasa hivi maelfu wangeshauwawa kwa kisingizio ni waasi! Watanzania si mazuzu hata kidogo kudanganywa na porojo za udini, ukabila na hizo propaganda zenu za .... ooh CDM wanaua watu, .... cha matabaka.... mnataka kusema wale 25 waliouwawa kule Zanzibar mliwaua na baadhi kuwapeleka ukimbizini (Somalia!) ili Maalim Seif awe hapo alipo?
 
kama CUF inataka ustawi kwa siasa za sasa....basi ibadlishe mfumo mzima wa uongozi.....walenge kundi la vijana pia.......watanue wigo wajikite zaidi maeneo yenye wafuasi wao wachache....
 
Back
Top Bottom