Mchaga Tajiri, Bahili!

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493




Mzee mmoja wa kichagga tajiri kwa jina la MDAWA alipata ajali mbaya sana ya gari. Alipoteza
fahamu na kupelekwa KCMC huku matumaini ya kupona yakiwa yametoweka kabisa. Kutokana na

juhudi za madaktari (pengine na Mungu wake) aliweza kupata fahamu baada ya wiki tatu. Muda

wote huo familia yake ilikuwa ikokaribu naye kusubiri litakalotokea. Mkewe na watoto wake watatu waliruhusiwa kuwa naye pale ICU (Intensive Care Unit) kwa zamu. Basi baada ya
kupata fahamu nesi aliyekuwa anamhudumia alimwambia ;

NESI: Baba pole sana

MZEE MDAWA: Unanipa pole kwani nini kimetokea?

NESI: Baba ulipata ajali mbaya sana ya gari wiki tatu zilizopita.

MZEE MDAWA: Kweli, Kari yangu itakuwa imepona?

NESI: Hapana imeharibika kabisa Baba.

MZEE MDAWA: Hai jamani FII EKIS (VX) yangu. Niliinunua kwa bei kubwa mno. Sasa
nitapata wapi
nyingine...aaaiiii aaaaaaiii aaaaaiiii!

NESI: Baba usilie, hilo mbona ni kidogo? Unajua mkono wako wa kushoto umekatika kabisa?

MZEE MDAWA: Mkono wa kushoto? Umekatika? Ule mkono niliovaa ile saa yangu ya bei mbaya? Yaani

saa yangu nayo imekwenda? Aaaiiii....aiiii...aiiiii, jamani saa yangu.

NESI: Baba acha kulia, utaumia zaidi

MZEE MDAWA: Hapana mwanangu, kama kari yangu na saa fyote fimekwenda kwa nini roho isiniume

? Hifyo fitu ni fya bei mbaya sana ati...

NESI: Baba tulia, familia yako iko hapa wanataka kukupa pole.

MZEE MDAWA: Iko hapa ee? Mama Sikola, uko hapa?

MAMA: Ndiyo ! mume wangu, siwesi kukuacha mwenyewe. Pole sana mpenzi. Tunamshukuru mungu

sasa unaongea. Yesu asifiwe sana !

MZEE MDAWA: Sawa, Kodilafu uko hapa?

GODLOVE: Ndiyo Mzee, siwezi kukuacha mwenyewe katika hali hii. Pole sana Baba.

MZEE:Sikola, na wewe uko hapa?

SKOLA: Ndiyo Baba, hatuthubutu kukaa mbali na wewe ukiwa katika hali hii baba. Ni hali ya

kutisha sana .

MZEE: Na huyu kitinda mimba wangu Ferenaisi, yuko hapa?

Verynice: Niko hapa baba, nyumba yote iko hapa kukupa pole.

MZEE: Basi nyie wote hamna akili hata mmoja. Yaani Mmekuja wote hapa, dukani kabaki nani

leo? Yaani munanona kari yangu ni hiyo imepika msinga tayari na saa yangu ya bei mbaya

imepotea badala ya kukaa dukani wote munaongosana kuja huku KCMC. Nyie ni wajinga

wa mwisho kabisa.
 
Ahsante Rev kwa burudani iliyofanya niangue kicheko. Vipi sasa ile kitu umeachana nayo kabisa baada ya kupata promotion?
 
nimecheka sana, hayo majina yanavyotamkwa sasa...ferenaisi....Masa una balaa wewe...lol ...tudumu wachagaaaaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom