Mch. Mwasapile vs. Mch. Rwakatale

Miss Judith inabidi tuwafundishe hawa ndugu zetu kwa upendo na uvimilivu mkubwa kwani naona hatari ya kupotea njia na kutekwa na shetani kama vile mama yetu Eva alivyotekwa na enticing words of the satan na ku handle in devils hands the mighty power given to the man by God kwa condition ya utii. Waliamua kumtii shetani na kudharau maagizo ya Mungu, still todate we practice the same sin.

Its very clear kwamba God declared I am (Jesus) The TRUTH, WAY and the LIFE. Akaongeza nobody comes to the father except through me, akaendelea kusema yaja roho ya mpinga kristo akai describe hiyo roho characteristic yake ni kuwa kila roho isiyo kiri kuwa Yesu alikuja katika mfano wa mwandamu, akafa, akazikwa na siku ya tatu akafufuka kisha akapaa mbinguni kwa baba na kuwa atarudi tena kuwachukua walio wake. Akasema nitawa letea msaidizi atakaye kuwa pamoja nasi mpaka atakapo rudi. Hii ni foundation ya imani.

Ndugu zetu wanaoitwa wakristo bado hawazingatii hayo maagizo. Wanatenda dhambi ile ile ya kukosa utii. Hawataki kuamini kuwa imani huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu. Hawataki kusoma/meditate kwenye neno la Mungu ili wapate imani na kupitia Imani wapate ufunuo wa roho mtakatifu ambapo watasikia neno la wokovu ambao utawapa fursa ya kuwa viumbe wapya (Born of spirit). Wanapenda mazoea na kupata masses comfort a kind of mob psychology. Wengi hawana nguvu ya Mungu (Roho matakatifu) ndani yao na hivyo hawajui kuwa siyo wakristo maana neno liko clear kwamba asiye ndani yangu wala mimi simjui. Kwasababu hawana huyo roho basi are sweeped by any voice coming to them kwasababu walio wa kristo waijua sauti yake. Kama miracle ingekuwa kigezo cha utakatifu ama alama kuwa wewe huna dhambi basi wanawaisrael wasinge weza kumgeuka mungu huko jangwani nakuanza kuabudu sanamu. Maana hakuna miracle kama kula mana, kware, kuongozwa na nguzo ya moto usiku na wingu mchana. Kama miracle ingekuwa sign basi wale wachawi wa misri wasingeweza kugeuza fimbo zao kuwa nyoka kama alivyofanya Musa.

Tutafakari kidogo hao nyoka...ina maana kwamba devil anaweza ku mimic a God kind of miracle ila miracle ya Mungu lazima iwe high class na i demostrate power kwamba hata kama wachawi waliweza lakini nyoka wa Musa aliwameza majoka yote ya wachawi na bado akabakia katika the same size and form..kwamba God is the same and all creation is contained in him. Sasa huyo Babu anafanya miracle kwa kikombe cha dawa lakini hiyo miracle imeshindwa kulinda watu wote walioenda huko kwa imani ndiyo maana wengine walikufa kabla ya kupata huduma...hapo Mungu unamwona wapi? the power of God can not be limited kwenye Kikombe na babu tu..Inamaana babu kwa Imani angeweza kudeclare kwamba anybody from the moment ameondoa mguu wake nyumbani hakuna atakaye kufa na bado hiyo declaration ikawa endorsed with heavens kwasababu is God in functioning through holly spirit. Holly spirit's power is not limited kwenye kikombe na babu He is almighty! Utaona mwanamke aliyekuwa akitokwa damu alipogusa pindo tu alipona pamoja na ule umati kuwa mkubwa na ukumbuke that happened ata time when holly spirit was not yet released on earth..uwepo wa Yesu tu pale magnitude ya holly spirit ilikuwa mpaka to the atmosphere...Jaribu kuona power ya holly spirit kama radiation na media kuu ya kubeba hiyo power ni uttered words..unapo release words kwa imani impact yake ni wewe unaweka boundaries ukisema the whole world it goes ukisema Tanzania nzima it goes. Condition ni imani ndani ya moyo na uttered word! Ndiyo maana Mungu alipo umba hakuwaza tu no alitamka dunia tokea na ikawa na nguvu ile ile iliyo create heaven and Earth (Holly spirit) ndo iko ndani yetu...

So you can see how doubtfull is babu kwenye hiyo miracle yake!

ni kweli nakubaliana nawe na kuungana nwe katika wito wa kuwafundisha wapendwa wetu wanaopotea wasipotee zaidi. kwa hakika huyu ni jaribu jipya na la aina yake kwa wakristo hata wakamwacha Roho wa uzima na kuyageukia mazingaombwe hata kabla ya kujua nguvu iliyo nyuma ya mazingaombwe hayo. Neno la Mungu ni taa na mwangaza wa maisha yetu, lakini wakristo wenzangu wameyakataa maneno ya Mungu na wameamua kujifunza katika kikombe cha babu na hawana muda wa kusoma ama kusikiliza wito wa kuyarejea maneno ya Mungu aliye hai. ni huzuni kuu, ni maombolezo kwao wote wenye mwili na wenye tumaini la kuiona furaha kamlifu itokayo kwa Bwana wetu Yesu kristu aliyetukirimia baraka hizi za rohoni.

ubarikiwe sana mpendwa kwa uafafanuzi wako mzuri wa kweli ya Mungu. hakika umeutimiza wajibu wako na baraka za Mungiu zitakaa nawe na kufanyika ulinzi maishani mwako. mimi sitachoka. namwomba Mungu anizidishie uvumilivu na upole ili kama nimepata kibali machono pake basi nizishuhudie nguvu na uweza wake katikati ya mataifa kwa ujasiri na hekima yote Roho atalayonijalia. niwafundishe masikini, wagonjwa na wakosaji njia zake ili warejee kwake.

ubarikiwe uingiapo, ubarikiwe utokapo, sasa na hata milele. amina.

Glory to God
 
nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.

binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.

sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.

kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!

binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!

siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)

naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.

HUKUMU NI ZAKE BWANA

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God

Atawauliza "mnamwamini MUNGU" mtajibu "ndiyo tunamwamini" atawaambia "basi niaminini nami aliyenipeleka"
N.B kila neno katika BIBLIA lafaa kwa mafundisho, hakuna ajuaye sana wala ajuaye kidogo mbele za MUNGU, wote hatujui, na maandiko yasema sehemu fulani "tunaokolewa kwa neema tu" ujuzi wetu hauna msaada wowote. MUNGU akipenda atuepushe kukinywea kikombe cha ghadhabu yake, watu wote tuseme amen.
 
Hellow brethren here is an audio preaching that can help you know what it means by the word of God
Audio messages - Welcome to Pastor Joseph online. and || Pastor Chris Online - Channel || http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed/?videoID=vid3cac606
Be blessed
 
Atawauliza "mnamwamini MUNGU" mtajibu "ndiyo tunamwamini" atawaambia "basi niaminini nami aliyenipeleka"
N.B kila neno katika BIBLIA lafaa kwa mafundisho, hakuna ajuaye sana wala ajuaye kidogo mbele za MUNGU, wote hatujui, na maandiko yasema sehemu fulani "tunaokolewa kwa neema tu" ujuzi wetu hauna msaada wowote. MUNGU akipenda atuepushe kukinywea kikombe cha ghadhabu yake, watu wote tuseme amen.

Yesu alisema ukiijua kweli itakuweka huru, na akasema tena, wamuabuduo halisi watamwabudu Mungu kwa roho na kweli, Mungu ni roho na imetupasa kuwabudu katika roho na kweli. tafakari hayo na kisha tufafanulie una maana gani unaposema kuwa ujuzi wetu (wa neno la Mungu) hauna msaada wowote? bila kuijua kweli (Neno la Mungu) utawezaje kumwabudu Mungu kwa roho na kweli?

Glory to God
 
Kwako Miss Judith, Usiku wa kuamkia leo kuna jambo limenitatiza sana ningependa niondoe khofu yangu kwa kuliweka wazi. "Babu" kasema ameoteshwa na "Mungu" halafu "Babu" akaendelea kusema "Mungu" amemwambia atoze shilingi mia tano tu! Swali "Mungu" ana haja gani mia tano zetu? Hizi mia tano nina shaka nazo! Na sidhani kama Yesu aliponya watu kwa kuwatoza aliwaponya watu ili wapate kuamini Mungu yupo na ana uwezo wa kufanya jambo lolote hiyo ni "imani" kuwafanya watu waamini. Hii mia tano inanitatiza sana mimi.
 
Ndugu yangu Mohamed shosi, kwa kuwa mwenyewe kasema mungu amemuotesha hiyo dawa na kumuagiza atoze sh. 500/- tu kwa kila anayeihitaji, na yeye akaamini na kuchukua hatua na hatimaye kafanikiwa kuwaaminisha watu wengi tu wa mataifa mbalimbali juu ya hiyo dawa yake, basi hakuna ubishi kuwa hii nayo ni imani. Homework tuliyonayo ni:
1. je, hii ni imani ya aina gani?
2. imani hii inamuelekea mungu gani?
3. hii ni imani ya dini gani?
4. mungu mwenye utaratibu huo alioutoa ni yupi?, yuleyule aliyemtuma Yesu duniani kuokoa wanadamu, au mwingine?

Toka mwanzo nimesema waziwazi kuwa kutokana na utaratibu mzima wa ndoto hii na ufunuo huu na jinsi unavyotekelezwa likiwemo:
· hilo la kutoza sh. 500/- kwa kila kichwa,
· tiba kwa kikombe kimoja cha dawa bila kumhudumia mgonjwa kiroho,
· tiba kufanyikia loliondo peke yake,
· wengine wanapewa kikombe wakiwa ndani ya magari na wakishakunywa wanageuza na kuondoka bila hata neno moja la Mungu
· nk.

Kwa kweli mi sioni kabisa imani na utaratibu wa dini ya kikristo katika haya mambo yanayotokea huko loliondo, labda mtu wa dini nyingine aje abainishe kama dini yake inayakubali uponyaji wa utaratibu huu kiimani. Tena niwatahadharishe watu kuwa, kule kusema kuwa tiba imegunduliwa na mchungaji mstaafu wa KKKT baada ya kuota ndoto (kupata maono) haitoshi. Lazima tuchunguze na kuujaribu kila ufunuo na tujiridhishe kuwa uko consistent na imani yetu, vinginevyo tutakuwa tumekwama katika kumpa Mungu ibada kamili, safi na utukufu inavyosyahili.

Mungu aliyemtuma Yesu kuja kutafuta na kuokoa kilichopotea, hahitaji hata senti yetu moja (sembuse mia tano?). neema ya Mungu wetu huyu hutolewa bure hata kama wengi wanaona 500/- ni sawa na bure, lakini bado si bure. Na kwa kwa maelfu ya watu wanaomiminika huko hata kama anabaki na 200/- bado anaweza kuwa milionea very soon! Hapo hatujazungumzia zawadi nyingine ambazo watu wanaweza kuwa wanaenda kumpa baada ya kupona au kupata faraja ya tiba yake. Hizi hazisemi kabisa!

Yesu alikuja kuokoa waliopotea dhambini na kuwavuta wapate kuamini na kutubu wamrudie Mungu wa kweli. Huyu hahubiri mtu, anagawa dawa kwa malipo, amelenga kutibu mwili hajishughulishi na kutibu roho za watu walioangamia dhambini. Anasema kila anywaye atapona na kuwaita watu wote waende samunge kunywa dawa. Hata wakati wa Yesu, si wote waliponywa, kulikuwa na vipofu wengi sana katika Israel wakati ule, lakini ni Bartimayo na wachache wengine pekee walioponywa, hata enzi za naaman kulikuwa na wakoma wengi sana lakini ni naaman pekee aliyeponywa wakati wa Elisha, kulikuwa na vichaa wengi sana Israel wakati wa Yesu, lakini aliyeponywa ni legion pekee nk nk.

Ni wakati sasa wa kuwa waangalifu na ndoto kama hizi. Na kuendelea kumuomba Mungu atuzidishie hekima manake maangamizi yatokanayo na kukosa maarifa sasa ni dhahiri zaidi kuliko wakati tulipoanza kuamini.

Ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God
 
Ndugu yangu Mohamed shosi,

Homework tuliyonayo ni:

Shukrani sana Miss Judith,

Upeo wako wa kufikira na kuchambua mambo ni mkubwa sana, huwa nafurahi ninapokutana na watu kama wewe wenye kusimamia misingi ya kweli ya dini zao. Hata baniani anatakiwa aangalie maadili ya dini yake na si kinyume. Unapomponya mtu kwa jina la Mungu ni wajibu wewe mpomyaji umepe neno la Mungu amtambue na kuyatambua maamrisho ya Mungu.

Loliondo tumeshuhudia mamia kwa maelfu ya wagonjwa wenye imani tofauti na wasio amini (wapagani) wamepewa kikombe wametoa mia tano wamegeuza wakaondoka na kuendelea na "miungu" wao na kumsahau "mungu" aliewaponya ugonjwa wao.

Khofu yangu kuwa pengine imani ya kumwamini "mungu" aliemuotesha babu si issue, issue ni hilo "jero" maana imedhihiri kuwa bila "jero" no cup of herb.

Asante sana dada judith kwa fikra pevu.............
 
Toka mwanzo nimesema waziwazi kuwa kutokana na utaratibu mzima wa ndoto hii na ufunuo huu na jinsi unavyotekelezwa likiwemo:
· hilo la kutoza sh. 500/- kwa kila kichwa,
· tiba kwa kikombe kimoja cha dawa bila kumhudumia mgonjwa kiroho,
· tiba kufanyikia loliondo peke yake,
· wengine wanapewa kikombe wakiwa ndani ya magari na wakishakunywa wanageuza na kuondoka bila hata neno moja la Mungu
· nk.
Hivi Yesu alifika Tanzania,malawi au Papua new guinea??
 
Pamoja na reservations zangu juu ya dawa/tiba hii, huyu babu amekuwa very clear juu ya kile alichoota. 'Ametumwa kuandaa na kutoa hiyo dawa kwa sh 500'. Hajaagizwa kufanya zaidi ya hapo.
 
Mimi sina shida na ndoto yake ila wasiwasi wangu mie upo kwenye "mia tano" huyo aliemuotesha ndoto ni huyu huyu Mungu wa Isaya na Yakobo? aliemfanya Yesu akawaponya watu bila malipo? au kuna Mungu mwingine aliemuotesha? je hizi mia tano (sio nyingi kwa mtu kushindwa kuimudu) lakini je zinaenda wapi? Mungu alimpa maelezo ya hizo "mia tano"? je Mungu huyu tumjuae sie wa Isaya na Yakobo anahitaji mia tano zetu??????????
 
Mungu wa babu (kwa uwezo wake mkuu) alijuwa kutakuwa na gharama kuiandaa dawa hiyo na hiyo 500 ndio inatosha! Hebu angalia babu anahudumia watu wote hao kwa muda wote huo, unadhani atalima saa ngapi ili apate kula?

Mwenyewe umesema hapo mwanzo tusimlinganishe babu na Yesu! Babu ni binaadamu wa kawaida kama mimi na wewe, Yesu ni Mungu! Hivi unadhani dawa zote hizi tunazolipia mamilioni mahospitalini zimetoka wapi? Hudhani kuwa ni Mungu wa Ibrahim anafanya kazi yake na waja wake tunapona na kupata afya njema tena ili tuendelee kumtumikia?

Hoja ya kwamba eti kwa sababu inatozwa pesa basi haitoki kwa Mungu (wa kweli) haina mshiko na kwa hakika inamdhalilisha huyo Mungu tunayedhani tunampigania hapa.
 
Mungu wa babu alijuwa kutakuwa na gharama kuiandaa dawa hiyo na hiyo 500 ni

Mkuu "mungu" wa "babu" atakuwa ni tofauti na Mungu wa Isaya na Yakobo kwani Mungu wa Isaya na Yakobo hana shida ya mia tano zetu bali sisi ndio wenye shida na uzima wa milele na yeye ndie mwenye kuwezesha sie tukauona uzima wa milele kwa kuliamini neno. Huyu "mungu" wa babu yeye hana haja na watu kupata neno lake anachoangalia ni "babu" kukusanya mia tano tu..............
 
Anataka wote wapone/tupone. Kama ni kweli watu wengi wanapona kwa hiyo mia 500 baada ya kuahangaika na kutumia mamilioni kwengineko huoni hilo pekee linatosha sana! Na kwa hakika babu hajasema kama hiyo mia 500 unayotoa unamtolea Mungu. Mara ngapi tunachanga malaki na hata mamilioni ili huduma za kiroho na hata za kimwili ziweze kufanyika/kusambazwa na kuwafikia watu wengi zaidi?
 
Nina maswali mengi sana yananiumiza kichwa na majibu yako ya jumla yanazidi kunichanganya, hivi huyu "babu" aliongea na Mungu kama alivyoongea na Musa wakati anampa amri kumi?
 
Samahani sana mkuu yaani "babu" unataka kumfananisha na Yesu????????? Khaaaaa yaani wewe jamaa wa ajabu sana unamfananisha Messi na Ngasa?! Yesu ni world ICON huwezi kumfananisha na mtu wa kawaida mkuu..............

Yesu sio ICON wewe! huwezi kum term Yesu kama I con, et tena "world Icon"
 
haya mambo ya iamni bwana me hua wala sipendi sana kuyahusisha na fikra, manake ukishaweka fikratu tyari doubt ni nyingi mno.
Mbona Musa aliambiwa ayachape maji kwa fimbo ndo njia ikatokea, kwa nini asiambiwe ayaamuru tu yasogee na njia itokee?
Samaki na mikate ilibarikiwa ikaongwzeka!!
Me adhani kikiubwa ni kua lazima kila muujiza uje kimiundombibnu ambayo ikihusishwa na hali ya kawaida ya maisha yetu tutaipoke kiwepesi.
Ingekua vigum zaidi kuamini kama babu angeua anasema neno"pona" na watu wakapona, ila kwa kua tumezoea kunywa dawa ndo tukapona basi babu nae muujiza kaoneshwa kwa njia hyohyo ya kiuponyaji tulozoea.
 
Shukrani sana Miss Judith,

Upeo wako wa kufikira na kuchambua mambo ni mkubwa sana, huwa nafurahi ninapokutana na watu kama wewe wenye kusimamia misingi ya kweli ya dini zao. Hata baniani anatakiwa aangalie maadili ya dini yake na si kinyume. Unapomponya mtu kwa jina la Mungu ni wajibu wewe mpomyaji umepe neno la Mungu amtambue na kuyatambua maamrisho ya Mungu.

Loliondo tumeshuhudia mamia kwa maelfu ya wagonjwa wenye imani tofauti na wasio amini (wapagani) wamepewa kikombe wametoa mia tano wamegeuza wakaondoka na kuendelea na "miungu" wao na kumsahau "mungu" aliewaponya ugonjwa wao.

Khofu yangu kuwa pengine imani ya kumwamini "mungu" aliemuotesha babu si issue, issue ni hilo "jero" maana imedhihiri kuwa bila "jero" no cup of herb.

Asante sana dada judith kwa fikra pevu.............

mkuu Muddy ,

nakushukuru sana kwa kutambua na kuliona hilo la mia tano kwa ajili ya tiba ya babu. na nimefuatilia vizuri unavyomjibu SMU na nimekubaliana na mtazamo wako na kwa kweli ni sahihi. ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom