Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

Kama hata mtoto wa darasa la pili anamkubali msigwa kuwa aliongea vitu vya maana sasa wewe mwenye phd itakuaje ?unaesema hakuna kitu.pole wasomi wetu.ndio maana mtoto tanzania amedumaa hakui yupo pale pale.ni kwa sababu wengi wa wabunge pale wana akili finyu sana sana.hawastahili kuwepo pale.uchaguzi unaokuja utasadia kuwang'oa ili wapate nafasi kwenda kuendeleza majungu yao kule vijiweni
 
Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.
Mmmhhhhh, ptuuuuu!!!
 
Mh Msigwa wenye akili na wamekusikia vilaza wamebaki mabwepande wanasubiri kuteka mwingine tena
 
Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.

Starn, kuna sehemu inasema mtu kama ni kiongozi wa dini au aliwahi kuwa kiongozi wa dini kama Imam, mchungaji au Monks haruhusiwi kuongoza wananchi kuwatoa katika maisha mabaya na ya kuonewa na kuwapeleka kwenye haki na mafanikio?

Askofu Makarios wa Cyprus aliamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha siasa baada ya kuona viongozi ni dhaifu na akawaongoza vizuri wananch wa Cyprus, Ayatollah Khomein wa Iran aliongoza mapinduzi ya kiislamu kuondoa utawala wa Shah kutoka katika unyonyaji na manyanyaso ya Shah wa Iran, Askofu Desmond Tutu aliongoza harakati za kudai haki kule Afrika ya Kusini dhidi ya Makaburu na kushinda tuzo la nobel, Monk wa Budha Dalai Lama amekuwa akiongoza na bado anaongoza mapambano dhidi ya Utawala wa kimabavu wa China juu ya nchi yake ya Tibet, pia Askofu mkuu wa Manila Jaime Lachica Sin aliongoza mapinduzi nchini Ufilipino yajulikanayo "people power revolution" kumng'oa Dikteta Ferdinand Marcos na kumuweka madarakani Bibi Corazon Aquino baada ya mumewe aliyekuwa kiongozi wa upinzani Seneta Benigno Aquino Jr kuuawa na utawala wa Dikteta Jenerali Marcos.

Kwa mifano hiyo mchungaji Msigwa anawajibu wa kutetea haki za watanzania dhidi ya unyonyaji wa magamba ambao wanatakiwa kutoka madarakani haraka kabla nchi haijaharibika zaidi
 
asante mchungaji kwa darasa safi hw dd i mc this naamin utakuwa mfano kuwachunga hao kondoo ndani ya bunge
 
Da! Tanzania ina vichwa bwana why mh. Kikwete havitumii? Kweli tanzania tutaangamia wakati tuna rasilimali watu kama hawa. Cheki sasa walimu wenzangu wameanza kujichukulia chao mapema kwa wanafunzi (500). Huko mbeya "Survival for the fittest" kweli hii kitu iwekwe kwenye kumbukumbu. Leo hii habari naenda kufundishia shuleni kwa walimu na wanafunzi pia. Asante uliye irudisha tena.
 
Amenitoa machozi kuna watu watasaga meno juu ukatili wanaofanyia watu wa tsifa hili mchungaji ameongea kwa uchungu kabisa inasikitisha jamani magamba mmeshindwa ondokeni ama,
 
Ingawa ni maelezo marefu,si vibaya tukajikumbusha mambo haya kutoka kwenye Hansard za MKUTANO WA NANE

Kikao cha Tano – Tarehe 19 Juni, 2012

VIDEO:





MHE. MCH. PETER S. MSIGWA:

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuuambayo naipenda sana inayosema:-


"Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result"

ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona yaani uwendawazimu nikufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-"Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them". Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason, mahali ambapo tuna question na mahali ambapo tunatoka na solutions


is the opposite, binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupohapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika namamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabarambovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu zaWatanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo yakhanga!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulayakarne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwana fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofikakarne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hiikatika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania,tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamotozinazotukabili kama taifa.

Badala ya kukaa na kujiuliza kwa ninitupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongeangonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga,kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.

(Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamiaya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapalakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. JamesMadison mwaka 1822 alisema, "
knowledge forever will governignorance".

Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-governknowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge,tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hanatofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtumwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we takingthis nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha zaWatanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo yamsingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? Karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanzakudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi.

Pianinashangaa katika mpango wake wa bajeti taifa hili kamatunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma?

Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maanayake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wakoshuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sanakuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwasana. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wabajeti tulio nao hapa,
there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa.

Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wakivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatuamatatizo yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume niwengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini?

Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ilituwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto,ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusomashule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya,hauzungumzi.

Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifalimetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maananimesema problems can not be solved by the same level ofthinking that created them, you guys you are tired!

Kwasababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuwekakwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iwezekutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is theprinciple, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanityis keeping doing the same thing in the same way andexpecting different results and this is what we are doing.


Tunafanya hayohayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo.Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo nimatatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada yamwaka ni matatizo yaleyale,
why can't we think a little bitmore?

We can't stretch our brain a little bit more kama taifa?(Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengineambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoaushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekanawanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoamaamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business asusual. Ndugu zangu, where are we going? Where are weheading?

165

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tenakaribu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa,

they can notthink properly, they can not question, they can not ask.

Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwestretched ili uwezekuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapaduniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungenitunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bungela kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change

namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapakwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja.

Tuna mfumona traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi naulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwakuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala yakutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition

siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuriili na wewe utimize wajibu wako. (Makofi)



Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwakalinaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCMitaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo laSerikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kunammoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kamamtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa


I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya Wachungaji vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishaurihapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosemakama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanyemaombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo?

As aTheologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njiaza ku-produce zaidi, we don't pray for this, we don't have topray for this. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapatumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki nawanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewafedha bali wananchi wa Iringawamenichangua, wananiaminina ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitajikujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenyematatizo. Wehave to address this problems lakini siyo tunakujahapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watumnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili? (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba

niachie hapo. Ahsante sana. (Makofi)

Tukiacha U-Vyama hii Speech nadhan ndio the best Speech ever since Year 1900 pengine mpaka Year 3000.
 
Back
Top Bottom