Mbwembwe za nini Bwana, kwani huwezi kufanya kimyakimya?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,819
Mijitu mingine ikipata nyumba ndogo huanza mbwembwe kwa wake zao na ndugu na jamaa pia.
Utakuta mtu anaondoka nyumbani alfajiri, unarudi saa tisa usiku, shati limejaa ma lipstic, unarudi na harufu ya pafyum ya kike, na mbaya zaidi ndani una bikini NYEKUNDU, mkeo akikuuliza unakuja juu kinyama.
Hivi ni lazima ukiwa na nyumba ndogo uupigie baragumu ulimwengu?
 
umenena. Waeleza wamezidi, sijui ni ulimbukeni au sifa za kijinga. Wengine hadi matumizi yanasitishwa! Kisa nyumba ndogo
 
Ukiwa mkubwa utajua kunasaidia nini, kuvunja ndoa unadhani jambo rahisi?

Again. . . UNAFIKI.
Kama unaipenda/taka/thamini sana hiyo ndoa utatulia nayo badala ya kutoka nje huku ukijua kabisa ukigubdulika umekwisha.
 
Bora huyo anayeweka mambo hadharani ili mwenzie ajue ukimwi unamnyemelea, aweze kuchukua tahadhari kuliko yule wa kimya kimya....... Silent Killer!!!!!
 
hisia ki2 kingine wakuu. Kunakujkataza na kuzkana zsikuzid ila...,....
 
Bora huyo anayeweka mambo hadharani ili mwenzie ajue ukimwi unamnyemelea, aweze kuchukua tahadhari kuliko yule wa kimya kimya....... Silent Killer!!!!!

hahahahahah nimeipenda hii ina ukweli mwingi, swali ni je wanawake wangapi wenye uthubutu wa kuondoka wanapoona mume mzinzi kupitiliza? Wengi wanasubiri muujiza kuwa one day atabadilika
 
Naona sasa mambo ya nyumba ndogo yameshakubalika kwenye jamii ya Tanzania. Sasa sielewi kwa nini watu hutokwa na mapovu pindi wagunduapo kuwa wenza wao wanazo.
 
Kwasababu mkuki kwa binadamu mchungu zaidi ya klorokwini. Watu wakiwa na nyumba ndogo hua wanatangaza kwa sifa ila wakigundua wenzao nao wanao wananywea na kuanza kulia lia.
 
Heheheee kweli lakini!
 
Kwasababu mkuki kwa binadamu mchungu zaidi ya klorokwini. Watu wakiwa na nyumba ndogo hua wanatangaza kwa sifa ila wakigundua wenzao nao wanao wananywea na kuanza kulia lia.

Umesema kweli kabisa. Nyumba ndogo ukiianzisha hamna tatizo. Mwenzako naye akianza unakuwa mkali mbogo
 
Mijitu mingine ikipata nyumba ndogo huanza mbwembwe kwa wake zao na ndugu na jamaa pia.
Utakuta mtu anaondoka nyumbani alfajiri, unarudi saa tisa usiku, shati limejaa ma lipstic, unarudi na harufu ya pafyum ya kike, na mbaya zaidi ndani una bikini NYEKUNDU, mkeo akikuuliza unakuja juu kinyama.
Hivi ni lazima ukiwa na nyumba ndogo uupigie baragumu ulimwengu?

Ukiona hivyo basi ujue LIMBWATA limekolea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom