Mbwana Samatta

Shirikisho la Soka nchini (TFF) limesema kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta ni wa klabu ya Simba kwakuwa klabu hiyo ilifuata taratibu zote za uhamisho wake kutoka African Lyon mwanzoni mwa msimu uliomalizika.
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa kutokana na kumbukumbu walizo nazo, Samatta si mchezaji wa Lyon na kwamba Simba wana haki ya kumuuza.
Simba wameafiki kumuuza Samatta kwa mabingwa mara mbili mfululizo wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Osiah alitoa ufafanuzi huo kufuatia uongozi wa klabu ya Lyon kukaririwa ukidai kuwa wao (Lyon) ndio wamiliki halali wa mchezaji huyo na kwamba wanastahili kupokea fedha zote za usajili wa mchezaji huyo kutoka TP Mazembe.
"Simba walifuata taratibu zote za kumsajili Samatta kutoka Africa Lyon na ndio maana TFF ilimuidhinisha mchezaji huyo kuichezea Simba katika msimu uliomalizika," alisema Osiah.
Alisema kuwa hata kama kuna malipo kwa mchezaji au klabu hiyo hayajakamilishwa na Simba, bado jambo hilo haliwezi kuifanya TFF ione kwamba Samatta ni wa Lyon.
Simba imeripotiwa kumuuza mchezaji huyo Mazembe kwa ada ya uhamisho wa dola za Marekani 100,000 ambazo ni sawa na Sh. Milioni 150.
Baada ya kusajiliwa na Simba akitokea Lyon mwanzoni mwa msimu ulioisha, Samatta aligoma kuichezea klabu hiyo ya Msimbazi hadi alipotimiziwa sharti la mkataba wake la kupewa gari.
 
Kwani simba wao hawataki wachezaji wazuri?
Kwanini wamuuze Samata wakati huyo ndie mchezaji kinara wa simba
kwani manu ilimuuza Ronaldo kwenda Real.....Mpira ni biashara kama hujui, unauza unanuanua na unatengegeneza wengine....mfano hizo mil 150 zitanunua akina samatta wangapi?
 
Simba ipo tofauti sana na Yanga, kwao kuuza wachezaji si ishu, wanajua watawapata wap!
 
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti wa Leo mshambualiaji chipukizi wa Simba na ambaye anakamilisha taratibu za kusajiliwa TP Mazembe kwa dau la TZS 270m anatakiwa na timu za Villacher Sportverein inayocheza ligi kuu Austria na timu ya Stabaek inayocheza ligi kuu Norway.

Villacher ambao wako kwenye nafasi nzuri ya kucheza either UEFA Champions League au Europa League mwakani wanamtaka Sumatta kwa €200m sawa na karibu TZS 500m.

Pia club kongwe ya Ureno ya Sporting Lisbon alipootoke Christiano Ronaldo inamtaka pia akafanye majaribio nao.

Pia kwa mujibu wa mwanasheria wa Samatta club ya TP Mazembe imeombwa kutuma mkataba wa mchezaji huyo toko April 16 mpaka leo hawajatuma. TP Mazembe wanataka kumsainisha Samatta mkataba wa miaka 5 wakati kwa mujibu wa sheria za FIFA mchezaji wa umri wake anatakiwa asaini mkataba usiozidi miaka mitatu.

Hii ni fursa nzuri kwa mchezaji watu ila awe makini kufanya chaguo sahihi kwa manufaa yake na Taifa kwa ujumla.
 
Mwanasheria amemshauri asikubali kusign contract mpaka aupitie mkataba ambao mpaka sasa TP Mazembe hawajatua, Simba watamsend kufanya majaribio if deal ya Mazembe itaendelea kuwa kwikwi
 
Nyota ya Samatta yang'ara, GO...GO...GO ON YOUNG MAN BUT BE SMART.
 
Mbwana wala TFF hata Taifa kwa Ujumla hakuna aliye win. Mkataba wa dola laki moja kwa miaka mitano kama ni kweli ni UMBUMBUMBU. Labda kama kuna viongozi wamepiga ka ufisadi. Mikataba mizuri maximum ni miaka miwili.

Kwa samatta, mkataba wa miaka mitano zinatakiwa zilipwe bilioni walao tatu hivi. Miaka mitano ni jela na hako katoto kana uwezo wa kucheza ulaya kwa bei mbaya.
 
Na Zahoro Mlanzi

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mbwana Samatta nyota yake inazidi kung'ara baada ya Klabu yake mpya ya TP Mazembe kumpeleka kufanya majaribio katika
timu za Arsenal ya Uingereza na Anderletch ya Ubelgiji Desemba mwaka huu.

Samatta ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', alisaini mkataba wa miaka mitano hivi karibu wenye thamani ya sh. mil. 150 na mabingwa wa hao wa Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mlezi na Mshauri wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema wameshamalizana na TP Mazembe na sasa Samatta ni mchezaji halali wa mabingwa hao wa Afrika.

"Namshukuru Mungu safari ilikuwa ya mafanikio na tumerudi salama, rafiki zetu walitupokea vizuri wakiongozwa na Mwenyekiti, Katanga Musa Katumbi na Meneja, Fredrick ambapo tulisaini mkataba bila matatizo yoyote," alisema Kasongo.

Alisema wamesaini mkataba wa miaka mitano, ambao kila baada ya miaka miwili lazima wakae tena chini kuzungumza ambapo pia suala la marupurupu limeachwa kutokana na timu hiyo kutoa marupurupu mengi kwa wachezaji wake.

Kasongo alisema mbali na kukamilisha suala hilo, pia klabu hiyo imewaambia wana mkataba na timu za Arsenal na Anderletch ambapo kila mwaka hupeleka wachezaji wanane kwenda kufanya majaribio na kwa mwaka huu, Samatta ni miongoni mwa wachezaji watakaokwenda huko.

"Unajua TP Mazembe wana mkataba na Arsenal na Anderltch wa kupelekeana wachezaji kufanya majaribio, Samatta atakwenda huko na atakaa kwa muda fulani na klabu hizo zikivutiwa na kiwango chake, yeye mwenyewe ndiye atakayeamua klabu atakaoichezea," alisema Kasongo.

Wakati huo huo, Kisongo alisema timu hiyo inatoa marupurupu ya kutosha kwa wachezaji wake ndiyo maana wachezaji wengi wanashindwa kwenda kucheza Ulaya kutokana na fedha za ziada wanazozipata.

Alisema timu hiyo hupewa maslahi makubwa, jambo ambalo linazidi hata mishahara wanayopata na ndiyo maana klabu nyingi za Ulaya zinashindwa kuchukua mchezaji kutoka katika timu hiyo.
 
Hi habari siyo sahihi kama ingelikuwa ni sahihi basi TP MAzembe isingekuwa inapeleka wachezaji wake ulaya ila timu za ulaya ndizo zingekuwa zinapeleka wachezaji wake TP Mazembe......................
 
Hi habari siyo sahihi kama ingelikuwa ni sahihi basi TP MAzembe isingekuwa inapeleka wachezaji wake ulaya ila timu za ulaya ndizo zingekuwa zinapeleka wachezaji wake TP Mazembe......................
hi habari ni sahihi kabisa bila hata doa,kama uanifuatilia sana timu ya TP MAZEMBE ungekuwa unalijua hili.
 
Naamini huyu dogo atafika mbali sana kisoka kwa sababu ana uwezo mkubwa, anajiamini na umri wake bado ni mdogo. Kwa mara ya kwanza nilimuona kwenye mechi baina ya Simba na African Lion msimu mmoja kabla hajahamia Simba.

Aliwasumbua sana mabeki wa Simba, wakati huo wakiongozwa na beki imara sana aitwaye Joseph Owino. Ndiye mchezaji pekee aliyenivutia kwa upande wa Lyon na nilipouliza jina lake, jamaa wakaniambia anaitwa Mbwana Samatta. Nilijisemea siku ile kwamba huyu kijana ana very bright future kwenye soka.

Namtakia kila la kheri.
 
Habari njema bora ulaya kwa maslahi kidogo kuliko maslahi makubwa T P Mazembe ambayo hayakufanyi ukutane na changamoto nyingi maishani,hakuna jipya la kijifunza hata kina Etoo wangeweza kucheza Mazembe lakini hakuna jipya.
 
Hi habari siyo sahihi kama ingelikuwa ni sahihi basi TP MAzembe isingekuwa inapeleka wachezaji wake ulaya ila timu za ulaya ndizo zingekuwa zinapeleka wachezaji wake TP Mazembe......................
Sio kweli mkuu,
Kuna wachezaji wanatoka Portugal na wanakuja kucheza TP Mazembe kwa mkopo, hawa jamaa wapo vizuri na makini.
 
Na Zahoro Mlanzi

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mbwana Samatta nyota yake inazidi kung'ara baada ya Klabu yake mpya ya TP Mazembe kumpeleka kufanya majaribio katika timu za Arsenal ya Uingereza na Anderletch ya Ubelgiji Desemba mwaka huu.

Samatta ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', alisaini mkataba wa miaka mitano hivi karibu wenye thamani ya sh. mil. 150 na mabingwa wa hao wa Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mlezi na Mshauri wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema wameshamalizana na TP Mazembe na sasa Samatta ni mchezaji halali wa mabingwa hao wa Afrika.

"Namshukuru Mungu safari ilikuwa ya mafanikio na tumerudi salama, rafiki zetu walitupokea vizuri wakiongozwa na Mwenyekiti, Katanga Musa Katumbi na Meneja, Fredrick ambapo tulisaini mkataba bila matatizo yoyote," alisema Kasongo.

Alisema wamesaini mkataba wa miaka mitano, ambao kila baada ya miaka miwili lazima wakae tena chini kuzungumza ambapo pia suala la marupurupu limeachwa kutokana na timu hiyo kutoa marupurupu mengi kwa wachezaji wake.

Kasongo alisema mbali na kukamilisha suala hilo, pia klabu hiyo imewaambia wana mkataba na timu za Arsenal na Anderletch ambapo kila mwaka hupeleka wachezaji wanane kwenda kufanya majaribio na kwa mwaka huu, Samatta ni miongoni mwa wachezaji watakaokwenda huko.

"Unajua TP Mazembe wana mkataba na Arsenal na Anderltch wa kupelekeana wachezaji kufanya majaribio, Samatta atakwenda huko na atakaa kwa muda fulani na klabu hizo zikivutiwa na kiwango chake, yeye mwenyewe ndiye atakayeamua klabu atakaoichezea," alisema Kasongo.

Wakati huo huo, Kisongo alisema timu hiyo inatoa marupurupu ya kutosha kwa wachezaji wake ndiyo maana wachezaji wengi wanashindwa kwenda kucheza Ulaya kutokana na fedha za ziada wanazozipata.

Alisema timu hiyo hupewa maslahi makubwa, jambo ambalo linazidi hata mishahara wanayopata na ndiyo maana klabu nyingi za Ulaya zinashindwa kuchukua mchezaji kutoka katika timu hiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom