Mbuzi wa miguu minane azaliwa Dodoma

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
Na Danson Kaijage,
Chamwino

MBUZI wa ajabu amezaliwa
katika mkesha wa kuamkia
mwaka mpya 2012 akiwa na
miguu minane na mikia
miwili. Mnyama huyo wa ajabu
alizaliwa katika kijiji cha
Manchali, kata ya Manchali,
wilayani Chamwino, akiwa
mzima lakini akafa baada ya
masaa matatu. Mmiliki wa mbuzi huyo,
Christopher Chipene, alisema
hiyo ilikuwa mara ya nne kwa
mbuzi wake kuzaa ambapo
katika awamu tatu za awali
alizaa ndama wazima bila ya matatizo. Tukio hilo ni la pili katika
familia ya Chipene ambaye
amekiri kwamba katika siku
za nyuma binti yake
alijifungua mtoto mwenye
mwili wa plastiki badala ya ngozi, japo mtoto aliyezaliwa
alifariki baada saa chache. Naye Ofisa Mtendaji wa Kata
ya Manchali, Amos Songo, na
Ofisa Kilimo na Mifugo wa
Kata Lista Ngimbwa walisema
hilo ni tukio la ajabu na la
kwanza kutokea katika kata hiyo.

Chanzo:TANZANIA DAIMA
 
Back
Top Bottom