Mbuzi wa Kafara

654

Senior Member
Feb 1, 2012
172
40
Wakuu,
Nimekuwa nafuatilia kwa karibu haya maendeleo ya mageuzi katika nchi yetu, kwa muda mrefu wengi wetu tumekuwa na dhana inayoelekea kuamini kuwa Mkuu wa Nchi plae jengoni, amekuwa 'catalyst' kama sio chanzo cha uozo mwingi unaojitokeza katika jamii yetu.
Kwa mfano, wale tuliosoma makala ya Jenerali Ulimwengu juu ya ofisi ya Waziri Mkuu, katika makala ya hivi karibuni tunatambua kuwa hali ni tete! na kama hatua madhubuti za makusudi hazitachukuliwa kila siku, sio tu ofisi ya CAG inapaswa kufungwa, ya Waziri Mkuu na hata Mjengo.
Sasa, je nikweli kuwa JK amekuwa Mbuzi wa kafara, baada ya kuridhi uozo wa wale waliomtangulia, akiwama marehemu JKN? Nawasilisha argument ifuatayo ili iangaliwe japo kwa uchache.
'Kikwete ametolewa mbuzi wa Muhanga ,kila mtu anajuwa toka enzi za Julius Nyerere kama Nchi haiendi mbele kila siku inarudi nyuma.
Nani alievunja mashamba ya mkonge , viwanda vya chuma ,urafiki,kiltex,mwatex,sunguratex ,bora shoes ,Kikwete ?
Viko wapi leo viwanda vyote kule Tanga na Dar,? Nani kauwa Sukita ? Jee kuna Waziri yoyote alijiuzulu kwa kuuwa uchumi wa Tanzania tangu tupate Uhuru ? Kuna mtu yoyote aliejuwa Almasi na Dhahabu iliokuwa ikipatikana wakati wa Mwalimu? TANI NGAPI ZILIPATIKANA KWA MUDA WOTE ALIOKAA MADARAKANI ?
Kikwete pole baba kamba imekatikia pabovu kwa hiyo lawama zote unapewa wewe. Lakini wote hao watajibu jinsi wanavyo kukandia siku ya hukumu ya kweli ikifika.'
 
Ni sahihi mkuu... Afadhali kipindi cha JK maisha yana unafuu kuliko kipindi cha JKN. Zama zile tulikuwa tunapanga foleni ya kupata kipande cha mkate. JK amerithi maoza ya watangulizi wake
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu na si vinginevyo!
-ni kweli kwamba kikwete amerithi maovu ya waliomtangulia na kwamba analaumika kwayo!
-ni kweli kwamba yapo baadhi ya mambo mazuri aliyofanya kikwete ktk utawala wake
-kinachompata leo kikwete ni stahiki yake, kwani kaomba madaraka kwa lengo la kurekebisha makosa na kuendeleza mazuri. Hapaswi kusifiwa kwa mazuri yake kwani huo ndio wajibu wake bali kusemwa kwa mabaya iwe kayakuta ama kayafanya!!
 
Ni sahihi mkuu... Afadhali kipindi cha JK maisha yana unafuu kuliko kipindi cha JKN. Zama zile tulikuwa tunapanga foleni ya kupata kipande cha mkate. JK amerithi maoza ya watangulizi wake

Niambie ubora uliopo leo kulinganisha utawala wa awamu ya kwanza bearing in mind the following:
1. Kipindi cha uhaba wa vitu enzi ya Nyerere ilikuwa just after the war (leo hii hakuna vita lakini tumeshuhudia mgao wa sukari)

2. Elimu ilikuwa bure hadi elimu ya juu, leo vipi?

3. Hakukuwa na mgao wa umeme, reli zote zilikuwa zinafanya kazi

Mambo yako mengi ya kutofautisha.

Haya, niambie ubora wa maisha uliopo leo hii ni upi? Kikwete hana uwezo wa kuongoza, plain simple! Hakuna cha mbuzi wa kafara wala nini, he is incompetent!
 
Je fedha zote zinazoliwa kwenye mikataba feki,utalii,elimu,halmashauri kwa ujumla,miundo mbinu,kilimo Jk na timu yake wangezisimamia vizuri tusingesong mbele? Mi naona visitafutwe visingizio.
 
Je fedha zote zinazoliwa kwenye mikataba feki,utalii,elimu,halmashauri kwa ujumla,miundo mbinu,kilimo Jk na timu yake wangezisimamia vizuri tusingesong mbele? Mi naona visitafutwe visingizio.

Nafurahia ulivyoiweka Di.. - kama kulikuwa na uozo basi ukiomba kazi hiyo ina maana unajiamini kuwa wewe ndiyo utakayeweza kuu rekebisha. Itashangaza utakapo anza kutuaambia kulikuwa na uozo.. mtoa mada anachezea uwezo wetu wa kufikiri ..pls this is a great thinkers forum not wazee wa ....
 
kuna kazi kubwa kumtetea kikwete,pole zikuendee wewe uliyeamua kubeba hilo jukumu
 
Hatutaki precedence hata kama kuna wengine walikosea. Tupo 2012!

Big up, Mkuu!!!

JK alikuta hazina imenona, hella zote kazifuja kwa kupenda anasa kwake!! Mara semina elekezi, safari za nje zisizo na idadi na zenye kuwa na watu wengi sana, baraza la mawaziri kubwa na lisilo na tija kwa nchi kwa sababu limejaa watu wasioweza chochote, etc, etc.

Mbona Mkapa hakulaumiwa kama anavyolaumiwa JK???

JK ni janga la taifa na adui mkubwa wa nchi hii kuliko magonjwa!!
 
Wakuu,
Nimekuwa nafuatilia kwa karibu haya maendeleo ya mageuzi katika nchi yetu, kwa muda mrefu wengi wetu tumekuwa na dhana inayoelekea kuamini kuwa Mkuu wa Nchi plae jengoni, amekuwa 'catalyst' kama sio chanzo cha uozo mwingi unaojitokeza katika jamii yetu.
Kwa mfano, wale tuliosoma makala ya Jenerali Ulimwengu juu ya ofisi ya Waziri Mkuu, katika makala ya hivi karibuni tunatambua kuwa hali ni tete! na kama hatua madhubuti za makusudi hazitachukuliwa kila siku, sio tu ofisi ya CAG inapaswa kufungwa, ya Waziri Mkuu na hata Mjengo.
Sasa, je nikweli kuwa JK amekuwa Mbuzi wa kafara, baada ya kuridhi uozo wa wale waliomtangulia, akiwama marehemu JKN? Nawasilisha argument ifuatayo ili iangaliwe japo kwa uchache.
'Kikwete ametolewa mbuzi wa Muhanga ,kila mtu anajuwa toka enzi za Julius Nyerere kama Nchi haiendi mbele kila siku inarudi nyuma.
Nani alievunja mashamba ya mkonge , viwanda vya chuma ,urafiki,kiltex,mwatex,sunguratex ,bora shoes ,Kikwete ?
Viko wapi leo viwanda vyote kule Tanga na Dar,? Nani kauwa Sukita ? Jee kuna Waziri yoyote alijiuzulu kwa kuuwa uchumi wa Tanzania tangu tupate Uhuru ? Kuna mtu yoyote aliejuwa Almasi na Dhahabu iliokuwa ikipatikana wakati wa Mwalimu? TANI NGAPI ZILIPATIKANA KWA MUDA WOTE ALIOKAA MADARAKANI ?
Kikwete pole baba kamba imekatikia pabovu kwa hiyo lawama zote unapewa wewe. Lakini wote hao watajibu jinsi wanavyo kukandia siku ya hukumu ya kweli ikifika.'

Hakuna aliyemtoa Kikwete mbuzi wa kafara. Yeye mwenyewe amekuwa na tamaa ya madaraka ili

hali akijua hana uwezo wa kuongoza. Kumbuka aliomba toka mwaka 1995! Alipoingia aliahidi

kuleta mabadiliko makubwa! Amekuwa akifanya nini kama sio kwenda nje ya nchi? Ametolea

kafara gani wakati all the resources anazo? Lets see

1. Over 40million human resource

2. Plenty of virgin land full of mineral and fertility

3. Lots of tourists attractions

4. Abundant mass of water

5.Good will as found in the name of the nation

6. All forces are under his command

7. He leads the cabinet which decides how the country's money should be spent!

Alichofanikiwa mpaka sasa ametuongezea deni la taifa to 14 trillions! Usiseme ametolewa

kafara! Kwani ye ndo raisi peke yake duniani aliyerithi nchi ikiwa na matatizo? Ushaniudhi

kwanza!
 
Back
Top Bottom