Mbunifu wa mavazi Amina design atoa mada kuhusu faida za ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83

Mbunifu wa Mavazi Amina Plummer Akitoa Mada kwenye Semiana ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Zanzibar yenye Lengo la Kuwafundisha Mbinu Mbalimbali za Biashara pamoja na Matumizi Sahihi ya Vipodozi Pendwa vya Luvtouch.

Mbunifu wa mavazi Amina Plummer amewaasa wanawake wa Zanzibar kujikita kwenye ujasiriamali kwa kuwa ndio njia pekee ya kumkomboa mwanamke amesema ajira nyingi zimekuwa na ubaguzi na pili ni nafasi chache sana zinatolewa kwa wanawake hivyo basi wanawake hawana budi kujikomboa kwa njia ya ujasiriamali mama Amina alisema hayo wakati akitoa mada alipowatembelea wanawake wa zanzibar walioniufaika na mradi wa manjano dream makers ulio chini ya taasisi ya manjano foundation yaliomalizika kwenye hotel ya mtoni marine Zanzibar.

Mbunifu wa mavazi Amina Design akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Pamoja wa Baadhi ya wasaidizi Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.

Akieleza Zaidi Mama Amina Plummer Ambaye ni Mbunifu wa Mavazi amewaomba wanawake wa Zanzibar Kupenda Ujasiriamali kwa Kuwa ni Kazi Pekee ambayo kadiri Unavyoifanya kwa Juhudi na Maarifa Pia inasaidia Kuongezeka kwa Kipato cahako.Hivyo wakina mama wa Zanzibar hawana Budi Kuchangamkia nafasi hiyo ya kujifunza Ujasiriamali Kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation .


Washiriki wa Semina Hiyo kutoka Visiwani Zanzibar wakisikiliza kwa Makini Mda zilizokuwa zikitolewa kwenye Mafunzo hayo.
 
Back
Top Bottom