Mbunge wa Ukonga yuko wapi?

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Nasikitikia wakazi wa Ukonga hasa wanaopitia barabara inayoanzia Mombasa kuelekea moshi bar hadi kwa Mkolemba maana barabara ni mbovu sijawahi ona pamoja na kuwa serikari imekuwa ikivuna kodi katika machinjio ya Mazizini kwa miongo mingi sasa.Nakumbuka Kikwete katika kampeni zake alidai ndani ya siku 100 barabara itakuwa imekamilika,Swali la kujiuliza hizo siku 100 hazijafikia tangu aingie madarakani? Wale mlio karibu na Mbunge wa Ukonga mkumbusheni Siku zinasonga na watu ni walewale.:smow::smow::smow::smow::smow::smow:
 
Mkuu kwa kweli umenigusa sana na thread yako. Binafsi nakaa maeneo ya kipunguni. The shortest possible road ya kufika nyumbani kwangu ni kupitia barabara hiyo ( Sidhani kama ni sahihi kuitwa barabara!!!!!), lakini huwa nalazimika kupitia barabara ya kitunda. Wakati fulani huwa najiuliza, hivi hawa wabunge wanajua hata geographical area ya maeneo yao????. Ile barabara ina urefu kama wa 5km kutoka mombasa mpaka Moshi bar, lakini una -drive kwa karibu nusu saa kipande kifupi kama hicho kwa sababu ya mahandaki yaliyopo. Labda usemi kuwa ukiwa Dsm, ukitaka kutafuta eneo la kujenga, tafuta wakati wa masika. By the way Kikwete anajua kweli kama kuna raia tunaishi huko!! sidhani. By the way huyo mbunge yupo hai, maana simsikii!!!!
 
wabunge wamebaki wachache sana wenye uchungu na raia
wengine wote wahuni tu na sie tunazidi wapigia kura hao wahuni!!
 
Nasikitikia wakazi wa Ukonga hasa wanaopitia barabara inayoanzia Mombasa kuelekea moshi bar hadi kwa Mkolemba maana barabara ni mbovu sijawahi ona pamoja na kuwa serikari imekuwa ikivuna kodi katika machinjio ya Mazizini kwa miongo mingi sasa.Nakumbuka Kikwete katika kampeni zake alidai ndani ya siku 100 barabara itakuwa imekamilika,Swali la kujiuliza hizo siku 100 hazijafikia tangu aingie madarakani? Wale mlio karibu na Mbunge wa Ukonga mkumbusheni Siku zinasonga na watu ni walewale.:smow::smow::smow::smow::smow::smow:
Pole sana, utamuona uchanguzi ukikaribia..
 
Hivi anaitwa nanai?:mod:

Anaitwa Eugene Mwaiposa;akichukua jina la ukoo la mme wake Ally Mwaiposa ambaye baba yake alikuwa shehe wa Wilaya ya Kyela;wana ndoa hawa walikutana walipokuwa masomoni miaka ya 90 kule Bulgaria!

Kwake ni Kipunguni B kama unatokea uchochoro wa Chadibwa;hata mimi ni Mbunge wangu lkn mhhh!
 
Aliyewaambia mbunge ana uwezo wa kujenga hiyo barabara nani? Kazi yao ni kupigia kelele tu. Ombeni katiba mpya iwape mamlaka hayo!
 
nasikitikia wakazi wa ukonga hasa wanaopitia barabara inayoanzia mombasa kuelekea moshi bar hadi kwa mkolemba maana barabara ni mbovu sijawahi ona pamoja na kuwa serikari imekuwa ikivuna kodi katika machinjio ya mazizini kwa miongo mingi sasa.nakumbuka kikwete katika kampeni zake alidai ndani ya siku 100 barabara itakuwa imekamilika,swali la kujiuliza hizo siku 100 hazijafikia tangu aingie madarakani? Wale mlio karibu na mbunge wa ukonga mkumbusheni siku zinasonga na watu ni walewale.:smow::smow::smow::smow::smow::smow:

mwenzio kila siku kwake ya 99 mia aifiki hata sikumoja siku utakapomwona lowassa kapewa nchi ujue ya mia imefika kwake
 
Kwani pale airport junction via majumba 6 mpaka banana...mbunge wa kipande hicho ni nani?
Maana napo pale ni issue, mkandarasi anakaribia kufikisha nusu mwaka kwa kipande hicho cha kwanza, sijui atafika lini chanika.
 
Nadhani watu wa ukonga tuache kulalama bali tusherehekee CCM ilishinda tena kwa kura nyingi.. swali, Ni sie tuliowapigia CCM kura au sio sisi? Binafsi nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanaipinga CCM japo kwa jimbo letu lililo nyuma kimaendeleo pengine hata na baadhi ya vijiji. Nilihuzunika sana kuona CCM inazoa kura nyingi tena mbunge huyo mchovu akishinda kwa asilimia kubwa...Hebu tafakari Kawe (CDM), Ubungo (CDM) haya ni majimbo yenye maendeleo mara 100 kupita ukonga sasa jamani tunalalamika nini??? Suluhisho... chagua CDM ili mbunge akapambane kudai haki yetu fullstop
 
mchuma janga(mpiga kura) hula na wakwao (ccm+nyinyi wapiga kura) sema ratio ya kula hili janga inaatofautiana kwa sababu kuna wengine linawapiga sana kuliko wenzao!!!!!! so guys mmeichagua ccm you have to reap your sweets fruits
 
Nasikitikia wakazi wa Ukonga hasa wanaopitia barabara inayoanzia Mombasa kuelekea moshi bar hadi kwa Mkolemba maana barabara ni mbovu sijawahi ona pamoja na kuwa serikari imekuwa ikivuna kodi katika machinjio ya Mazizini kwa miongo mingi sasa.Nakumbuka Kikwete katika kampeni zake alidai ndani ya siku 100 barabara itakuwa imekamilika,Swali la kujiuliza hizo siku 100 hazijafikia tangu aingie madarakani? Wale mlio karibu na Mbunge wa Ukonga mkumbusheni Siku zinasonga na watu ni walewale.:smow::smow::smow::smow::smow::smow:

Kazi inaanza rasmi baada ya semina elekezi; anza kuhesabu kuanzia hitimisho la semina elekezi kwani ndio watendaji wanapata maelekezo rasmi nini wafanye sehemu zao za kazi; au naongopa?
 
Tehe tehe, Mh Mbunge anasubiri semina elekeze, ataanzaje kupiga kelele kuhusu barabara wakati serikali iliyopo madarakani ni ya chama chake, na ni sharti kuiunga mkono. Goja utamuona mwaka 2014 atakapokuja kuongea na wananchi lengo likiwa ni kufahamiana na kuweka mikakati ya 2015-2020.
Kuvumilia ni sehemu ya maisha lakini kuvumilia uvundo ni kero. Poleni sana, ndo kwanza mwaka wa 1 kati ya 5, kero kweli kweli.
Elimisha mtu kwa mtu, mtaani kwako ili ifikapo 2015 ukombozi uwajiliye.
 
Next time mjipange kumpigia mbunge ambaye anaweza kuwatetea,wabunge wanaopinga mazuri kwa wananchi kwa mfano wa chama kongwe hakuna sababu ya kuwachagua,hiyo ndiyo athari ya siasa kwenye maisha kwa wale ambao hata kujiandikisha au kupiga kura siyo dili
Jamaa moja wkt wa uchaguzi alinikera aliponiambia siasa hainisaidii kitu chochote,kwake kupiga kura ni kupoteza mda
 
Nasikitikia wakazi wa Ukonga hasa wanaopitia barabara inayoanzia Mombasa kuelekea moshi bar hadi kwa Mkolemba maana barabara ni mbovu sijawahi ona pamoja na kuwa serikari imekuwa ikivuna kodi katika machinjio ya Mazizini kwa miongo mingi sasa.Nakumbuka Kikwete katika kampeni zake alidai ndani ya siku 100 barabara itakuwa imekamilika,Swali la kujiuliza hizo siku 100 hazijafikia tangu aingie madarakani? Wale mlio karibu na Mbunge wa Ukonga mkumbusheni Siku zinasonga na watu ni walewale.:smow::smow::smow::smow::smow::smow:

Mimi nilivyoiona Avatar yako nikasahau kuendelea kusoma.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom