Mbunge wa Ubungo John Mnyika anyimwa na polisi kufanya mkutano

Mbunge anataka kuongea na wapiga kura wake inakuwa longolongo ghrrrrrrrrrrrrrr...
 
Na mawasiliano ya cm bila barua wataproove vipi kuwa ni Polisi, hawawezi kuwa wanazi wa CCM?
 
My worry! Siku moja tutaua makusudi raia wa tanzania kwenye mikutano hii kwa kuwasingizia al shabaab ili tupate sababu nyepesi ya kuzuia wananchi kuhuzuria mikutano inayoitishwa na CDM. Ole wake yule atakayeinua silaha na kutoa roho ya mtanzania ktk mikutano ya kiharakati!
 
jeshi la posili linajidhalilisha sana. Ina maana hawana uwezo wa kutunga uongo mwingine zaidi ya alshabab!!! Copy and paste?
 
mkutano umefanyika kama kawa na mimi nilikuwepo hapakuwa na alshabab wala alsha bibi, polisi wameona haya. sasa mbunge ameelekea kituo cha polisi kuwachukua viongozi waliokamatwa sijui kama atarudi wanaweza kumtia ndani wale kwani ameongozana na baadhi ya vijana walio jaa fuso moja, watasingizia kuwa chadema wamevamia kituo cha polisi.
 
Polisi walifika eneo la Mkutano,mkabala na Kituo cha Mabasi Ubungo-mbele ya Yenu Bar wakiwa na OCD wa Kimara,Afande Mambo Sasa! Wamekamata gari la Mbunge lililokuwa na vifaa vya kupaza sauti,wamekamata na viongozi wa chama jimbo la Ubungo.Pia wamechukua vitabu vya "muongozo wa Katiba", "Katiba" na nyaraka nyingine ambazo Mbunge Mnyika alikuwa amepanga kuvigawa kwa wananchi.

Mnyika alipo wasili tu nao wakaondoka kwa kasi. Mbunge Mnyika alipatiwa kipaza sauti na wafanya biashara wadogo wadogo eneo la tukio na kuhutubia.

Kwa sasa,yeye pamoja na wananchi wanaelekea ktk Kituo cha Polisi,Mbezi kwa Yusuf ambapo anaenda kufatilia hatma ya viongozi waliokamatwa na vifaa vyote!!

Nawasilisha.
 
Viongozi waliokamatwa: Diwani wa Kata ya Saranga (Alphonce Kinyafu), Katibu Mwenezi Chadema Jimbo(Ally Makwilo), Dereva Mbaga(gari ya Mbunge)!!
 
hivi kati ya hao al shabaab na mafisadi nani hatari?make sa hivi hamna huduma za jamii na watu wanakufa a polisi wanawajua mafisadi lakini wanakula nao na kupeana mikakati ya kuiangamiza chadema japo nasema hawataweza
 
Kinachofata chadema tuanze kulipa visasi kwa jeshi la polisi na CCM.....
 
POLISI WAWAKAMATA VIONGOZI WA CHADEMA NA KUSHIKILIA VYOMBO VYAO

Baada ya Polisi kupiga marufuku mkutano wa Mbunge wa Ubungo kwa kutumia simu. Wamewakamata viongozi wa CHADEMA na Vyombo vya sauti vya mkutano, nyaraka za chama, vipeperushi, copy za muswada wa mabadiliko ya katiba na katiba za 1977 ambavyo alikuwa awagawie wananchi.

Hata hivyo wafanyabiashara wameokoa jahazi kwa kumpa Mbunge vipaza sauti ili aendelee na mkutano na alifanya hivyo.

Wanachama wengine wameenda kuwatoa viongozi walioshikiliwa na Polisi
 
Elezea vizuri mkuu? waliokamatwa ni kina nani? pamoja na Mnyika? Watachukuaje vyombo alafu mkutano ukaendelea?
 
Polisi wa Urafiki vp? Sisi huku Kilungule na king'ong'o mpaka msakuzi hata bia hatunywi majambazi nje nje hawaji kuwakamata wanahangaika na wahubiri...?

Wangeanza na madereva wakorofi hapo Ubungo na machinga wanaoziba njia na vibaka pale Songas darajani tungewaelewa
 
POLISI WAWAKAMATA VIONGOZI WA CHADEMA NA KUSHIKILIA VYOMBO VYAO

Baada ya Polisi kupiga marufuku mkutano wa Mbunge wa Ubungo kwa kutumia simu. Wamewakamata viongozi wa CHADEMA na Vyombo vya sauti vya mkutano, nyaraka za chama, vipeperushi, copy za muswada wa mabadiliko ya katiba na katiba za 1977 ambavyo alikuwa awagawie wananchi.

Hata hivyo wafanyabiashara wameokoa jahazi kwa kumpa Mbunge vipaza sauti ili aendelee na mkutano na alifanya hivyo.

Wanachama wengine wameenda kuwatoa viongozi walioshikiliwa na Polisi

Zamani nilikuwaga najiuliza mara mia mia kwa nini qualification za kujiunga na polisi ni division four either na credit moja au with no credit? Kumbe kulikuwa na maana kubwa sana katika hili! Kwanza ni mtu ambaye kielimu hasongi mbele tena kirahisi, lakini pia uelewa wake unakuwa umetafsiriwa na matokeo hivyo akishapewa kazi anaweza kutumiwa kama robot machine! Kwa taarifa yako ni kwamba kati ya watanzania wanofanyishwa kazi ngumu na maslahi ni duni ni hawa jamaa lakini wanajiona kama wako peponi vile! Pitia quarter zao uone maisha yao kuanzia nje mpaka ndani ya nyumba zao kama unaroho ndogo unaweza kuzimia kwa muda lakini bado wanatumiwa na wao wanatumika.
 
Kweli wamekosa kazi za kuzifanya!! Loh! Kodi yangu inaenda bure..
 
Back
Top Bottom