Scolari Ndenga
JF-Expert Member
- Aug 4, 2008
- 271
- 43
Kwa mujibu wa status katika facebook wall ya John Mnyika muda mchache uliopita ametoa taarifa ya Uongozi wa Chadema Jimbo la Ubungo kupokea simu toka Jeshi la Polisi yenye kumzuia kufanya mkutano ambao ilikuwa auanze kuufanya mnamo saa kumi kamili alasiri eneo la uwanja wa Yenu Bar mkabala na Kituo cha Mabasi-Ubungo.
Mnyika, ametoa msimamo wa kuendelea na mkutano huo sambamba na mikutano mingine yote aliyokuwa amepanga kuifanya kwani hajapatiwa taarifa kwa maandishi.
Alisema katika status yake hiyo kuwa Jeshi la Polisi lilishapatiwa taarifa mnamo tarehe 3 na kukumbushwa tarehe 4 ya mwezi huu, (Novemba), 2011 bila ya wao kutoa majibu yoyote.