Mbunge wa Tarime aongea pumba ITV, kumekucha

Ana sema ugomvi mkubwa wawatu wa tarime ni ardhi na ugomvi wa juzi ulisababishwa na chama fulani ambacho kilidhani kina hati miliki ya Tarime!
Yeye ndiye asiyetakiwa Tarime, hakuchanguliwa na wananchi alichakachua matokea na ndiyo maana anapigwa, hata Nyamwaga anaposema kwao haendi. Wabunge wa CDM wanatakiwa kuja kutetea haki za wananchi. Hatutaki vihiyo wa ccm hata kujieleza hawezi I wonder how he became MP !!!!
 
sasa yeye ndio mbunge wa kule na anajua kinachoendelea. wewe pengine hata hujawahi kukanyga huko tarime unambishia na kuita alichoongea pumba, unadhani kati yake na wewe nani mwendawazimu >?? wewe hapo
we bwe.ge nini? Unadhani waliompigia kura huyo Mbunge ni wakurya tu? Pelekeni pumba zenu za ubaguzi kwenye vikao vyenu vya kuvuana magamba. Au hujui kila raia wa Tanzania yupo huru kuishi popote?
 
Na kuongezea tu ni kwamba Massawe (mtata) anaagiza au anasimamia agizo kuwa asiye mkurya aondoke Tarime. Hii maana yake anayepaswa kuwa wa kwanza kuondoka ni Massawe mwenyewe na Kamati yote ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Tarime ambayo M/Kiti wake ni DC (sio mkurya). Mbona mwaka huu maigizo mengi?

Masawe anajaribu kujisogeza karibu na ccm ili mkulu aendelee kumuacha tarime.

Ni vizuri ikumbukwe kwamba wananchi wa tarime hawajawahi kukubaliana na uamuzi wa serikali kuweka kanda maalum ya tarime/rorya tena bahati mbaya sana chini ya masawe ambaye hapo kabla alikuwa ocd tarime na chini ya uongozi wake matukio ya uhalifu na mauaji yalikuwa ni mengi sana kiasi kwamba matarajio ya wanatarime ni kwamba masawe alistahili kufukuzwa kazi kwa kushindwa majukumu yake.

Sasa jambo la ajabu sana ni kwamba masawe akateuliwa kuwa kamanda wa kanda maalum tarime/rorya na bahati mbaya sana hajajirekebisha, nadhani uwezo wake ni mdogo sana kiutendaji, sasa wananchi wa tarime hawajawahi kuwa na amani wala usalama wao na mali zao tangu kanda maalum ianze. Kinyume na matarajio uwepo wa kanda maalum umesababisha ongezeko la mauaji, uhalifu na uvunjifu wa haki za kiraia na za kibinadamu na kwa sehemu kuwa unafanywa na kutekelezwa na jeshi la poisi kanda maalum tarime/rorya chini ya masawe. Nadhani mnakumbuka tukio kubwa sana na la aibu la mwaka jana, wanawake kubakwa na kudhalilishwa na polisi wa kanda maalum tarime/rorya chini ya masawe huyu huyu na hakuna hatua zozote zilizochukuiwa.

Kiujumla uwepo wa kanda maalum tarime/rorya si kwa manufaa na maslahi ya wananchi wa tarime na rorya kama serikali ilivyotaka watu waamini, kilichopo ni katika "kuwashughulikia" wakurya na ndio maana polisi kuua watu huko tarime limekuwa ni jambo la kawaida. Kuna siku moja mkulu wa kaya akitetea kuanzishwa kwa kanda maalum ya tarime/rorya alisema ati Tarime wakati huo wa ukoloni ikiitwa north mara lilikuwa ni eneo gumu sana kulitawala kutokana na sababu za kihistoria, kwamba hata wakoloni wa kijerumani walikuwa wakipata shida sana kulitawala eneo hilo. Nadhani ccm na serikali yake imeamua kuwa mkoloni wa kijerumani ndani ya wilaya ya tarime.

Kama wananchi wa tarime wangesikilizwa ama kuulizwa kuwepo ama kuondolewa kwa kanda maalum ya tarime/rorya, ni wzi kwamba siku hiyo hiyo wangefungasha virag vyao wakaondika, wananchi hawaitaki hii kanda maalum, inawanyanyasa badala ya kuwalinda , inapora mali zao badala ya kuzilinda.
 
Anasema matatizo ya tarime yaachiwe wanatarime wenyewe, na watu wengi wanatoka nje ya tarime kuja kuchochea vurugu, na watahakikisha wale wote wasiyo wanawatarime watawahamisha

Hawa watoto wa chadema muda mwingine wanatia kinyaa............
Sasa hapa umeanzisha thread ya nini?
Alichosema mbunge ndio mtizamo wake, wewe ulikuwa unataka asemeje?

Kuweni na akili jamani, pamoja na kujazwa ujinga mwingi...tumieni akilini zenu pia kama zipo!

Ushauri wa bure: Ni vema mmalize shule kwanza, muje huku uraiani, pengine mtaona mambo kwa mtizamo tofauti!
 
Sasa kama wewe umemaliza shule lakini huwezi kuyaona mambo kwa uhalisia wake, kuna sababu gani ya kujivunia kumaliza shule na kuwashauri wenzio wamalize shule kwanza??

Kuunga mkono pumba za nyangwine ni sawa na kutokwenda shule kabisa. Nani asiyejua kwamba Tundu Lisu amekuwa mwanaharakati wa mazingira na rasilimali zetu za asili tangu miaka na miaka!? bila shaka wanamagamba hawakumbuki!

Nani asiyekumbuka kazi nzuri na za kutukuka zilizofanywa na LEAT chini ya uongozi wake Tundu Lisu?? Kuanzia Bulyanhulu hadi North mara? Bila shaka ni wanamagamba hawakumbuki!

Nani asiyekumbuka ni kwa kiasi gani Tundu Lisu amekuwa msaada kwa watanzania wengi wanaoonewa na serikali dhalimu ya ccm? marehemu chacha wangwe ni mmoja kati ya wengi walionufaika na usaidizi wa Tundu Lisu, tena bila malipo; chama cha magamba kilimbambikia kesi zaidi ya kumi ili kummaliza lakini kwa msaada wa Tundu Lisu alitoka gerezani na kuja kushinda ubunge tarime! bila shaka wanamagamba hawakumbuki!

Tundu Lisu anafahamika zaidi na wanatarime kuliko mbunge nyambari kwakuwa yeye muda wote alikuwa amejificha dsm, asingeweza kutia mguu tarime, alikuwa bado anatumikia laana ya mzazi wake. Lakini kwa sababu ya uroho wa madaraka ndipo akakumbuka kwamba tarime ni "nyumbani kwao". Hata hizo rasha rasha za mawe ni salamu tu kwamba wananchi hawamtambui kwa kuwa ameshindwa kuwajibika. Kama angekuwa anatambua wajibu wake kwa wapiga kura wake pamoja na wananchi wa jimbo la tarime angekuwa tarime sasahivi akiendelea kusaidiana na wapiga kura wake kutatua matatizo yao, lakini ajabu na kweli nyambari yuko dsm anauza sura kwenye vituo vya television na radio za burudani!!

Tundu Lisu anafahamika sana Tarime kuliko mbunge wa tarime nyangwine, amekuwa ni msaada kwao wakati wa shida na raha, na ndio sababu wananchi wa nyamongo walipopata matatizo mtu wa kwanza kumtafuta alikuwa ni Tundu Lisu. Wanatarime wanamuamini na yeye anawathamini ndio maana haoni shida kutoka singida na kwenda tarime kusaidiana na watanzania wenzake kunapokuwa na matatizo!!
 
Sasa kama wewe umemaliza shule lakini huwezi kuyaona mambo kwa uhalisia wake, kuna sababu gani ya kujivunia kumaliza shule na kuwashauri wenzio wamalize shule kwanza??
Kuunga mkono pumba za Nyangwine ni sawa na kutokwenda shule kabisa. Nani asiyejua kwamba Tundu Lisu amekuwa mwanaharakati wa mazingira na rasilimali zetu za asili tangu miaka na miaka!? bila shaka wanamagamba hawakumbuki.

Nani asiyekumbuka kazi nzuri na za kutukuka zilizofanywa na LEAT chini ya uongozi wake Tundu Lisu?? Kuanzia Bulyanhulu hadi North mara? Bila shaka ni wanamagamba hawakumbuki!

Nani asiyekumbuka ni kwa kiasi gani Tundu Lisu amekuwa msaada kwa watanzania wengi wanaoonewa na serikali dhalimu ya ccm? marehemu chacha wangwe ni mmoja kati ya wengi walionufaika na usaidizi wa Tundu Lisu, tena bila malipo; chama cha magamba kilimbambikia kesi zaidi ya kumi ili kummaliza lakini kwa msaada wa Tundu Lisu alitoka gerezani na kuja kushinda ubunge tarime! bila shaka wanamagamba hawakumbuki!

Tundu Lisu anafahamika zaidi na wanatarime kuliko mbunge nyambari kwakuwa yeye muda wote alikuwa amejificha dsm, asingeweza kutia mguu tarime, alikuwa bado anatumikia laana ya mzazi wake. Lakini kwa sababu ya uroho wa madaraka ndipo akakumbuka kwamba tarime ni "nyumbani kwao".

Hata hizo rasha rasha za mawe ni salamu tu kwamba wananchi hawamtambui kwa kuwa ameshindwa kuwajibika. Kama angekuwa anatambua wajibu wake kwa wapiga kura wake pamoja na wananchi wa jimbo la tarime angekuwa tarime sasahivi akiendelea kusaidiana na wapiga kura wake kutatua matatizo yao, lakini ajabu na kweli nyambari yuko dsm anauza sura kwenye vituo vya television na radio za burudani!!

Tundu Lisu anafahamika sana Tarime kuliko mbunge wa tarime nyangwine, amekuwa ni msaada kwao wakati wa shida na raha, na ndio sababu wananchi wa nyamongo walipopata matatizo mtu wa kwanza kumtafuta alikuwa ni Tundu Lisu. Wanatarime wanamuamini na yeye anawathamini ndio maana haoni shida kutoka singida na kwenda tarime kusaidiana na watanzania wenzake kunapokuwa na matatizo!!

Acha uongo wewe.........kumbe na wewe ni wale wale!
Chadema waliiona ile tragedy ya Nyamongo kama political oppurtunity na wali move in haraka ili kutaka Ku-score political points! Yaani wewe unawatania watu wa Tarime, msaada waliotaka wao ni kuzikwa kwa maandamano.

Lissu alikwenda pale kuongoza maandamano na kuchochea hisia za watu wa Tarime dhidi ya serikali.
 
Rais angaliwa wabunge wako na makada wa chama chako cha CCM hii dhambi ya kubaguana mbaya itakuja kuleta madhara makubwa sana katika taifa hili na kwa ushauri wangu tu. DHAMBI HII ITAKUWA MIKONONI MWAKO HAKIKA

Hivi kule kunatakikwa kukaa wakurya tu sio watanzania sasa na yule kamanda MASAWE aondoke kule maana na yeye ni mgeni jamani jamani tanzania tanzania tunaenda wapi jamani?
 
Wanatarime kwa hali waliyofikia wanahitaji msaada kutoka kwa wasomi, vijana ambao ni CDM, CCM hawawezi kuwasaidia kwani wana 10% zao kwenye hiyo migodi. Kama si kweli kwa nini hawachukui hatua? watu wanauawa, wamwagiwa maji ya sumu kwenye mito na kubaki masikini.

Tanzania iachiwe watanzania na si wahindi, wachina, Wasomali na wazungu ete
 
Acha uongo wewe.........kumbe na wewe ni wale wale!
Chadema waliiona ile tragedy ya Nyamongo kama political oppurtunity na wali move in haraka ili kutaka Ku-score political points! Yaani wewe unawatania watu wa Tarime, msaada waliotaka wao ni kuzikwa kwa maandamano.

Lissu alikwenda pale kuongoza maandamano na kuchochea hisia za watu wa Tarime dhidi ya serikali.

Acha ushamba wewe, watu wa tarime hawahitaji kuchochewa, wanaelewa wanachokitaka.

Hata mwanamagamba mwenzako Shamsi Vuai Nahodha anajua wanachotaka watu wa tarime lakini nyie vigamba uchwara ndio mnajifanya kufumbia macho ukweli wa mambo.

Lema ni mbunge wa arusha lakini alikwenda tarime, Wenje ni mbunge wa nyamagana lakini alikuwepo na Marando alikuwepo pia. Lakini kwa kuwa mmefilisika kisiasa na kiuongozi mkaamua kuleta mbele hoja yenu ya ukabila kwa kumshikia bango Tundu Lisu na kuwaacha wengine.

Watu wa nyamongo hawawezi kuhitaji msaada wa kuwazika ndugu zao ambao serikali ya magamba imewaua, na msivyo na aibu serikali yenu ikaamua kupora miili ya marehemu na kuwalazimisha ndugu zao kuizika, na mbaya zaidi jinsi msivyo na ubinadamu mkaamua kuitupa miili hiyo barabarani na vichakani. Hii dhambi kwa hakika itawatafuna miaka yote, na nyangwine hawezi kwenda nyamongo kuongea na wananchi, na ikitokea akaenda huko itabidi azungukwe na polisi wauaji na ataishia kuwahutubia polisi hao hao!!
 
akikaa tarime atashindwa kuchakachua vitabu vyake vya low quality
 
sasa yeye ndio mbunge wa kule na anajua kinachoendelea. wewe pengine hata hujawahi kukanyga huko tarime unambishia na kuita alichoongea pumba, unadhani kati yake na wewe nani mwendawazimu >?? wewe hapo

hili jamaa ni pumba tupu yaani akili imechanganyika na maji... ndo maana mi nilikuwa nalipigisha magoti assembly kule Mkwawa secondary...
 
Back
Top Bottom