Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Mkuu, huyu binadamu mwenye magamba alimtenda nini baba yake?
Mkuu ni mambo ya ajabu sana, mengine hayaandikiki wala hayatamkiki kwa mtu mwenye kumheshimu binadamu mwenzake na hususani mwenye umri sawa na mazazi wake. Sasa huyu mwanamagamba pamoja na mambo mengine ambayo siwezi kuyasema, alimtukana vibaya sana baba yake mzazi na kama haitoshi akamtungia kitabu na kuendelea kumtukana.
Si unajua jamaa amejaliwa uwezo wa kuandika andika. Basi baada ya hapo ndipo mzazi wake alimlaani, na miaka yote amekuwa akiishi DSM, hakuwahi kukanyaga kwa mzazi wake Tarime. Hata alipotaka kugombea ubunge alilazimika kumuomba radhi mzazi wake lakini ngoma ilikuwa ngumu.
Angeanzia wapi kuongea na baba yake? Ilibidi awatume baadhi ya wazee wa Kikurya wenye ushawishi mkubwa kutoka DSM wakawatafuta na wenzao walioko Tarime ndio walifanya kazi ya kumuombea msamaha, ilibidi mzazi akubali kumsamehe kwa shingo upande kutokana na shinikizo kubwa.
Bahati mbaya hicho kitabu sikikumbuki title yake lakini hapa jukwaani kuna watu walishakisoma na wanaifahamu sana hiyo habari wanaweza kutukumbusha ni kitabu gani.
Haya maandiko yapo na watu wengi waliobahatika kukisoma wanashangaa kwamba huyu mkulu aliweza wezaje kuchaguliwa kuwa mbunge? Sasa kabla hata ya miezi sita ameonyesha udhaifu mkubwa na kutokubalika kwa wapiga kura wake.