Mbunge wa Rorya Lameck Airo (Obama) kujiuzulu ubunge?

quote_icon.png
Originally Posted by OgwaluMapesa
Mhe Mbunge wa rorya Lameck Airo ametishia kujiuzulu ubunge baada ya mgogoro kuibuka juzi baada ya kamati ya siasa kukata jina la rafiki yake charles Ochele obuto kugombea uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rorya

Mbunge wa Rorya Lameck Airo amesema endapo maamuzi ya kamati ya siasa ya mkoa hayatatenguliwa yuko tayari kurudisha kadi yake na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida

"'kama pesa ninazo sikuhingia kwenye siasa kuganga njaa bwana mdogo ,ninao uwezo wa kuwaajiri wajumbe wote wa kamati ya siasa ya mkoa, haiwezekani wakate jina la ochele anakubalika kuliko hata mimi ,mchango wake kifedha ni mkubwa mno ndani ya chama na alikisaidia chama kifedha kipind cha uchaghuzi mkuu hiki chama hakina shukrani "' mwisho wa Kumnukuu

Huyuaendelee na ubunge akajazilie namba ya vihiyo wa ccm kwa sababu hakuingia kwa uwezo bali visenti.
 
Tulishasema humu elimu ni muhimu sana watu ohoooo sijui kuna informal edu, haya muone sasa. Mimi si mtabiri lakini huyu Mbuge atafanya vituko sana ndani ya mwaka mmoja tu maana anafikiri suala ni kujigamba juu ya fedha mkononi bila hata kutuonyesha balance sheet yake.

Kwa nini asielezewe kuwa kuna hatua na namna ya kuzifuata anapokuwa na malalamiko? Mbona atarudisha kadi za kila chama atakachojiunga kwa mwendo huo hadi kadi ya mwenyezi Mungu. Maana hapa duniani kuna dhuluma nyingi tu, angekuwa na upeo mkubwa wa kuona mambo basi asinge tamka kurudisha kadi bali kusema atafuatilia katika ngazi husika kuona kuwa haki inatendeka kama haikutendeka.

Wewe mtu wakati wa Kampeni anasema waziwazi, "Obilo! kama si hii sheria sasa hivi ngombe......wangekuwa wameanguka hapa......".

Sasa atasemaje Bungeni maana watu huko hawasubiri iwepo misiba ili aangushe ngombe, huko watu wanaangusha issues!

Asinambie mtu karne ya 21, Mwakilishi wa jimbo anayekwenda kujadili miswada na kutunga sheria na kudhibiti Serikali anajivunia elimu ya msingi na kuwabeza waliosoma? Kuwa na maendeleo kibiashara (kama yapo) si lazima kuwa ni kuwa na sifa za kuwa Mbuge!!!
 
Huyu jamaa abadili jina asijiite Obama tena. Kama aliyeleta habari hajachakachua naona hapa hakuna mbunge.
1. Mbunge asiyejua amechaguliwa kuwawakilisha wananchi na siyo kamati ya siasa. Akitofautiana na kamati ya siasa ya chama anatosa wananchi?
2. Rafiki yake ni bora kuliko wananchi wote wa Rorya waliompa kura za kutosha
3. Unaweza kurudisha kadi na ukawa mwanachama wa kawaida?
4. Tangu wakati wa kampeni yeye ni kujigamba fedha tu hadi chama kinaonekana ombaomba kwake. Wamempa nafasi kwa sababu ya pesa.
5. Kuwa na uwezo wa kuajili wajumbe wa kamati ya siasa inamaanisha hawana maamuzi kuliko wewe mwenye pesa?
6. Kumbe rafiki yake anamgombania sababu ana pesa na anakubalika kwa sababu ya pesa zake na siyo uwezo wa uongozi?
7. Hivi nafasi hiyo ingekuwa inahitaji usaili angeweza kutambua uwezo wa huyo jamaa wakati mwenyewe upstairs nil
 
Mhe Mbunge wa rorya Lameck Airo ametishia kujiuzulu ubunge baada ya mgogoro kuibuka juzi baada ya kamati ya siasa kukata jina la rafiki yake charles Ochele obuto kugombea uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rorya

Mbunge wa Rorya Lameck Airo amesema endapo maamuzi ya kamati ya siasa ya mkoa hayatatenguliwa yuko tayari kurudisha kadi yake na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida

"'kama pesa ninazo sikuhingia kwenye siasa kuganga njaa bwana mdogo ,ninao uwezo wa kuwaajiri wajumbe wote wa kamati ya siasa ya mkoa, haiwezekani wakate jina la ochele anakubalika kuliko hata mimi ,mchango wake kifedha ni mkubwa mno ndani ya chama na alikisaidia chama kifedha kipind cha uchaghuzi mkuu hiki chama hakina shukrani "' mwisho wa Kumnukuu

Elimu yake darasa la saba invyosemekana!!
 
Hivi kama siyo ukosefu wa elimu ni nini? Itawezekanaje urudishe kadi halafu uwe mwanachama wa kawaida? Halafu kwa nini viongozi wa CCM wafuate maamuzi ya LAMECK AIRO? Rorya hatuna mbunge.
 
Back
Top Bottom