Wana JF mambo kama haya ni vizuri kuweka source hadharani.Mimi naona huu ni uvumi tu maana hiyo kesi itakuwa imeendeshwa kwa siku ngapi,maana hili jambo ni juzi tu na issue yenyewe ni kutishia kuua! Spidi hii ya mahakama imetoka wapi?
Kesi iliyokuwa inamkabili Mbunge CCM Mbarali ambaye alikuwa katika kambi ya wapinga mafisadi alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua amefungwa miezi 10 na hivyo kuachia kiti kama sheria za uchaguzi zinavyosema.
Pole Nape, Sita, Mwakyambe na Mama kilago malecela shughuli inakuja kwenu mpiganaji wa tatu ametoweka tukianza na Seleli, Mpendazoe na sasa Kilufi wa Mbarali
Angekuwa ni mbunge wa chama flani ndio amehukumiwa kifungo hicho, ungewasikia viongozi wa chama hicho wakisema, TUNAITISHA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA kupinga uonevu wa serikali. Tutaandamana mpaka Mahakama itoe amri ya kumuachia huru!!!
Lakini CCM wako kimya, wameiacha mahakama itekele majukumu yake ya kikatiba bila upendeleo wala woga.
Nadhani "Nguvu ya Umma" tunakitu cha kujifunza hapa.
Faini haikuwepo
ni mbunge kilufi wa mbarali amefungwa kwa maagizo ya serikali
Mi nilidhani Mahakama ni muhimili unao jitegemea kwa kutoa maamuzi kulingana na sheria zilizopo? Kumbe mahakama inaweza mfunga mtu kwa maagizo ya serikali? mmmhhh.. kazi ipo!
Hizi sheria zetu hazieleweki, hata Steven Wassira Tyson alishawahi kupatikana na kosa mahakamani la kutoa
rushwa katika uchaguzi (Refer kesi ya Warioba V Wassira: Bunda constituent). Adhabu aliyopewa ni
kutogombea cheo chochote kwa uongozi kwa kipindi cha miaka 5, na baada ya hapo akawa huru na sasa
hivi ni Mbunge na Waziri.
Pamoja na madhaifu hayo ya sheria yetu, inakuwa je JK anateuwa a convicted corrupt guy kwenye cabinet
yake? Ni ujumbe gani anatuma kwa Watanzania? Kwamba birds of the same feather flocks together, TAFAKARI!
Kama ni kweli, CCM wana mkakati mkali. Hiyo ni kazi ya Fisadi Mkubwa RA ambaye bado anaheshimiwa na Serikali yetu Fisadi. Ni mpango wa kuwanyamazisha wapinga ufisadi lakini ni njia ya kudhoofisha CHADEMA kwa maana wataanza kuwaweka ndani akina Lema, SLaa na wengine kufuatia kesi zinazowakabili. Ni mtego ambao CDM wanatakiwa kujipanga ili kuutegua.
Kesi iliyokuwa inamkabili Mbunge CCM Mbarali ambaye alikuwa katika kambi ya wapinga mafisadi alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua amefungwa miezi 10 na hivyo kuachia kiti kama sheria za uchaguzi zinavyosema.
Pole Nape, Sita, Mwakyambe na Mama kilago malecela shughuli inakuja kwenu mpiganaji wa tatu ametoweka tukianza na Seleli, Mpendazoe na sasa Kilufi wa Mbarali
Amehukumiwa miezi kumi jela au FAINI YA SHILINGI LAKI SITA. Jamaa ameshalipa hiyo faini..