Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina (CCM) kutopiga kura ya kupitisha bajeti 2012/2013 umeishia wapi?

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina (CCM), amejitokeza na kueleza msimamo wake wa kutopiga kura ya kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Mpina alisema kuwa aliendelea kuwa na msimamo wake kutokana na serikali kushindwa kujibu hoja zake za kuongeza fedha katika mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano.



Mbunge huyo alisema hoja yake kubwa ni kutaka fedha za maendeleo ziongezwe toka sh trilioni 2.2 kufikia trilioni 2.7 kwa fedha za ndani ili kukidhi mahitaji ya fedha zinazohitajika kutekeleza miradi mbalimbali iliyoainishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

 

Attachments

  • mpinga.jpg
    mpinga.jpg
    6 KB · Views: 69
Back
Top Bottom