Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akutana na waandishi wa habari

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


[h=3]Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akutana na waandishi wa habari nakuzungumzia kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.[/h]


msigwa1.jpg

msigwa2.jpg


Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akiongea na waandishi wa habari mkoani iringa jana.

---
Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa amesikitishwa kuona viongozi wakuu wa serikali kukaa kimya kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.



Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Msigwa amesema amesikitishwa sana na kifo cha Mwandishi mwangosi kwani hata kilipotokea yeye alikuwa safarini kuelekea Ujerumani lakini kwa kuufahamu mchango mkubwa aliokuwa nao Mwangosi katika kutetea haki kwa wananchi wa Iringa na tasnia ya habari ilimbidi ahairishe ili kuweza kutoa pole kwa familia ya marehemu.


Ameeeleza kuwa yeye kama mbunge amesikitishwa sana na kuona viongozi wakuu wanchi kama rais kutozungumzia suala hili na haswa kwa viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya ambao marehemu alikuwa akifanya nao kazi kwa karibu sana.



“Nimesikitishwa sana kuona kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kuzidi kuwepo ofisini kwa lile lilitotokea, mikono ya kamuhanda na mikono ya Said Mwema imejaa damu, na mimi naungana na wanahabari kuugomea uongozi wa RPC Iringa” alisema.



Ameongeza kuwa anasikitiswa sana Meya wa manispaa wa Iringa Amani Mamwindi kuhusika katika utoaji wa amri ya kuvunjwa kwa vijiwe vya wananchama wa CHADEMA.“Meya ametoa amri ya kubomoa vijiwe vya chadema akieeza kuwa ni amri ya jiji na kuacha jukumu lake kubwa la kuhakikisha kuwa takataka za mji zinatolewa na kuhakikisha uchumi unaendelea na badala yake kuhusika kubomoa vijiwe vya wanachama pamoja na kutoa bendera na hatutaruhusu hali hii iendelee” aliongeza msigwa.



Kuhusu yeye kutoonekana kuwajibika jimboni na kuwa na ziara nyingi za nje Msigwa amesema haendi huko tuu kwa maslahi yake binafsi ila anafanya ili kujifunza mambo mengi ambayo yatakuja kuwasaidia wananchi baadae nahii inatokana na yeye kuwepo katika uongozi wa katika wizara mbalimbali ambapo ziara hizo zina maslahi kwa jamii nzima.



Kutokana na hali hiyo mbunge huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano utakaofanyika katika eneo la soko kuu kuanzia saa nane kamili na kuongea na wananchi kuhusiana na mambo mengi yanayohusiana na maendeleo ya jimbo.
5996140674267894691-9104396332022446577

 
mheshmiwa Msigwa, keep up a Good job, swala la RPC liko wazi kisheria inabidi achukuliwe kwa kwenda kinyume na taaluma ambayo ni kulinda maisha ya watu na siyo kuuwa watu. kuhusu viongozi wa mkoa hao ni makuhaidi wa CCM maadam wakubwa zao wamekaa kimya tegemea nao kukaa kimya nakukumbusha hotuba kabambe ya april 2012 kuwa usitegemee vingozi hao hao walioaribu nchi kuwa na akili au mawazo ya ghafla ya kujenga nchi hii haiwezekani.

" insanity is doing the same thing and expecting different result" mhe.Frank Msigwa Bungeni april 2012
 
Siamini kama tupo Tanzania, nchi ambayo inasemekana inafuata misingi ya kidemokrasia, haki na utu wa kila moja!
Siamini kabisa!
 
Hivi samahani mkuu kwani wewe unaishi nchi gani? maana mabandiko yako mengi huwa unaposti habari za jana au magazeti ya jana!! labda nchi uliyopo tunatofautiana sana masaa?
 
Siamini kama tupo Tanzania, nchi ambayo inasemekana inafuata misingi ya kidemokrasia, haki na utu wa kila moja!
Siamini kabisa!

Aisee Mungi!
unataka kula keki halafu bado ubakie nayo? Tafakari, chukua hatua!!!
 
Back
Top Bottom