Mbunge wa Hai Mh. Mbowe afanya mambo...

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
attachment.php


Mbunge wa Jimbo la Hai mh. Freeman Mbowe amewatembelea wakazi wa Mtaa wa Lerai wilayani Hai na kuwakuta wakiwa kwenye kikao cha kupanga mkakati wa kujenga Darasa katika shule ya sekondary lerai, Mbunge alipofika wananchi Hao walifarijika nakufurahi kumuona mbunge wao akiendelea kuwatembelea ambapo mbunge kama ilivyo kawaida kwake aliwapongeza wananchi kwa jitihada zao na kuwaambia wanachi wao yeye akiwa kama mwana Hai atachangia ujenzi wa darasa hilo na hatimae kuukamilisha.

Mbunge amewapa wakazi hao mchanga kwa ajili ya ujenzi wa shule , Matofali 1100 na tractor pamoja na mafuta kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo. mbunge ametoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni tatu amewasaidia wananchi hao na wameshukuru sana kwani wananchi wanasema mh. Mbunge amewapunguzia mzigo mkubwa sana ambao ulikuwa unawakabili wananchi.

Wananchi wamefurahi na kumpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kuwakumbuka na kuwatembelea mara kwa mara. Huu ni utaratibu wa mh. Mbunge huyu kuwasaidia watu wake ambapo mpaka sasa ameshasaidia shughuli za maendeleo zenye thamani zaidi ya Tsh. Milioni mia tau tangu kuchaguliwa kwake.
 

Attachments

  • mbowe-hai.JPG
    mbowe-hai.JPG
    64.8 KB · Views: 444
ili mradi zisiwe pesa za chama tafadhali, na pia ningependa chadema wawe wanaanda na kutoa finincial audited accounts za pesa zinazochangwa na wananchi inasaidia kuweka uwazi na uwajibikaji( good governance and accountability)
 
Hongera mbunge nawasihi wabunge waende majimboni wakawajibike huko kwa kuwaunga mkono wananchi.
Waibue miradi ya kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine bora
Ningependa kusikia wako majimboni wanashishirikiana na wananchi kutatua kero zao hata kuwamasisha wanachama wa mitaa kufanya serikali wameshindwa kuonyesha njia
Chadema kumbukenz enz za mwalimu viongoz walikuwa wanafanya kaz kwenye mitaa, tarafa, kata na majimbo kwa kushirikiana na wahusika kuweni mstari wa mbele kwa shughuli za maendeleo mtajenga imani mkipewa nchi mtaiendeleza anzeni na mitaa, tarafa, kata na majimbo msiwe watu wa maneno vitendo zero hasa wabunge kura ziko majimboni si kwenye vyombo vya habari mwisho wa siku wananchi watakupima kama umekuwa mstari wa mbele jimboni kutatua kero zao.
Zinazowashinda ndo za kwenda nazo kwenye vikao vya halimashauri na hata kuzisemea bungeni.
 
Hongera Mbunge Mbowe kwa kuthamini kazi ya wananchi. Usiishie kutoa huo msaada tu lakini kama kiongozi hakikisha hiyo shule inakamilika kwa kuisimamia ipasavyo
 
ili mradi zisiwe pesa za chama tafadhali, na pia ningependa chadema wawe wanaanda na kutoa finincial audited accounts za pesa zinazochangwa na wananchi inasaidia kuweka uwazi na uwajibikaji( good governance and accountability)
umeanza mambo ya mnazi shekh tena unadhani chama hakina utaratibu kwani chama ni duka la rejareja?
 
Pesa zetu tulizochangia ndio imekuwa pesa za miradi ya maendeleo! Ipo siku tutaitaji mapato na matumizi ya pesa zetu
 
umeanza mambo ya mnazi shekh tena unadhani chama hakina utaratibu kwani chama ni duka la rejareja?
sheikh wangu kukumbusha uwajibikaji ni Mnazi? ni vema wachangiaji wakawa wanapewa taarifa ya hesabu zilizokaguliwa ndio misingi ya uwajibikaji dunia nzima, tazama obama na romney baada ya uchaguzi taarifa ya fedha za michango inakuwa wazi hivyo nahimiza cdm pia wafuate misingi hiyo itawasaidia pindi wakishika dola.
 
Hongera mbowe wapi Halima Mdee au uko saloon mnyika utajibeba 2015.Msigwa kudadadeki mwakalebela anachukua jimbo lake
 
Hongera yenu wenye wabunge wanaowakumbuka,mbunge wetu alituambia kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni"mnichague au msinichague,mimi nitashinda"HATUKUMCHAGUA NA ALISHINDA"Hajawai kuja na wala ctegemei!
 
ili mradi zisiwe pesa za chama tafadhali, na pia ningependa chadema wawe wanaanda na kutoa finincial audited accounts za pesa zinazochangwa na wananchi inasaidia kuweka uwazi na uwajibikaji( good governance and accountability)

kaka Mbowe ni Mbowe si akina mrema au garasha wengine wa CCM.Mbowe aligombea Jimbo hakushinda kwa mara ya kwanza ila akatimiza ahadi zake.Mbowe aliwahidi watu jimboni kwake wakichanga kwa kiasi chochote watakapofikia atachanga mara mbili kutoka mfukoni kwake.Sidhani kama mnamjua vizuri sana ndugu.Hizo njaa zenu na mazoea yenu huko ktk jamii zenu ya kunyang`anyana migao si kwa familia ya akina mbowe bro.

Mbowe hakuwahi gombea chakula wala hela na katk familia yao ndivyo.Babake angeweza hata mtenga kama angesikia mwanae anagombea hela na vitu vidogo.Kwa ujumla mbowe ana ujasiri wa kugombea hela kwa ajili ya watu wengine na kwake jombaa.

Hizi fikra za kimasikini ndizo zinauza nchi,mkienda nje vitu vidogo hupoteza fahamu zenu.
 
nchi itajengwa na wenye moyo wa uzalendo,sio majizi ama mafisadi.mbowe anastahili pongezi kwakweli na afundishe pia baadhi ya wabunge wa cdm wapge bidii ili kutia chachu.twafaham kuwa wao ktk majimbo yao hawatizamwi kwa ukaribu lengo ni kuwafanya wananchi wapunguze imani jambo ambalo m4c ikiongozwa na jabali la siasa mh.dr.slaa ameweza kuwajenga kisaikolojia wananchi.kwa kweli kazi nzuri.go-ahead mh.mwenyekiti.
 
Kama Chadema wasingekuwa wanatumia maandamano idadi uliyoiona ndo mahudhurio wangekuwa wanayapata hasa kwa kiongozi mkuu wa Chama (Mwenyekiti). Hapo alikuwa anapima upepo kama anaweza kukubalika bila maandamano, kakuta yupo mdogo wake, mjomba, rafiki wa kaka yake na majirani watatu. Jumla ya mahudhurio watu 10, kikao au kijiwe? bora mtoa maada angesema Mbowe akuta vijana kijiweni na kuwaunga mkono baada ya kukuta wanaongelea maswala ya maendeleo akaamua kuwaunga mkono. Kiongozi uwe unataarifu, ona sasa ulivyo kishusha Chama chetu, kwa idadi hiyo hata angetembelea yule diwani wetu aliyeungana na ccm si angepata wengi! sijui kama ameweka sera hadhalani kwa idadi hiyo na chama chetu tulivyo na dharau. mh......................................
 
Kwa kasi hii sijui ccm italichukuaje jimbo hili.! Biashara asubuhi, kamanda wa bilcanas anakimbiza mbaya kuelekea 2015
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom