Mbunge wa CUF Magdalena Sakaya na viongozi waandamizi wa CUF wanyimwa dhamana mara ya pili

Poleni cuf..
Lkn mnkumbuka unafiki wenu bungeni mlivyokua mnawapigia kura wagombea wa ccm mkadhani ndugu zenu? Adhabu ni hapahapa duniani!
 
Kuna watu wanabeza dhana ya nguvu ya umma, hili la mbunge huyu na wenzake ni funzo kwao. Msingi wa dhana ya dhamana ni kuaminika/kuaminiwa kwa mtuhumiwa mbele ya mahakama na jamii. Je, mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu anaweza kutoroka kama watuhumiwa wengine?Ukweli ni kwamba ni ngumu kwa mwanasiasa kutoroka kwa kesi kama ya Tabora, sasa kinacholeta maswali ni kwanini wamepewa masharti magumu kiasi hicho?

Sisi wengine tulishashtuka toka siku ya kwanza walipopelekwa mahakamani, waliwekwa ndani, halafu ikapangwa tarehe ya 'mbali', na leo wamerudishwa ndani na kesi haiendelei kesho bali mpaka tar 15-huku ni kukomoana na hapo ndipo unapohitaji nguvu ya umma! Dhamana ni haki ya mtuhumiwa na haipaswi kucheleweshwa.

Bahati mbaya kwao wanaCUF ni kwamba walishaamua kukaa mbali na umma, lakini karibu na CCM. Inasikitisha, lakini ukweli ndo huo-imekula kwao. Nguvu ya Umma daima-hata wanasiasa wakitusaliti, tunahamia NGOs na nguvu ya umma mpaka haki sawa kwa wote ipatikane.
 
jamani, this is too much!!!................ kwa kweli wana-chadema mlioko huko tabora na hata wanasheria walioko makao makuu mjitahidi kuingilia kati hapo kuleta haki................ kumbukeni haki pia inatakiwa hata kwa mshindani wako kisiasa ili hata uuma ujue kuwa kuna tofauti kati yenu na ccm.............. mbunge wa ccm anaweza hata kumkata mtama mkuu wa polisi ofisini kwake na akaachwa arudi nyumbani kwake (nakumbuka kitu kinachofanana na hicho kiliwahi kuripotiwa wakati wa kampeni za uchaguzi) lakini wa chama kingine, kakosa kadogo tu anachukuliwa kama gaidi aliyeshindikana (angalia ya mbowe jana na haya ya sakaya)!!!.................

mi si mwanasheria lakini naona kwa kweli hapo pana kitu kiko nyuma ya huyo hakimu................panahtaji ushirikiano wa wapinzani wote................... sioni ishu hapo ya kunyima watu dhamana, nani anayeweza kuamini kuwa sakaya anaweza kukimbia nchi au hata kujificha tu kwa kesi kama hiyo??................ mtu wa nafasi yake kwa kesi kama hii si angeweza kuruhusiwa hata kujidhamini mwenyewe?.......................
 
Bila kujali tofauti zetu naomba Chadema isaidie suala hili kwa mtindo wa People's Power. CUF wanaweza wasiwe wanaamini juu ya hii falsafa ya PP lakini ina manufaa kwa kuweka mashinikizo kwa serikali au watawala (dola, mahakama, bunge).
Naomba sana kama Lipumba alivyofanya kwa Mbowe basi na viongozi wa Chadema walipe fadhira kidogo kwa kuongeza Peoples Power ili maandamano yaitikise Tabora na kuifanya wilaya husika isitawalike kwa muda. Watawala waliochoka kufikiri wakikosa usingizi kwa dakika kadhaa tu basi wataamru mahakama imwache huru ili wapumue.

Umoja ni nguvu!!
 
Mtatiro vipi unafanya nini Dar es Salaam. Yaani Mh Mbunge akae Mahabusu mwezi mzima jamani! Very sikitishabo kwa kweli. Something must be done
 
Huyo hakimu inafaa achunguzwe na au mtoa habari kama ni habari za kweli au walishindwa masharti mengine ya dhamana. Si vyema kuihusisha mahakama na CCM. Kama hakimu ana mapungufu basi huyo hakimu hatoungwa mkono na CCM. Na kama mwandishi wa hii habari ndio ana mapungufu nae pia achunguzwe.

hivi huyu mwana mama ana undugu na MS au ni mk....
 
CCM wanazidi kufulia kisiasa hata "Rahisi JK" ndo kabisaa ona juzi kaanza vita na viongozi wa dini eti wanauza madawa ya kulevya kama sio kuchanganyikiwa ni nini??? Hawa jamaa sijui wanataka nini???
 
Hawa wana CUF wanabeza nguvu ya umma (maandamano) na wanapingana na chadema kwa mambo mengi. lakini wajue kuwa hakuna nguvu zaidi ya peoples power. Kama huyo mbunge angekuwa wa chadema ni wazi kuwa nguvu ya umma ingeshamto mara moja. lakini kwa sababu ni cuf wanaoamini katika matumizi ya majadiliano badala ya nguvu basi wanaendelea kusota wakati majadiliano yanaendelea. Chama cha maganba hakina lugha ya kusiikiliza zaidi ya matumizi ya nguvu.

Shame 2 u CUF. Mnaboa sana kwa KUSHINDWA kuwatoa hao viongozi wenu wa ngazi za juu. Mbowe amepelekwa arusha kwa ndege ya jeshi (ya kukodi jana) na akaachiwa siku hiyo hiyo pamoja na gharama zote iliyoingia serikali kumsafirisha. Hiyo ndio peoples power BWAna. PEOPLES POWER
 
Huyo hakimu inafaa achunguzwe na au mtoa habari kama ni habari za kweli au walishindwa masharti mengine ya dhamana. Si vyema kuihusisha mahakama na CCM. Kama hakimu ana mapungufu basi huyo hakimu hatoungwa mkono na CCM. Na kama mwandishi wa hii habari ndio ana mapungufu nae pia achunguzwe.

naomba picha yako bila ushungi na ukiwa umevaa kimini. nitumie privately.
 
chadema na wanasheria wake na vyama vya sheria tafadhali ingilieni ili suala la awa wawakilishi wetu mapema!!wanatuwakilisha wanainchi na tunataka dhamana...

shida ya tabora wote chama cha magamba...nilioenda kule nikashangaa jinsi mkoa ulivochini na bado wanawapigia kura hao wanaoteteana kijinga-jinga,so PP haitawezekana labda tu-hire toka mwanza waje uko
 
Mwanazuoni wa kiislamu sheikh Mataka leo ametutaka tusiingilie mambo ya mahakama, tuache sheria ifuate mkondo wake, kwa sababu ni msomi sana huyu sheikh basi tumsikilize.

Mie simjuwi huyo na sijamsikia labda ana point lakini ukumbuke post yangu imesema achunguzwe hakimu na mtowa habari, kuna mmoja kati yao hayuko sawa.
 
Poleni cuf..
Lkn mnkumbuka unafiki wenu bungeni mlivyokua mnawapigia kura wagombea wa ccm mkadhani ndugu zenu? Adhabu ni hapahapa duniani!


Hata mimi nampa pole sana Sakaya na wenzake ingawa CUF wanapaswa wajue kuwa CCM
haina rafiki wa kudumu bali kina maslahi ya kudumu. Waache unafiki na waungane na wapinzani
wenzao ili wachape kazi
 
Kumbe ndoa ya CUF na CCM ipo zenji tu? aisee..... aisee.......aiseeeee.............
 
Wakili anayesimamia hiyo kesi afuatilie hizo documents zinatakiwa kwa mtendaji wa kata halafu hakimu aandike remove order kwenda gerezani kabla muda wa mahakama haujaisha ili wapatiwe dhamana.
Wakigoma kutoa dhamani baada ya hizo docs kupatikana basi tuandamane kwenda kwa jaji mkuu wa Tz maana mahakama zetu zimekuwa corrupt kupita kiasi, huu ni ukandamizaji uliopitiliza.
 
Hivi ni kipi kilichomfanya Prof. Lipumba kwenda Central Police kutaka kumuwekea
dhamana Mbowe (wakati akijua kabisa kuwa mazingira hayaruhusu) na kuwaacha
viongozi wa chama chake cha CUF (akiwemo Sakaya) wanaosota huko Tabora?
Is this a joke? Au ni unafiki?
 
Pole sana mh sakaya hawa ndio majuha mda wao upo ukingoni nguvu zao zimebaki kwa police na mahakama wanaotumiwa vibaya utadhani mwanamke anayetumia vibaya viungo vyake vya mwili.
 
Back
Top Bottom