Mbunge wa CHADEMA (Msigwa) atalipoteza jimbo kwa mwendo huu

mkuu kitanzini wamejaa waswahili na wengi wao shule hakuna kidoogo maeneo ya miyomboni sokoni na stendi wanajitambua kifikra na ndo kula nyingi za CDM zilitoka hapo,ila maeneo ya Kitanzini walinunuliwa na el 2000 kila siku nyumba hadi nyumba
Usitukane watu wa Kitanzini wewe, huwajui kwa kuanika wala kuanua!!

Kwani umeambiwa kwamba Kitanzini hatukupata Kura?
 
wakuu tumwache msigwa yuko sawa''ndugu yetu sugu atarudi bungeni????mbeya sio mchezo
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.

Nchi hii itajengwa na wenye moyo tu,na wala si wapenda hongo za sukari,tshit nk yaani kwa kifupi wapenda dezo (PATA RAHA SIKU 10 TESEKA MIAKA MI5).
 
...hapana, elewemi CCM ni "WEZI" wakati nyie mnahangaika kusema wameshinda kumbe wenzenu walishaiba, mie siamini CCM kama wameshindwa kiukweli, naomba MSIGWA aje hapa atudokeze au kama kuna mtu wa Iringa.
 
wakuu tumwache msigwa yuko sawa''ndugu yetu sugu atarudi bungeni????mbeya sio mchezo

Kuna kanuni moja tu ya kura za kisiasa. Kama wote mnaanza Kampeni mkiwa na Kura 100 kwa kila mmoja, basi ushindi hauji kwa kura ulizo nazo wewe bali ni kwa kuchukua kura za mwenzako. kama eneo "A" mpinzani wako ana kura 20 na wewe eneo "D" una kura 50 basi mwenzio akichukua zako 30 za eneo "D" na wewe ukachukua zake 10 za eneo "A" utapata kura 30 na yeye 40. Hajakushinda kwa sababu watu wake hawajakuchagua bali amekushinda kwa sababu amechukua kura za watu wako!! Huo ndiyo UKWELI!!

Hii ndiyo hesabu inayoweza ama kumrudisha Sugu bungeni au kumbwaga.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.

Wakuu hapo kwenye red zingatieni haya:Hii kata inaitwa Kitanzini-miomboni hiyo moja.Pili Matokeo hapa yalikuwa hiv.Magamba(Jesca-647) na CHADEMA(Kalolo 582) tofauti ni 65.Tatu-Miomboni ni Stendi kuu,Soko Kuu in short Town Center ambako kote Kalolo aliongoza,japo fire walipishana 4,lakini asilimia kubwa CDM waliongoza kwa kishindo.KUMB:Hapa ni town center,Who knows what Tanzanians Want now.Na HUKO KITANZINI(Jina lenyewe kama linavyojisema) Wengi wakazi wake(Kwanza nidiklee interest,Nachukia sana Udini alioasisi Baba Riz & The company) nachosema,wengi ni wale wanaofuata TAMKO LA IGUNGA,Huo ndio ukweli na nitausimamia daima.Inawezekana walipiga kura kwa misingi hiyo.Magamba ndiko walikopatia ushindi.Kuna kituo komoja hivi;Magamba 74 CDM 19!!!!! What a hell!!!!!!!Lakini hiii isiwe eti ndio hoja ya huyu ndugu kusema eti Msigwa anaharibu,Naishi hapa,napafahamu,HUYU Mch.Kaikamata IR hata akilala bado haiondoki kudondokea kwa magamba hii Jimbo chalii angu,ni kwere Msigwa ati.Alitetea Stendi ya Miomboni asijinyakulie mtoto wa Mzee wa pale Feri mas-hala nini.Msigwa hang'oki labda 15 yrs later.La gangilonga,kweli pale kamati ya siasa CDM mkoa ilibugi hata mimi niliona,hiyo ndio nakubali tulikosea.Ni kweli wakazi wa pale wasomi,hawahongeki 5000 kama Kitanzini,na walisema wazi CDM Kandideti was not pafect in such maana 2010 magamba walimdiss,ni kama Kosa kamati kuu ilifanya kwa Shibuda,so they are weking on it.Naomba Kukosolewa,nawasilisha.Nitatafuta data furu nhjikipata tym halafu nitaleta kituo kwa kitu.
 
Mimi kama Kiongozi wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nataka kuweka wazi kwamba ni mapema mno kumpima Msigwa utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi kumi na moja tu.

Kwanza yeye alipoingia madarakani alikuta Mbunge aliyemtangulia kachukua mafaili yote ya Ofisi, ikumbukwe kwamba mbunge huyo, Monika Mbega (CCM)alikuwa ni Mbunge wa Iringa mjini tangu mwaka 2000 hadi 2010. Kwa maana nyingine ni kwamba Mbega ameondoka na taarifa rasmi za Ofisi ya mbunge wa Iringa Mjini za kipindi cha miaka 10.

Hivi Msigwa anaweza kujua ni miradi mingapi ilikuwa inasimamiwa na Ofisi ya Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita bila ya kuwa na kumbukumbu za kiofisi ambazo Monica Mbega ameondoka nazo? Kwa mfano ni vikundi vingapi vya uzalishaji mali vilifadhiliwa na ofisi ya mbunge na vilifadhiliwa kwa kiasi gani cha fedha.

Watoto na watu wengine walio kwenye mazingira magumu wamesaidiwaje na Mbunge aliyepita na wako kwenye hatua ipi. Mbega aliwasiliana na ofisi ngapi kwa niaba ya watu wa Iringa na aliwasiliana na ofisi hizo kwa lengo lipi. Hoja yangu hapa ni kwamba kabla ya kumbebesha mzigo mkubwa Msigwa ni lazima kwanza tumsaidie kupata nyaraka hizo muhimu za kiofisi ili aweze kuchapa kazi kiufanisi.

Ni kweli kwamba Msigwa ni mwenyekiti wa Iringa Mjini, lakini swala la Uchaguzi wa kata hizi za Gangilonga na Kitanzini ambazo tulipoteza tulifanya mkosa ya kiufundi kwenye kuchagua wagombea na jinsi tulivyoendesha kampeni zetu. Hakuna wa kumlaumu katika hili, kwani wote kwa pamoja tuliipoanza kampeni tuliamini kwamba tutashinda lakini hali ya mambo baadaye haikuwa upande wetu.

kushindwa kwetu kulitokana na makosa ya kiufundi ambayo hatudhani kama huko tuendako tutayarudia tena. Kitu pekee ninachokiona ni kwamba watu wengi wanafikiri kwa kupambana na Msigwa itakuwa ni rahisi kwao kuwa wagombea wa CHADEMA kwenye nafasi ya Ubunge hapa Iringa Mjini mwaka 2015.

Ushauri wangu kwao badala ya kuanzisha kampeni za kupakana matope na kujifagilia basi tumsaidie Msigwa ili ikifika mwaka 2015 wana Iringa Mjini waone tofauti kati ya mbunge wa CCM na wa CHADEMA. Tunaye diwani mmoja Bwana Nyalusi yeye naye aonyeshe kwenye kata yake ya Mvinjeni jinsi ya kuendesha utawala bora ili mwaka 2015 tuwe na cha kuwaonyesha wananchi.
Asante sana Katibu wa Chadema (Mkoa) kwa ufafanuzi wako na kutoa msimamo wako kama sio wa Chama. Kwa jinsi ninavykufahamu wewe binafsi, Msigwa, Chiku na Mama Mgonukulima naamini kama mnayofanya itatufanya tuendelee kutembea kifua mbele. Bila shaka mmejipanga vizuri kukabiliana na hizi hujuma zinazoanza na kuendelea kujitokeza. Kila la heri Mr Kilewela
 
...hapana, elewemi CCM ni "WEZI" wakati nyie mnahangaika kusema wameshinda kumbe wenzenu walishaiba, mie siamini CCM kama wameshindwa kiukweli, naomba MSIGWA aje hapa atudokeze au kama kuna mtu wa Iringa.

Nimekupata Mkuu,fuatilia hapa chini,kwa kifupi ni Furu kutumia UJAMBAZI na KUTUMIA RUSHWA,na ndio maana Uchaguzi umefanyika Kata 2 wanashangilia Mkoa mzima,what a strange.walikuwa na hamu ni nouma,Siunajua Timu yako mnapofungwa 5-0 mapa dakika ya 89,Mnaanza kufikiria hata Goli la Kufutia machozi kisha mnashangilia KULIKO HATA WASHINDI.Hao ndio Ze-Magambazi,Tamko la Igunga liliwasaidia sana Safari hii.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawgwaa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.

Nimekaa Iringa kwa miaka mitano tangu enzi za mama mbega mpaka sasa anapoanzia Msigwa, kipindi cha kupiga kura sikufanikiwa kupiga kura kutokana na kwamba nilijiandikisha nje ya Iringa. Kiukweli mimi ni mpenzi wa CDM ila ki ukweli Msigwa alishinda kutokana na beef za wanamakundi ndani ya CCM mkoani Iringa na sii kwa sera za CDM. Nimekaa na wanachuo wa iringa waliopambania mabadiliko mkoani iringa kwa kuhamasisha wakazi wa iringa kuwabwaga CCM na kuichagua CDM. Kwa sasa Sipo Iringa tena ila namshauri Msigwa apite mitaa yote ya Iringa hasa mitaa wanayopatikana wasomi kama mitaa ya Contena la Ruco kuna wanaharakati wenye uchu na ukombozi thidi ya CCM inayowakandamiza raia. Msigwa usitegemee mambo yetu ya bungeni tu, fanya mambo hadharani hasa jimboni kwako na wananchi wapendezwe na mienendo yako kwa manufaa yao.
 
Kiukweli mimi ni mpenzi wa CDM ila ki ukweli Msigwa alishinda kutokana na beef za wanamakundi ndani ya CCM mkoani Iringa na sii kwa sera za CDM.

Nimekaa na wanachuo wa iringa waliopambania mabadiliko mkoani iringa kwa kuhamasisha wakazi wa iringa kuwabwaga CCM na kuichagua CDM. .

Hizi dhana mbili kwa ukweli siziamini sana kwani zinawafanya wengine waonekane bora kwa wengine. Kusema kwamba kwa "beef" za CCM ndiyo maana Msigwa akashinda siyo kweli na ni kutaka kuwafanya wana Iringa Mjini hawajui ni nini maana ya mabadiliko. Bifu zao ni kichocheo kilicho wafanya wana Iringa waone kwa urahisi kwamba CCM hawako kwa maslahi yao na hivyo kuigeukia CHADEMA na Msigwa.

Duniani kote wananchi hubadilisha uongozi kutokana na makosa ya uongozi wenyewe. kama siyo sera za CCM kutofautiana na zile za CHADEMA unafikiri wana Iringa wangeichagua CHADEMA? Kulikuwa na mgombea mwingine wa nafasi hiyo hiyo ya Ubunge kutoka NCCR-Mageuzi, Mariam Mwakingwe. Mbona yeye hilo Bifu la wana CCM halikumsaidia kushinda? Ili uweze kumshinda mpinzani wako kisiasa ni lazima uka-pitalize kwenye makosa yake na ndivyo CHADEMA na Msigwa tulivyo fanya na wala si dhambi kisiasa.

Na hii dhana ya kuamini wana Iringa waliichagua CHADEMA kwa sababu ya wanachuo siyo ya kweli hata kidogo ingawa ki ukweli na wao wana mchango wao. Mwaka 1995 hapa Iringa kulikuwa hakuna CHuo Kikuu chochote kile lakini wana Iringa waliichagua NCCR-Mageuzi na Mbunge wake Mfwala Magoha Kibaassa. Hata wananchi wa kawaida ambao si wanachuo wanao uwezo wa kuchambua mambo na kufanya maamuzi sahihi ya kubadili viongozi. Sijui takwimu zinakuonyesha wasomi walikuwa wangapi kwenye uchaguzi wa Mwaka 2010 au ni asilimia ngapi ya wana Iringa Mjini wote.

Naujua na kuuthamini sana mchango wa wasomi katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yoyote ile, lakini sitaki mchango wao huo uwe ni kifungo kwa wengine. Kwa nini tusimhamasishe Msigwa kutembelea watu wake wote badala yake tuna specify kwa wasomi wa kwenye Contena la RUCO ambayo ni sehemu ya kunywea Pombe?

Wasomi waje na vitu Creative na Tangible kwa ajili ya manufaa ya watu wa Iringa halafu hapo ndipo tutaona mchango wao na tofauti yao na wananchi wasio wasomi ,na siyo kumshinikiza Mbunge awafuate kwenye Grocery zinazouza Pombe.

Iringa Mjini kuna Kata 16 na kote huko kuna watu na wanashawishiana wenyewe kwa wenyewe kufanya mabadiliko.
 
Jamani uchaguzi ulikuwa kata za gangilonga kama sikosei, huko ndio wenye neema wana kaa wataitisa ccm kweli?

Umesahau kuwa kata ya Kitanzini pia, kata ya Wahangaikaji wa mjini, inayounganisha eneo la kati kabisa ya mji ikiwepo stendi kuu ya Iringa nayo ilifanya uchaguzi na CCM wakachukua.

Kwa maoni yangu, Mch. Msigwa yupo vizuri kabisa na anafanya alichopaswa kukifanya, tatizo ninaloliona ni kuwa bado CCM ina nguvu mjini Iringa,Wana Iringa hawakuichukia CCM per see bali walimchukia Monica Mbega, ndio maana pamoja na Mch. Msigwa kushinda Ubunge lakini katika uchaguzi uleule CHADEMA iliambulia kiti kimoja tu cha Udiwani huku CCM ikichukua viti 15 hivi kama sijakosea.

So tusitafute mchawi, na kwa hakika kabisa mchawi hawezi kuwa Mch. Msigwa, bali hii iwe ni tahadhari kuwa nguvu kubwa zaidi inahitajika ili kuifanya Iringa kuwa ngome ya CHADEMA, so far bado...
 
Kamwene mna matatizo kweli. Hata mwaka haujaisha tayari Msigwa hafai?
 
Binafsi sioni tatizo juu ya mch.Msigwa sababu ni mpambanaji wa ukweli sana huyu bwana na na2maini anajua matatizo ya wana irnga na yupo kwa ajili ya wananchi kushindwa kwa chadema hzo kata mbili kitanzani na Gangilonga isiwe kigezo cha kumwona mch.msigwa hafai muhimu kwangu 2mpe sapoti na kama kuna ushauri c vibaya kumpatia kwa maendeleo ya jimbo.
 
Bado ni mapema snaa, tumpe muda na tuangalie kama anatuwakilisha vyema. Kinachotakiwa ni uakilishi mwema na sio tu kung'ang'ania magamba wakati yakifika kule yananyamazishwa
 
Binafsi sioni tatizo juu ya mch.Msigwa sababu ni mpambanaji wa ukweli sana huyu bwana na na2maini anajua matatizo ya wana irnga na yupo kwa ajili ya wananchi kushindwa kwa chadema hzo kata mbili kitanzani na Gangilonga isiwe kigezo cha kumwona mch.msigwa hafai muhimu kwangu 2mpe sapoti na kama kuna ushauri c vibaya kumpatia kwa maendeleo ya jimbo.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.

Kwa kata ya Gangilonga ambayo inajumuisha maeneo ya Wilolesi,Gangilonga,Sabasaba nk ni maeneo yaliyoshikiliwa na CCM kwa muda mrefu sana,inawezekana ni kwasababu ya kujaza wakazi wengi ambao ni viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa wa Iringa na kwa upande wa maeneo ya Kitanzini ni uswahili fulani hivi,kuna wazee wa-mji ambao kula yao inategemea fadhila za CCM...nimewai kuzungumza na Mzee mmoja ambaye nilimkuta amevaa sare za CCM na anafanya kazi za kubeba mizigo stendi.Nikamuuliza kwanini unavaa hizi sare wakati wa kazi akaniambia "Mimi CCM siipendi lakini nategemea kula kupitia CCM,akasema hiyo CHADEMA ni ya kwenu vijana" Nilijaribu kumshauri akanielewa vizuri.Nachotaka kusema kushindwa kwa CDM kwenye hizi kata mbili ni tatizo la kihistoria,hizi ni ngome za CCM kwa muda mrefu.......
 
So tusitafute mchawi, na kwa hakika kabisa mchawi hawezi kuwa Mch. Msigwa, bali hii iwe ni tahadhari kuwa nguvu kubwa zaidi inahitajika ili kuifanya Iringa kuwa ngome ya CHADEMA, so far bado...
Huu ni ushauri wa maana sana kwa ajili ya maendeleo ya chama hapa Iringa. Kuhusu ngome ya CCM hakuna ngome isiyowezekana kubomolewa duniani cha msingi ni aina ya nyenzo zitakazotumika.

Kwa mfano kuna watu wanaamini CHADEMA ina nguvu kubwa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro lakini jiulize ni mikoa gani CHADEMA imepata wabunge wengi wa kuchaguliwa na Arusha na Kilimanjaro wametoa wabunge wangapi?
 
nDUGU, HATUNA SABABU yakupinga au kukosoa kila jambo, kama ukweli upo basi tujitahidi kulifanyia kazi ili kuongeza kasi kukubalika.Tukubali pia viongozi wa CDM wote ni binadamu wanaweza kubweteka ila ukweli bado safari ni ndefu sana. Hivyo taarifa za kiutendaji ni muhimu sana kwa kila ngazi.Wanahitaji pia kutoa vipimo vya utendaji kwa kila mbuge,diwadi na mwenyekiti mwenye dhamana. Wasibweteke kamwe na hawana budi kukubali taarifa na uwezo wa waliopewa dhamana na wananchi.
 
Back
Top Bottom