Mbunge wa CCM wilayani Misenyi akimbiwa kwenye mkutano wa hadhara

Uyu mama kinachomponza ni mikopo aliyotoa kwa kina mama ya VIKOBA, wakina mama waliichukua hii mikopo wakishangilia ila kwa sasa imewatokea puani, wanadaiwa na wameshindwa kuirudisha, wanasakwa kila kona na wengine wamekimbia nyumba zao. Hii kitu imepelekea vijana wengi kumchukia uyu mama maana mama zao wanashindwa hata kulima kisa MIKOPO. Hawataki hata kumwona huyu mama. Nakwambia kwasasa hata akisimama mpiga debe anachukua hili jimbo. MISENYI ndo HOME KWETU, tunajuta kumchagua uyu mama ingawa kula zote alizipata toka kwa akina MAMA ambao hivi sasa wamemgeuka.
 
Najipanga 2015 via CDM, najua nitazichota za Minziro, Kajunguti, Katoro, Kitobo, Kanyigo, Mugana, Luzinga, Burembo, Mtukula, Nyankere, Bunazi, Bulifani, Kashaba, Bukabuye, Gera yoo iwe boojo! Assumpita kitu gani bhana! Amechanganyikiwa na mkopo wa crdb, atawakumbuka saa ngapi , wapiga kura!
 
ha ha ha ha ha ha ha vilaza wa CCM nao bana huwa hawana point...wangempa kipigo tu kikaeleweka ingekuwa fresh kabisa
 
Huyu mama kila nikimsikia bungeni au nje ya bunge huwaga anachongea skielewagi zaidi ya kusifia ilani ya chama cha mapinduzi na ahadi za jk,.
 
Uyu mama kinachomponza ni mikopo aliyotoa kwa kina mama ya VIKOBA, wakina mama waliichukua hii mikopo wakishangilia ila kwa sasa imewatokea puani, wanadaiwa na wameshindwa kuirudisha, wanasakwa kila kona na wengine wamekimbia nyumba zao. Hii kitu imepelekea vijana wengi kumch ukia uyu mama maana mama zao wanashindwa hata kulima kisa MIKOPO. Hawataki hata kumwona huyu mama. Nakwambia kwasasa hata akisimama mpiga debe anachukua hili jimbo. MISENYI ndo HOME KWETU, tunajuta kumchagua uyu mama ingawa kula zote alizipata toka kwa akina MAMA ambao hivi sasa wamemgeuka.

Ndiyo maana mabenki wanasema Watanzania hawakopesheki. Hao akina mama warudishe mikopo ya VIKOBA kukimbia kimbia haitawasaidia kitu.
 
2015 nimvae nini? mimi ni mzaliwa wa huko Nkenge nimesomea huko; na ninafahamika vizuri, tatizo baba yangu ni mfuasi wa CCM - sijui niingie kwa ga ipi?

Mi juzi juzi nilikuwa Misenyi nikapata mlo wa mchana hotelini Bunazi (makao makuu ya wilaya hiyo) nilisikia wazungumzaji meza jirani wakisema huyu mbunge wetu hawezi kupata tena 2015. Mi si mwenyeji wa Misenyi wala si mhaya lakini nilisikia kwa masikio yangu mazungumzo ya watu hotelini. Walipoondoka nikaambiwa mmoja ni Mkuu wa wilaya!!!! Nikashangaa nikataka kujua kama halmashauri ina shida, niliposoma taarifa ya CAG nikakuta halmashauri ina 'clean certificate' kwa hiyo ni kweli kwa kiasi kikubwa Assumpta kuna kitu hakiendi sana jimboni kwake Misenyi. Bora gamba liondoke tuingize ladha ya CDM!
 
Tuache porojo hii miaka mitatu tuliyonayo ni muda wa kukijenga chama,kufungua matawi na ku-recruit wanachama wapya ili chama (cdm)kiwe na task force mkoani kagera ila tukikaa hapa na kujiaminisha mwishowe ni kulirudisha jimbo mikononi mwa magamba,maswala ya ubunge mi mwenyewe nagombea kupitia cdm ila kura za maoni ndo zitaamua.
 
uwewe unakujua huko misenyi au ni mpayukaji wa CCM
Kazi ipo kule mimi ni Mbunge wangu natokea kwenye jimbo lake kata ya Kilimilile. Kimsingi yaliyotokea hapo ISHOZI sio ya kushangaa kwa vile sio mara ya kwanza, Mh alishawahi kugomewa tena akihutubia Kijiji cha Membwe kata ya Kilimilile wakati wakamwacha pale wakaondoka zao!
 
Mi nilikuwepo kwenye mkutano wa Asumpta pale ishozi kijiji cha luhano 'asosaiti' kituo cha mazao.alianza kwa kuomba msamaha kwa aliyoyasema bungeni kwamba wananchi wapelekewe mahindi badala ya umeme ndo akaulizwa kama alichaguliwa kwa sababu ya kuwaokoa na njaa akabaki kimya! Akaulizwa kama anakumbuka alichotumwa bungeni akajiumauma ndo watu wakaanza kuondoka,hata hivyo watu walikuwa wachache sana,nilihesabu 32 mimi ni wa 33.
 
Wamefanya jambo la maana sana, walipomchagua walijua wamepata mtetezi wa kweli, bora sasa wameamka!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom