Mbunge wa CCM, Esta Bulaya, Afanya Tukio la Kishujaa Mjini Dodoma!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,179
Wanabodi,

Katika pita pita yangu viunga fulani hapa mjini Dodoma, nimepita mahali nikukata baadhi ya watu na heshima zao, wakimsifu huyu mbunge kijana wa CCM, Mhe, Esta Bulaya, kuwa amefanya tukio kubwa la ushujaa mkubwa katika medani za siasa.

Kwa jinsi nilivyosikia kuhusu alichokifanya mbunge huyu, naomba nikiache kwanza kama tetesi, na nikisha thibitisha, nitarejea kuwapatia ushujaa huo wa Mhe. Esta Bulaya!. Lengo la kuupandisha uzi kabla ya kuutaja ushujaa wenyewe ni kukupa wewe mwana jf ile the jf advantage be the first to know kuwa, Tanzania kumejitokeza shujaa mdogo mwanamke!, ambaye japo ni mdogo na yuko kwenye chama cha majambazi lakini ni shujaa aliyepo in a wrong party!.

Kwa kusaidia tuu, ni kuwa mbunge huyu, amefanya kitendo fulani cha kishujaa kwa kutanguliza mbele maslahi makubwa ya taifa dhidi ya maslahi ya chama chake cha CCM, ambapo ni mbunge pekee mwanamke wa CCM alijitoa mhanga na kusimama kuhesabiwa miongini mwa wabunge wachache wa CCM wenye uchungu wa ukweli na umasikini wa nchi hii, ambao wako tayari kuipigania nchi na kulipigania taifa, kinyume cha wengi wa wabunge wa CCM ambao wameingia bungeni kwa drive ya njaa zao kutafuta maslahi binafsi badala ya maslahi ya taifa, hivyo wanachopigania kule bungeni, na wanachosimamia ni matumbo yao tuu na sio maslahi ya taifa!.

Natafuta kwanza uthibitisho wa huo ushujaa wa Mhe. Esta Bulaya, ili tuliingize rasmi jina lake miongoni mwa mashujaa wa taifa hili!.

Tuvute subira kidogo!.

Wasalaam.

Paskali

Dodoma!.

Kabla ya huo ushujaa, Mhe. Ester Bulaya aliripotiwa hivi humu jf

[h=2]"Re: Godfrey Zambi na Ester Bulaya bungeni waitabiria CCM yao kuanguka mwaka 2015"[/h]

Update 1. jana usiku:
Hatimaye ninepata uthibitisho wa kitendo hicho cha kishujaa cha Mbunge wa CCM, Mhe. Ester Bulaya!.

Licha ya kupata uthibitisho huo, bado kitendo chenyewe sikitaji kwanza mpaka nitakapo pata go ahead ya relevant authorities!, kwa sababu nimeshikwa sikio kwa kuaminiwa as "off the record" hivyo ni busara na ustaarabu kuomba kibali cha aliyekupa tip kuwa unampango wa kuitoa "on the record".

Sababu pekee ya kuleta hii thread ni kuwajulisha tuu kuwa pamoja na ukweli kuwa CCM imeoza kwa rushwa na ufisadi mwanzo mwisho, na wanaitafuna nchi hii kama mchwa, tena ni walafi wa rasilimali zetu kama mafisi wanaoiba hazina yetu waziwazi mchana kweupe kwa kuivuna kama shamba la bibi, ndani ya hao hao mijizi na mifisadi ya CCM, kuna vijana wachache wazuri ambao sio mafisadi na wako tayari kusimama kuhesabiwa!.

Wengi wa wabunge wa CCM wameingia bungeni sio ili kuwatumikia wananchi, bali kujineenesha wao na matumbo yao hivyo mule mjengoni wao wako kutetea maslahi yao!, lakini miongoni mwao, wamo wachache walioingia mle kutetea maslahi ya taifa na Mhe. Ester Bulaya yuu mmoja wao!.

Nitamalizia hivi punde na kitendo chenyewe cha ushujaa wa mbunge huyu baada ya kupata idhini husika.

Kwa wale wenye mcheche sana, samahani sana endeleeni kuvuta subra!. Good things hazihitaji haraka wala papara!.

Na hii ya kutanguliza kupost ni kukuanda wewe kisaikojia kupokea habari za ushujaa ambao wengi hamtaweza kuijua impact yake, bali mtakuja kuijua miaka mitatu baadaye 2015 hivyo wewe mwana jf unakuwa the first to know.

Mfano news za Nundu zilizotokea leo usiku kwenye TV zote leo na zitakatangazwa kwenye kwenye magazeti yote ya kesho, is not news anymore kwa wana jf kwa sababu sisi jf tumeishajua kila kitu tangu mchana! kupitia hapa
Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Asanteni tuhifunze zaidi "managing divesity"

Pasco!.

Update 2: Final Update

Confirmed,

Mhe. Ester Bulaya ndie mbunge mwanamke pekee na kijana shujaa wa CCM aliyesaini ile petition ya Mhe. Zitto kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu!.

Wabunge kutoka CCM jumla ni 6 wakiongozwa na shujaa Mhe. Deo Filikunjombe, Nimrod Mkono, na wengine. Swali ni kwa nini Ester ndio anayestahili pongezi mpaka kumuita shujaa?.

Kati ya wabunge wote waliosaini petition ile kwa upande wa CCM, wengine wote ni wabunge wa majimbo isipokuwa Ester Bulaya, yeye ni mbunge wa kuteuliwa, ni kama mbunge wa hisani wa CCM!. Kitendo cha kutoogopa hisani na kusimama kuhesabiwa ni kitendo cha ushujaa wa hali ya juu sana!.

Wabunge wenzake wote waliosaini ni watu wenye shughuli zao nyingine, ubunge kwao ni utumishi tuu kwa wananchi as a part time job, hivyo kwao lolote liwalo, if anything happens to them in CCM, they have nothing to loose and everthing to gain kwa sababu ni wabunge wa majimbo, CCM ikiwapiga chini bado watayatwaa majimbo yao kupitia chama chochote, na hata wakiukosa ubunge, wataendelea kuishi kwa shughuli zao nyingine, lakini kwa Ester Bulaya, kwake CCM ndio baba CCM ndio mama, Ubunge ndio the only full time job yake, if anything happens to Ester huko CCM, she has everthing to loose and nothing to gain from CCM!.

Hii maana yake ameisha jiandaa kwa 2015 anajua kabisa CCM haiwezi kumpitisha tena!. Ukijumlisha ukaribu wake na Halima Mdee (house mates), then it's obvious 2015 shujaa huyu atakwenda upande wa pili!.

She has the guts to say no to nonsense!. Kuna wabunge wengi wa CCM akiwemo January ambao tuliwaona kama mashujaa, kitendo cha kutomuunga mkono Zitto ni uthibitisho tuu kuwa they are barking dogs only, seldom bite!. They don't have the guts to say no to nonsense!.

Nawaombeni wanabodi wenzangu, mhesabuni Mhe. Ester Bulaya miongoni mwa mashujaa 76 wa taifa kwenye orodha ya Zitto na jina lake liingizwe kwenye list ya mashujaa ambao mwaka 2015 wata team up na timu ya ushindi kuelekea kwenye ule ukombozi wa pili na wa kweli wa taifa letu!.

Kwa wale ambao mtatofautiana na mimi kwenye dhana ya ushujaa, naheshimu mitazamo yenu.

Hongera sana Mhe. Ester Bulaya, CCM watakunyanyasa na kukunyanyapaa, CCM watakutenga, ila kiukweli huko CCM uliko is a wrong party, lakini kwa kusimama kwenye kweli katika hili, naamini 2015 pia utasimama kwenye vyama vya ukweli na sio hao mchwa wanaolitafuna taifa letu na Mungu atasimama na wewe na Watanzania watasimama na wewe, kokote utakakoamua kwenda, Mungu atakutangulia kunyoosha mapito yako, na amini usiamini utashinda na CCM itaaibika.

Ubarikiwe Sana!, wewe ni shujaa wa kweli, mimi nakuita ni shujaa mdogo mwanamke, una very bright future kwenye politics za bongo kwa sababu you have the powers!.

Paskali
 
huyo ndo pasco bana, lazima awasifie magamba ata kama maji yashawafika shingoni, asubili m4c
 
Jamani tusimlaumu huyu pasco kwani huenda alikunywa mvinyo wa dom zas y akawa na haraka ya kupost uhuni wake humu kwani yy ameshindwa nn kusubiri ili apate vithibitisho ndo aje humu jf pia inaelekea anaanza kuwapaka mafuta magamba wenzake.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom