Mbunge wa ccm- luhaga mpina aikataa bajeti kwa hoja nzito ya azimio la bunge

Laptop01

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,365
796
Mbunge wa Kisesa, Joelsn Luhaga Mpina anasema hataiunga Mkono Bajeti ya Serikali kwa sababu imeenda kinyume na Azimio la Bunge ambapo yaelekea Bunge lilikubaliana kiasi fulani cha fedha kitatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa Maendeleo ya Taifa na ktk Bajeti hii kiasi hicho hakiwi reflected, katika hatua nyingine, mbunge huyo ametaja vifungu vya Sheria ya Ukaguzi wa Umma (2008) vilivyokiukwa.

My Take:
Kama Hoja za Mbunge huyo ni kweli, pana udhaifu katika Mihimili hii miwili ya dola (Serikali na Bunge) katika kuifikisha Tanzania katika maisha bora kwa kila MTZ kwani hatutendi kwa misingi ya mipango na sheria zetu
 
JLuhaga Mpina kwa kweli umenifurahisha sana,wewe si mnafiki kama wengine,umesema ukweli mtupu,kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wako,bila kujali itikadi ya vyama.Mungu wangu akulinde na akufanikishe katika mipango yako yote.
 
Inachekesha pale ambapo mtu antekeleza jukumu lake la msingi harafu wewe una msifia excessively. Tutambue kuwa nijukumu la bunge kupitia na kutoa mapendekezo( neg or pos) kabla bajeti haijapitishwa kwa utekelezaji.
 
Mbunge wa Kisesa, Joelsn Luhaga Mpina anasema hataiunga Mkono Bajeti ya Serikali kwa sababu imeenda kinyume na Azimio la Bunge ambapo yaelekea Bunge lilikubaliana kiasi fulani cha fedha kitatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa Maendeleo ya Taifa

Hawakawii kubadilika kama kinyonga, wakishawekwa kikao na LUKUVI kisha kuwatiisha wanabadilika.

YETu MACHO........



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Back
Top Bottom