Mbunge wa CCM kizimbani

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
[h=2]Mbunge CCM kortini kwa rushwa[/h]

Mbunge wa Muheza (CCM), Herbet Mntangi

Mbunge wa Muheza (CCM), Herbet Mntangi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kujibu tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Mntangi alifikishwa mahakamani hapo jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) wilayani hapa akikabiliwa na mashtaka ya kutoa rushwa ya Sh. 135,000 wakati wa kura za maoni za kuteua mgombea ubunge kupitia CCM mwaka 2010 wa jimbo hilo.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salum Msigiti, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, George Magoti , alidai kwamba Mntangi alitoa kiasi hicho cha fedha Mei, 2010 wakati wa kura za maoni.
Magoti aliiambia mahakama kuwa kipindi cha kura za maoni ndani ya CCM alimpa kiasi cha Sh. 135,000 Katibu wa CCM wa Kamati ya Sera na Propaganda wa Kata ya Ngomeni wilayani hapa, Juma Bakari, ili anunue kadi mpya za wanachama na kuwagawia wana-CCM wengine.
“Mheshimiwa hakimu mnamo Mei mwaka 2010, mtuhumiwa alitoa pesa hizo kama rushwa kwa katibu huyo kwa lengo la kuwashawishi wana-CCM wa Kata ya Ngomeni wamchague wakati wa kura za maoni jambo ambalo ni kinyume cha sheria za uchaguzi,” alidai Magoti.
Magoti alidaikuwa mbunge huyo alitoa fedha hizo kwa Bakari ili anunulie kadi mpya za wanachama watakaompitisha kwenye kura za maoni na kupata nafasi ya kuwa mgombea ubunge wa wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini mwaka 2010.
Ofisa huyo wa Takukuru alidai kuwa kitendo hicho ni rushwa kwani fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi wanachama hao ili wampitishe Mntangi kwenye kura za maoni kinyume cha taratibu, kanuni na sheria ya rushwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 5, mwaka huu, upande wa mashitaka utakapowasilisha na kusoma hoja za awali kuhusiana na mashitaka hayo.
Mbunge huyo yupo nje kwa dhamana ya watu wawili wenye mali zisizohamishika.

CHANZO: NIPASHE
 
Mbunge CCM kortini kwa rushwa

hiyo ndiyo ccm bwana, ukitenganisha wizi wa kura na rushwa, matumizi ya vyombo vya dola hakuna ccm..... huyo mmoja ni sawa na tone 1 katika bahari.. sera ya ccm ni kuendeleza rushwa kwa nguvu zao zote na kuzidisha umaskini kwa watanzania
 
Hii habari ilisharushwa humu. TAKUKURU wamejaribu kujitutumua, ila itaishia hewani tu hii kitu. Maana tulishapewa takwimu, zaidi ya asilimia tisini (90%) ya kesi wanazoshitaki hawa TAKUKUTU huwa wanashindwa.
 
Richmond imemponza sana huyu Mzee, sasa wanamnyang'anya na Ubunge.

Mbunge CCM kortini kwa rushwa

Mbunge wa Muheza (CCM), Herbet Mntangi

Mbunge wa Muheza (CCM), Herbet Mntangi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kujibu tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Mntangi alifikishwa mahakamani hapo jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) wilayani hapa akikabiliwa na mashtaka ya kutoa rushwa ya Sh. 135,000 wakati wa kura za maoni za kuteua mgombea ubunge kupitia CCM mwaka 2010 wa jimbo hilo.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salum Msigiti, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, George Magoti , alidai kwamba Mntangi alitoa kiasi hicho cha fedha Mei, 2010 wakati wa kura za maoni.
Magoti aliiambia mahakama kuwa kipindi cha kura za maoni ndani ya CCM alimpa kiasi cha Sh. 135,000 Katibu wa CCM wa Kamati ya Sera na Propaganda wa Kata ya Ngomeni wilayani hapa, Juma Bakari, ili anunue kadi mpya za wanachama na kuwagawia wana-CCM wengine.
“Mheshimiwa hakimu mnamo Mei mwaka 2010, mtuhumiwa alitoa pesa hizo kama rushwa kwa katibu huyo kwa lengo la kuwashawishi wana-CCM wa Kata ya Ngomeni wamchague wakati wa kura za maoni jambo ambalo ni kinyume cha sheria za uchaguzi,” alidai Magoti.
Magoti alidaikuwa mbunge huyo alitoa fedha hizo kwa Bakari ili anunulie kadi mpya za wanachama watakaompitisha kwenye kura za maoni na kupata nafasi ya kuwa mgombea ubunge wa wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini mwaka 2010.
Ofisa huyo wa Takukuru alidai kuwa kitendo hicho ni rushwa kwani fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi wanachama hao ili wampitishe Mntangi kwenye kura za maoni kinyume cha taratibu, kanuni na sheria ya rushwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 5, mwaka huu, upande wa mashitaka utakapowasilisha na kusoma hoja za awali kuhusiana na mashitaka hayo.
Mbunge huyo yupo nje kwa dhamana ya watu wawili wenye mali zisizohamishika.

CHANZO: NIPASHE
 
Kosa lake ni kumshabikia samwel sitta na mwakyembe katika sakata la richmond.
Dr. Hosea na el walisoma darasa moja mirambo sekondary-tabora na baadaye kwenda udsm.
Wana milambo tuambieni kama mlifundishwa ufisadi na kulindana katika dhambi hiyo.
 
Mbona sio siri karibia robo tatu ya Wabunge wa CCM walipita kwa njia hizo za rushwa..! toka kwenye michakato yao ya kura za maoni mpaka kwenye ubunge wenyewe..! Na mpaka rais wao nae kapita kwa njia hiyo.. Haya ya nchi kwenda mrama ndo matokeo yake.. Nchi ikiishakuwa na corrupted leaders haitasonga mbele abadan..
 
huyu jamaa sindoyule aliye pinga hoja ya zitto mbungeni alipowakisha hoja kuhusu katani?? au sio huyu?

nisaidieni.
 
Back
Top Bottom