Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema apelekwa mahabusu

Huu ni usanii wa kijinga na ambao hauna tija. Lema anaonekana kama kituko sasa. Upuuzi mtupu!

nyie ndio wapuuzi mnamkamata kila siku kwa makosa yasio na kichwa wala miguu mnategemea nini? Atakuwa na wadhamini wangapi? Nilijua 2 kikao hiki lema hatakuwepo maana ile hotuba aliyotowa kwenye bunge la budget hakika asinge weza kupona.
 
Katika wabunge wote wa chadema Lema is my hero

Ana akili kama za malcom x..

Watamtoa tu..walichokifanya ni nonsense
\


Yess walichofanya ni NONSESE, kama vile wafanyavyo hawa polisi siku zote kwa sababu tu wanapigishwa kwata na magamba.

Mnakumbuka polisi walivyoumbuka kwa lile sakjata la Kamanda Mbowe 'ku-jump' bail? Kwa kitu cha upuuzi tu (kama hakimu alivyoonyesha baada ya dak 10 tu mahakamani) polisi wa magamba waliliingizia taifa hasara ya mamilioni kwa ajili ya kumsafirisha huyo Kamanda chini ya ulinzi mkali! Nchi hii inafilisiwa na wengi, wakiwamo polisi wa magamba.

Kina Chagonja na Kova walijisikia aibu kubwa sana baada ya lile tukio!
 
Mara kadhaa nmekuwa nasema, Lema ni aina ya mwanasiasa ambaye vichwa panzi wengi watachukua mda sana kumuelewa!
Siasa anayoiwasilisha kwetu kizazi hchi cha masharabaro ni "oversize", siasa ya ukombozi na mapinduzi ya fikra na mtazamo.....

Hata kama wengi wetu tutamwona mwehu na mpenda sifa asiyefaa ila ukweli mchungu utakuwa sisi (wengi wetu) ndio hatujui kipi sahihi kwa mda upi sahihi yatupasa tufanye nini....

Tafakari kuu ni namna ya kuziunga mkono hzi harakati wakati tunaelekea miaka 50 mingine ya "uhuru" (????)
 
Hizi mbwembe zingine bwana... Siasa za utoto.
Uamuzi mzuri waache wananchi wote tuyajuwa unaweza kuuona utoto mpaka mwenyewe yanakutokea yanayomtokea Lema jamani ifike mahali Polisi wafanye kazi zao sio kuvimbisha misuli na ubabe akiiset vizuri hii move inaweza kuleta maajabu
 
Jamani majuzi millya alitoka mahakamani na msafara wa miguu hadi ofisini kwake police hawakumkamata ila lema katoka hivyo hivyo kwa miguu tena na watu wachache anaambiwa kaandamana why Tanzania tuna double standads?

Mwizi wa billion 200 anfungwa miaka miwili na wa milion themanini anafungwa miaka arobaini! Ukiwa na issue bongo kwenye serikali yetu unatafuta unaefahamiana au ndugu! je ukiwa hauna? Hupati fulsa ya kufaidi uhuru aliotuachia Nyerere! Haki sawa kwa wote sio ccm na jamaa zao tu!
 
Ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu .

Hata africa ya kusini kusingetokea watu kama Mandela wakakaa jela miaka kibao kungekua bado uhuru hawajapata. Bila kujitoa muhanga watu kama hawa, tutakua masikini milele kwa ufisadi usio na aibu wala huruma. Nakumbuka kuna mtu mmoja alisema eti akichukua rushwa Mungu amchukue, lakini wala hakemei rushwa hata kidogo. Hivi cheo chake si bora angepewa Lema?
 
mambo mengine bwana, huyu bwana mdogo kupenda sifa na kuwatumia maley man wa arusha ndio nn?

watu wamekuchagua kwa kutaraji maendeleo lkn kila ucho ww na scandal za kijinga kwa nn ?

jifunze bwana mdogo kuendesha siasa za kistaarabu hebu waangalie wenzio wa chama chako mbona hawako kama ww ? au ww tu ndio shujaa na unaonewa ?

Hapo kwenye red, Nani kakudanganya wambunge ndo wanaleta maendeleo. Bora mkae bila mbunge kuliko kuwa na mbunge anaekula kodi za wananchi kwa kupiga tu makofi mbungeni
 
Mara kadhaa nmekuwa nasema, Lema ni aina ya mwanasiasa ambaye vichwa panzi wengi watachukua mda sana kumuelewa!
Siasa anayoiwasilisha kwetu kizazi hchi cha masharabaro ni "oversize", siasa ya ukombozi na mapinduzi ya fikra na mtazamo.....
Hata kama wengi wetu tutamwona mwehu na mpenda sifa asiyefaa ila ukweli mchungu utakuwa sisi (wengi wetu) ndio hatujui kipi sahihi kwa mda upi sahihi yatupasa tufanye nini....

Tafakari kuu ni namna ya kuziunga mkono hzi harakati wakati tunaelekea miaka 50 mingine ya "uhuru" (????)
Mkuu, Lema is something else...........kuanvichwa ninavyovijua mimi vinaweza kuwa kama yeye lakii havijawa kwenye political area aliyokuwa nayo Lema.

However, Lema amesema ''kuwa kwangu huru hakuna maana, kwani watatafuta jingine, ina maana zaidi kuwa sehemu wanayotaka na watanzania wengine..........kumbuka jana alisema nimeshawaandaa familia yangu.........intelijensia ilishaonyesha kuwa wanataka kumpeleka mahakamani leo na akaamua haina maana kuwa huru kwa udhamini wakati uhuru huo hauna maana.
 
Jamaa kasema anaenda kwa hiari yake na ndio maana kaanda kabisa waraka, nadhani anaenda kuweka mkakati mwingine huko huko jela, kakataa dhamana yeye mwenyewe sio kwamba kakosa dhamana, soma uelewe hio attachment.

Kaenda kuweka msingi imara huko sasa nyie vibaraka wa Magamba endeleeni tu kupiga domo ili mpate msosi wenu lakini ndio jamaa anajenga mazingira mzaruri zaid ya kuwaumbua kwenye bunge na nina uhakka ataibuka na ripoti maalumu toka jela....hakutaka ubunge kama ajira aliutaka ili auonyeshe ulimwengu kuwa anaweza.....
 
jamani majuzi millya alitoka mahakamani na msafara wa miguu hadi ofisini kwake police hawakumkamata ila lema katoka hivyo hivyo kwa miguu tena na watu wachache anaambiwa kaandamana why Tanzania tuna double standads?

Mwizi wa billion 200 anfungwa miaka miwili na wa milion themanini anafungwa miaka arobaini! Ukiwa na issue bongo kwenye serikali yetu unatafuta unaefahamiana au ndugu! je ukiwa hauna? hupati fulsa ya kufaidi uhuru aliotuachia Nyerere! Haki sawa kwa wote sio ccm na jamaa zao tu!!

Double standards na unafik, yaani kukosekana haki, ndiyo vitaiangamiza CCM na serikali yake. Bado kidogo tu.
 
Huu ni usanii wa kijinga na ambao hauna tija. Lema anaonekana kama kituko sasa. Upuuzi mtupu!

lkn kumbuka hii ni inchi yetu wote,na ilo tukio limetokea kwasababu lema yupo,ili atutetee wajnga,wapuuzi wasio na tija yaani mapanya kama mnavyotuita,shukuru Mungu chalii wangu ckujuii ila waza basi ata 2po tanzania bana na tuna haki ya kuishi tanzania
 
Good realization....
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.

Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba,
NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.
Na sasa siwezi kukaa kimya tena.NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote,mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.
Nimegunduwa kwa muda mrefu tumetawaliwa na viongozi wasiowafahamu wananchi wala kujuwa shida zao.

Nimegunduwa viongozi wanaishi maisha ya tofauti sana na wamekuwa wakiishi hivyo kwa muda mrefu na wameona kuwa ni haki yao waishi hivyo....

Ndo maana kuna watu wanshangawazwa na Lema.

Watu kama Lema ndo wengi nchini sema siyo tabaka la uongozi,na ndiyo maana tabaka la uongozi wanashangazwa.

Kumbe wananchi wakilia shida wao wanadhani ni uhuni.

Ni vyema wananchi wakaacha kuchagua viongozi walioko kwenye tabaka la uongozi pamoja na sympathizers wao kama ni kweli wanataka ukombozi.

Wananchi sasa ni wakati wa kuweka viongozi madarakani ambao wanajuwa wananchi wana shida gani.

No wonder mkuu wa nchi hajui shida zetu!
 
Hongera Lema hakika wewe ndiye Kiongozi unaetufaa haswa katika kipindi hiki ambacho watz tunataka haki... OCD Zuberi aliwaita vijana (Wapenzi wa Lema) PANYA walipokuwa mahakamani wiki iliyopita. Sasa ni aluta kontinua.
 
Cdhani kama kuna ukweli hapa!ngoja ntajaribu kupata ukweli!najiuliza iweje Lema akose wadhamini hapa?sijui
nadhani ungejitahidi kusoma hiyo meseji ya lema kwa ufasaha ukaelewa. hakukosa wadhamini ila kagomea dhamana kama njia ya kufikisha changamoto kwa umma kwamba jela, polisi na mauti haviwezi kuzuia mageuzi ya kweli dhidi ya manyanyaso, dhuluma, uonevu na ukandamizi.
 
mambo mengine bwana, huyu bwana mdogo kupenda sifa na kuwatumia maley man wa arusha ndio nn?

watu wamekuchagua kwa kutaraji maendeleo lkn kila ucho ww na scandal za kijinga kwa nn ?

jifunze bwana mdogo kuendesha siasa za kistaarabu hebu waangalie wenzio wa chama chako mbona hawako kama ww ? au ww tu ndio shujaa na unaonewa ?
Tupia na upande mwingine wa shilingi jee Serikali ya Tanzania na Polisi wanatenda haki kwa mbunge huyu huwezi amini CCM yote na mwenyekiti wao Mh Mrisho Jakaya Kikwete wametumbukia nyongo kwa kutaka kumtoa roho kijana huyo siasa gani za maguvu si warudishe utawala wa chama kimoja tujue moja basi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom