Mbunge wa Arumeru mashariki mbona hasomeki?(Sumari)

saxzu

Member
Oct 31, 2011
37
3
Yapata mwaka sasa lakini mbunge wa Arumeru Mashariki hatujui alipo wala hatuna taarifa sis wananchi wa jimbo hilo Bunge la bajeti mpaka limeisha hatujamuona nafikiri hata ajaapishwa: Ni hoja 2 namulizia Mbunge wangu
 
yupo ICU!kwa ufupi hamna mbunge kwa sasa!kabla hata ya uchaguzi alikua mgonjwa kalazimisha kugombea ubunge matokeo yake hata kuapishwa sidhani kama alifanikiwa
 
Anapumua kwa mashine!
Kwa kifupi yeye ni mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki, hata kuapishwa hajaapishwa
 
Sheria inasemaje? mbunge akishachaguliwa aapishwe baada ya siku ngapi la sivyo uchaguzi urudiwe? Imekula kwenu wana Arumeru Mashariki, mmechagua mzuka
 
Ni kweli kuwa hakuapishwa? Na kama yuko ICU, incapitated, nadhani itakuwa vyema kama wangeitisha uchaguzi mwingine.
 
Ama kwel hata mimi nilishawah kujiulza maswal kama hayo! Huyu jamaa nasikia huwa haishi huku tz(arumeru) sasa cjui anaish wapi! Mi nadhani Wana arumeru(Wameru) wameshashikwa,na wajifunze kutokana na makosa. 2015 ndo hyo inakuja,je wananchi bado mtaendelea kumpa kula???
 
Hi ni kutoka kwa eyewitnes. J2 nilibahatika kukutana na Jerry Solomon kanisani karibu na home kwake huko meru akeri. Ukweli anaonekana ameshoka sana na kama vili anatatizo la kupoteza kumbukumbu. Nasema hivi kwa sababu hiyo siku kulikuwa na harambee, basi alipotajwa ili atoe mchango yeye akaanza kuimba. Akaimba wee hadi wife akamfuata na kumbembeleza amalize wimbo. Kisha akatangaza hajui mkewe ana umri gani kwani siku hiyo iligongana na birthday ya mkewe. Akaimbisha kanisa 'happy birthday to you'. Kwa kifupi magamba hawana mgombea kwa sasa ndiyo maana hawaitishi uchaguzi.
 
Sasa Hapa Arumeruike coz nini kifanyike inavyoonekana ni kwamba Magamba wamekausha hata hawazungumzii ila ingekuwa ni pale Arusha town ungesha itishwa uchaguzi. ni hatua gani zifwate ili huu uchaguzi ufanyike?
 
CDM tunasubiri kulichukua jimbo letu walilochakachua kina EL mwaka jana wakampa huyo magamba ambaye ni mkwe wake
 
Hizo tshirt, kanga na kofia za mia5 mlizopewa mkamchagua mgojwa aliyekuwa ICU mnazo mpaka sasa.? Nawauliza wana Arumeru mashariki mjibu hili swali. Kuna watu wa kule Ngabobo, Leguruki, Ngarenanyuki wanatumia usafiri wa punda mpaka leo hakuna barabara ya kupita gari. Hakuna maji, umeme wala hospital. Maeneo ya Ndoombo, Ulonga, Seela, Songoro, Urisho, Mulala, Kilinga kwa gari dogo kufika kule ni sawa na kakakuona kuonekana. Barabara ya kwenda kwenye machimbo ya Tanzanite inayojulikana ni madini ya thamani duniani hapitiki. Wameru amkeni sasa achaneni na magamba.
 
yule mzee alipooza halafu ana ugojwa wa alzheimer ( ugonjwa wa kusahau)...
 
HABARI ZA KUAMINIKA ZINASEMA KWAMBA wazee na vijana wa arumeru wanaijubali sn chadema na waliimpigia kura kwa wingi sn mgombea wa chadema na AKASHINDA lkn kwa uzandiki na wizi wa ccm wakachakachua matokeo na KUMTANGAZA MBUNGE HY WA CCM kuwa ndio mshindi aliyempiku wa cdm kwa kura chache sn, kitendo hch KILIWAUDHI SN WAZEE WA ARUMERU WAKAMWAPIA MBUNGE HY KUWA KAMWE HATOKANYAGA BUNGENI, ghafla mbunge hy akapata kansa ya ubongo hvy hajaweza kwenda bungeni wl hajaapishwa, na hali yk ni mbaya kwani amepoteza kumbukumbu kbs. MAONI YNG: CCM ACHENI WIZI WA KURA WATU WAMEWACHOKA MTAISHIA PABAYA
 
Yani ni mahali penye neema ila pana shida hadi mwisho hata maji hayaonekani jimbo zima Linabank 1 CRDB then wafanyakazi wengi hususani walimu ni NMB wanalazimika kutoka kilinga,songoro,ngateu kwenda clock tower kufata hela simuombei mabaya huyo Mbunge ni bora akubali matokeo sasa kama hakumbuki atakuja kufanya nini tena Walimchakachua Josh Nasari sasa imekula kwetu tatizo lingine wazee wanalinda Chama na hawaangalii nin kinachoendelea.
 
Ugonjwa hauna mwenyewe, tusishangilie, tusiwaumize zaidi ndugu zake ambao wanateseka bila shaka kumhangaikia ili apone na kuendelea kuihudumia familia yake. Tusishabikie ugonjwa wa mtu kisiasa. Ilikuwa kosa la magamba kung'ang'ania kuchukua jimbo hata kwa njia ya wizi wa kura ilhali wakijua mgombea wao alikuwa mgonjwa. Tumwombee Jerry apone maradhi hayo kama ni mapenzi yake Mola ili atumikie wana Arumeru. Ikidhihirika kinyume chake, basi achaguliwe mbadala, hapo twaweza kushangilia kwani Mgombea Chadema aliyedhulumiwa haki yake, njia ya ushindi itakuwa nyeupe. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wape uvumilivu wana Arumeru. Mungu mpe afya Jerry S.
 
Jamaa yuko kule juu Akheri anapelekwa tu church na ile V8, afya yake imedhoofu sana.
 
Back
Top Bottom