Mbunge Viti Maalum Shinyanga Mjini, LUCY MAYENGA azomewa.

Jiwejeusi

JF-Expert Member
May 3, 2011
754
131
Ni katika harakati ya kujivua gamba na kuinusuru CCM mkoani shinyanga. Mbunge wa CCM viti maalum, LUCY MAYENGA amejikuta akipata aibu ya kuzomewa. Dhahama hiyo ilitokea baada ya mbunge huyo kutaka kuwarubuni vijana kwa kusema atawapatia misaada na mikopo ya wajasliamali. Vijana hao wa stendi ya basi walimzomea na kumwambia hatutaki misaada.
 
Duh sasa CCM naona wataanza kutembea na polisi kwakuwa zomea zomea inawakera sana sana .Walizoea kuwadanganya watu sasa ukweli uko nje hawezi tena kusema lolote
 
Ni katika harakati ya kujivua gamba na kuinusuru CCM mkoani shinyanga. Mbunge wa CCM viti maalum, LUCY MAYENGA amejikuta akipata aibu ya kuzomewa. Dhahama hiyo ilitokea baada ya mbunge huyo kutaka kuwarubuni vijana kwa kusema atawapatia misaada na mikopo ya wajasliamali. Vijana hao wa stendi ya basi walimzomea na kumwambia hatutaki misaada.

Good, hadi hapo watakapojua athari za ahadi hewa na kwamba ubunge ni utumishi na si ubwana!
 
Mbona na wao wanawazomea Wabunge wetu wa Chadema pale tunapoteyea kitu kwa maslahi ya Watanzania?,acha na hao wa ccm wazomewe kbs na safari hii ole wao wabunge wa magamba(ccm)wawazomee wabunge wangu wa Chadema.
 
waache wazomewe, kama wao wanazomea mahala patakatifu (bungeni) itakuwa wananchi kuzomea barabarani?
 
Chadema inachekesha kweli inajenga Taifa la wazomeaji ili ije itawale taifa la wazomeaji! Kweli nchi haita tawalika!
 
Ni katika harakati ya kujivua gamba na kuinusuru CCM mkoani shinyanga. Mbunge wa CCM viti maalum, LUCY MAYENGA amejikuta akipata aibu ya kuzomewa. Dhahama hiyo ilitokea baada ya mbunge huyo kutaka kuwarubuni vijana kwa kusema atawapatia misaada na mikopo ya wajasliamali. Vijana hao wa stendi ya basi walimzomea na kumwambia hatutaki misaada.

Acha uongo
 
hii ni TRY and ERRO
wanajua wana mvuto ila wanajaribu ni nani mwenye nafuu
ndio maana Mukama yeye kakimbilia kusema kwao MUSOMA (wapoti bwana)
 
Chadema inachekesha kweli inajenga Taifa la wazomeaji ili ije itawale taifa la wazomeaji! Kweli nchi haita tawalika!

Kwani nani alianzisha hayo mambo ya kuzomea? Ni CCM wenyewe unakumbuka waziri mkuu aliwambia wananchi wazomee mafisad! Au umesahau! Na je wenye tabia ya kuzomeazomea bungeni ni wabunge wa chama gani ka sio chama cha magamba, na wananchi wanapractise mlichowambia kupitia PM, na kuona kupitia wabunge wetu wa CCM
 
Chadema inachekesha kweli inajenga Taifa la wazomeaji ili ije itawale taifa la wazomeaji! Kweli nchi haita tawalika!
Mkuu tabia ya kuzomea sio nzuri kabisa na haikubaliki.lakini kumbuka ya kuwa wateule wa wananchi ambao ni wabunge wetu ndio wanaongoza kwa kuzomea tena wakiwa wanaonyeshwa live na television kutokana na hilo mimi naamini kabisa bunge letu linapandikiza tabia ya ajabu kwa vijana wa kitanzania, ni muda muafaka sasa vyombo vya habari kuanza kuwaelimisha hawa wabunge kuondokana na hii aibu
 
Chadema inachekesha kweli inajenga Taifa la wazomeaji ili ije itawale taifa la wazomeaji! Kweli nchi haita tawalika!

Mbungeni ccm huzomea hivyo sioni ajabu na wao wakizomewa uraiani tena ikibidi watwangwe mawe kabisa pumbavu zenu..
 
Action and reaction are equal and opposite tabia ya kuzomea inayofanyika bungeni hasa ktk masuala yanayohusu maisha ya watanzania na hao wabunge walio na magamba lazima waipate huku nje hiyo ni laana yao bungeni wanafanya ushabiki wa kitoto ku-support mambo ya kijinga kabisa mradi tu aliyezungumza anatoka chama chake,acha wazomewe sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hilo group la kina Lucy Mayenga ndilo la wazomeaji wakubwa bungeni kwa sababu hawana wanayemwakilisha humo mjengoni. Kwa mfano Mayenga anaongea na vijana wa shy mjini yeye kama nani??

Hatujasikia hata siku moja anachangia kitu chochote bungeni, hawa ndo wale wa kupiga makofi yale ya kinafiki bungeni. Asijisumbue kujizulia mabalaa bure akae tu ale bure, kwani anadaiwa na nani. Hana anaowawakilisha yeye amwangalie aliyemteua, atuache sisi wana Shinyanga tunajua hatuna mbunge baada ya kifo cha Shelembi(RIP). Tusubiri 2015 au sheria itakavyosema.
 
Back
Top Bottom