Mbunge viti maalum aibiwa baa!

Mwacheni!
Kwani kuwa baa dhambi?

Mama wa watu amekuwa confused na hali mbaya ya mjengoni ndo maana aliamua kunywa
 
Inasikitisha sana,mbunge kaibiwa watu wanafurahia!kwani na yeye si binadamu kama nyinyi
 
Wezi balaa kweli, wanakuibia halafu wanakuaga "TUKO PAMOJA"! Hawana tofauti na politician fisadi.
 
mbunge wa viti maalum ccm kutoka mkoa anakotokea Pinda ameibiwa baa usiku wa saa nane za usiku akila bata huko Dodoma.
Source: wapo Radio.

Mwanamke yuko baa mpaka saa nane!!!!!!! anyway kwakuwa ni wa CCM ni vizuri akajionea amani wanayoringia kama chama
 
we vipi mwenzako alikuwa ananpunga upepo ili auone unavyo pita vizuri aaaaaaaaaaaaaaaaaaahh
du nimesahau kuwa wao ndo mabingwa wa skendo
 
Kwa mantiki ya Kiswahili, mtu hawezi "kuibiwa". Kimsingi, hakuna kitu chochote "kinachoibiwa", ila, mali huibwa.

Ulipaswa kuandika "mali za mbunge wa viti maalum zaibwa akiwa bar...."

Kiswahili ni kigumu, tusiwe wepesi kuendelea kukubali makosa makubwa, kama vile wanaosema "nyimbo hii" wakati walipaswa kusema "wimbo huu".

Kiswahili sanifu: Mbunge kaibiwa mali zake,
 
Anaitwa pudesiana Kwembe!!!!!!!!

alafu juzi tu katangazwa bungeni anaitwa dokta pudensiana kikwembe phd
 
Kutoka Dodoma Sifa Lubasi anaripoti, kwamba Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Pudenciana Kikwembe (44), kutoka Mkoa wa Katavi, amevamiwa na kuporwa fedha na kadi tatu za benki wakati akiwa kwenye baa ya Lady May barabara ya Iringa mjini humo.

Akisimulia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8.30 usiku wa kuamkia jana kwenye baa hiyo. Alisema mtu asiyefahamika, alivamia baa hiyo akiwa na gobori na kumpiga risasi ya mguu mkaanga chipsi, Ally Kubula (22). Alisema baada ya kumjeruhi mkaanga chipsi huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma akitibiwa majeraha, alipora mikoba miwili; mmoja ukiwa wa Mbunge huyo wenye dola 600 za Marekani, Sh 180,000 na kadi za benki za NMB, CRDB na NBC.

Pia alipora mkoba mwingine wa Sharon Tuli, rafiki wa Mbunge huyo, ukiwa na simu mbili na Sh 100,000. Kamanda alisema juhudi za kumsaka mtu huyo zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kupitia sera ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi, kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha wanabainika na kuchukuliwa hatua stahiki.

Kupitia mtandao wa kompyuta, Mbunge huyo alikiri kuporwa fedha na kadi za benki. “Ni kweli kwamba tukio hilo lilitokea jana (juzi) saa 2.30 usiku katika baa ya Lady May Pub, iliyoko barabara ya Iringa … nilifika mahali hapo kupata chakula na kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu zilizoko Dodoma wanaotoka Rukwa na Katavi kuhusu mambo mbalimbali,” alisema Mbunge.

Habari Leo
 
Hiyo mikutano ya usiku wa manane na wanafunzi wa vyuo vikuu haileti ukweli kwa maana anachelewesha wanafunzi kupumzika na kuwahi madarasani kwa ajili ya kufanya tafrija usiku. Wanafunzi hao ndio waliomtolea uvivu.
 
Yeye alikuwa amewakusanya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka mkoa wa Katavi na Rukwa kwa ajili ya kumtetea Picha asipigiwe kura ya kutokuwa na imani, je anajua itikadi za wengi wa wanafunzi hao wa vyuo vikuu kutoka huko kulyamba la mfipa? Je wanafunzi hao wana uwezo wa kusitisha hoja ya waheshimiwa wabunge? Mkoba ulioibwa ulikuwa na pesa za kuwahonga wanafunzi wa vyuo vikuu watoka kulyamba la mfipa?
 
SAM_1057.JPG


Mbunge viti Maalum CCM aliyeporwa Bar.
 
Hajaibiwa zimerudi kwa wenyewe, kama wanawatetea mafisadi wao wafanyweje, kumbe wizi mbaya eeeeee, Ya Malima yasije.....rudia
 
Siwapongezi majinzi,bt katika enzi hizi za kuongezeka gap kati ya wenye nacho na ambao hawana,linaweza likawa fundisho.Alitakiwa aje huku kwa wapiga kura wake at least angewaungisha wao.Lakn silahumu sana coz ni special chair
 
Back
Top Bottom