Mbunge Ukonga: Uamuzi chenji ya rada uharakishwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
SERIKALI imetakiwa kuharakisha utekelezaji wa uamuzi wa jinsi ya kutumia chenji ya rada katika kuboresha elimu nchini.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Eugen Mwaiposa alipokuwa akizungumzia changamoto zinazolikabili jimbo lake mkakati wake unaoendelea wa kukutana na wananchi wa jimbo lake katika kila mtaa.

Alibainisha kuwa mikutano hiyo itahusisha mitaa 19 kati ya 36 ya jimbo hilo, ambapo Juni 2, mwaka huu atakutana na wananchi wa mitaa ya Tungini, Chanika wakati siku inayofuata Juni 3 atakutana na wakazi wa mitaa ya mazizini, Ukonga ikijumuisha maeneo ya Kipunguni, Malkaz na Madafu.

"Ni muhimu kwa Serikali kuharakisha utekelezaji wa uamuzi wake. Chenji ya rada ifanyiwe uamuzi haraka ili zisaidie kuboresha elimu kwa kuwa shule nyingi zina hali mbaya na wanafunzi wengi wanakaa chini kwa kukosa madawati," alisema.

Alifafanua kuwa elimu ni moja ya maeneo yenye changamoto kubwa katika Jimbo la Ukonga huku kukiwa na upungufu wa madawati na idadi kubwa ya wanafunzi.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ubovu wa miundombinu hasa barabara, zahanati na vituo vya afya kukosa umeme, pamoja na uhaba wa maji akitaja maeneo ya Gongo la mboto, Mongo la ndege, Chanika na Msongola kuongoza kwa tatizo hilo.

Alisema kuwa ziara yake katika mitaa ya jimbo hilo kutoa mrejesho wa changamoto mbalimbali zilizotokana na mkutano wake na viongozi wa Serikali za Mitaa, kueleza utendaji wa kazi na kukusanya kusikiliza kero za wananchi, ambazo ataziwasilisha katika kikao kijacho cha Bunge.

Aliongeza kuwa atatumia mikutano hiyo pia kuwaelimisha na kuwahimiza wananchi kushiriki katika kutoa maoni kuhusu katiba mpya pamoja na sensa.
Mbunge Ukonga: Uamuzi chenji ya rada uharakishwe

 
Back
Top Bottom