Mbunge Sumari azidiwa, anapelekwa India leo

Well kama hata Kampeni "alisaidiwa" sidhani kama ni tatizo la madaktari au ni yeye tamaa yake binafsi ya madaraka!

Na kama alikuwa Waziri akashindwa kumshauri Rais and Co.. kuwa Tuboreshe Hospitali zetu e.g. Muhimbili ili waweze kutibiwa Wa-Tanzania wengi hasa wale ambao hawawezi kwenda India...

Sina haja ya Kumuombea Mema hata kidogo - Huwa sipendi Unafiki hata kidogo
 
Taarifa ni kwamba amepata tatizo kubwa katika ubongo wake ambako madaktari wamegundua kitu kilichoota ndani ya kichwa, kitu ambacho kinaathiri ubongo wake kiasi cha kupoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili wake. Sumari ambaye alilazimika kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anaondoka leo kwa ndege ya Oman Air.

Huyu tayari ni incapacitated, sijui wanasubiri nini kutangaza jimbo kuwa wazi.
 
hakuwepo bungeni muda sana Ina maana mpaka sasa anakula posho tu?!
Geti weli soni mbunge Shumariii.
 
kama ni mbunge harali mola amponye ampe uzima arudi kuwatumikia wananchi kuhusu mengine mi sisemi maana siwapendi wezi wa kura.......ila kila nafsi itaonja mauti
 
Mbona wamemchelewesha sana kumpeleka huko India? Hii ni misimanejementi kwa mgonjwa, angekuwa amepelekwa India mapema wakati bado ugonjwa haujashika kasi kwa nguvu.
 
"na wewe (Dr Slaa) tafuta hoja nyingine" by jeremiah sumari june 2009.

kauli hii ilitolewa bungeni na mhe.Sumari (naibu waziri wa fedha) wakati akijibu swali la nyongeza la Dr. Slaa kuhusu kufanya ukaguzi wa mahesabu ya meremeta na tangold.

kesho yake...
"waziri amejibu majibu ya hovyo hovyo" by zitto kabwe.

ugua pole mhe sumari, tupo nyuma yako katika sala.
Kumbe alikuwa hapingi ufisadi na bado kapelekwa India kwa kodi za wananchi?

Only in TZ.
 
Nakumbuka akiwa Naibu waziri wa mipango alishawahi mjibu jibu la hovyo sana Dr Slaa wakati anaulizia swala la Deep Green na Meremeta. Akijibu kwa hasira alisema "Na wewe huna kitu kingine cha kuongea kila siku meremeta tu". Kauli hii ilikuwa mbovu sana na kwa upande mmoja alimdharirisha mbunge mwenzake. Watu wa design ya Sumari bora waishie India hukohuko, kwani hili ndio lilelile genge nyonya nchi. Kama mungu atamua kuwapunguza kwa style yake bora awamalize tu kwani sisi wanamapinduzi hatuna sumu ya kawatega wanyonya nchi ili ikuwatokomeza kama wao wanavyofanya
 
Jamani tumuombeeni apone, tuweke pembeni politics, binadamu tupendane,hii ndio amri kuu.!
 
Nakumbuka akiwa Naibu waziri wa mipango alishawahi mjibu jibu la hovyo sana Dr Slaa wakati anaulizia swala la Deep Green na Meremeta. Akijibu kwa hasira alisema "Na wewe huna kitu kingine cha kuongea kila siku meremeta tu". Kauli hii ilikuwa mbovu sana na kwa upande mmoja alimdharirisha mbunge mwenzake. Watu wa design ya Sumari bora waishie India hukohuko, kwani hili ndio lilelile genge nyonya nchi. Kama mungu atamua kuwapunguza kwa style yake bora awamalize tu kwani sisi wanamapinduzi hatuna sumu ya kawatega wanyonya nchi ili ikuwatokomeza kama wao wanavyofanya
Nakubaliana na wewe mkuu.
 
Hali ya afya ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari, si nzuri na mchana huu anasafirishwa kwenda India kwa matibabu. Sumari ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, alianza kuugua hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambako baadhi ya maeneo alilazimika kusaidiwa kampeni. Tunamuombe Mungu ampe afya njema arudi kujenga Taifa.

Taarifa ni kwamba amepata tatizo kubwa katika ubongo wake ambako madaktari wamegundua kitu kilichoota ndani ya kichwa, kitu ambacho kinaathiri ubongo wake kiasi cha kupoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili wake. Sumari ambaye alilazimika kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anaondoka leo kwa ndege ya Oman Air.

Iliwahi kuzungumzwa hapa, japo baadhi yetu tulijadili bila utu. Tujaribu kuweka ubinadamu mbele, siasa baadae.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mbunge-wa-arumeru-mashariki-ni-mgonjwa.html

Mungu awaongoze madaktari wamaomtibu ili wamsaidie apone
 
Back
Top Bottom