Mbunge Sumari azidiwa, anapelekwa India leo

Halisi, asante kwa taarifa hii.
Wana jf wenzangu, hawa hate preachers humu, wasio na ubinaadamu, wataifikisha jf pabaya!.

Kama alivyosisitiza Halisi, utu na ubinaadamu mbele.

Get well soon Mhe. Jerry Solomon!.

Pasco.
 
Ubinadamu mbele namtakia asafiri salama na Mwenye enzi Mungu ampe baraka apone na kurudia afya yake. Masikini watu wa jimbo lake wamekaa miezi mingi bila mwakilishi wao kufika bungeni, hata kule kluapishwa tu, sijui CCM yetu ilianfgalia wapi ikachagua mgombea mgonjwa!! Ushauri wa bure, akipata nafuu ajiuzuru ubunge kutoa nafasi uchaguzi kurudiwa na wengine wagombee na kuwapa uiwakilishi wananchi.
Tunamwombea apone haraka, lakini hapa tunajifunza kitu gani, unafiki wa CCM kujifanya wanawapenda sana viongozi wao huku wakiwaacha wananchi hasa wa jimbo lake wakihangaika bila mwakilishi, naomba akirudi awe amepona au...aapishwe ili aendelee kupokea posho hadi bunge livunjwe mwaka 2015 kama katiba inavyosema.
 
"na wewe (Dr Slaa) tafuta hoja nyingine" by jeremiah sumari june 2009.

kauli hii ilitolewa bungeni na mhe.Sumari (naibu waziri wa fedha) wakati akijibu swali la nyongeza la Dr. Slaa kuhusu kufanya ukaguzi wa mahesabu ya meremeta na tangold.

kesho yake...
"waziri amejibu majibu ya hovyo hovyo" by zitto kabwe.

ugua pole mhe sumari, tupo nyuma yako katika sala.
 
Ugua Pole Jerry, nakuombea urudi salama na ukifika tu nenda kaongee na wale wazee wakimeru (washili) na uwaombe msamaha.

Getwell soon
 
Tunashukuru kwa taarifa yako, na tumwombee Mungu amjalie afya njema arudi kuliwakilisha jimbo lake na kuendelea utumishi wake kwa taifa.

Tofauti za kiitikadi si chuki kama wengi wetu tulivyozoea kuziendesha hapa, tunashindana kwa hoja ndio maana ya demokrasi, lakini wakati huo huo tunatakiwa kudumisha utu na upendo kati yetu ndiyo silaha kubwa ya kutunza amani katika nchi yetu.

Umesema kweli mkuu. Tusiwe washabiki wasio na hekima wala busara.
 
Sure mdau
Sawasawa kabisa, hospitali za India kwa sasa ndio zimekua hospitali zetu kubwa za rufaa! Why not? Tuko busy na kuponda hela kusherekea miaka 50 ya uhuru, hatuna pesa za kurekebisha na kununua vifaa vya kisasa Muhimbili, sisi sio wajinga bwana, we know what we are doing!
 
Halisi, asante kwa taarifa hii.
Wana jf wenzangu, hawa hate preachers humu, wasio na ubinaadamu, wataifikisha jf pabaya!.

Kama alivyosisitiza Halisi, utu na ubinaadamu mbele.

Get well soon Mhe. Jerry Solomon!.

Pasco.
Pasco, utu haupimwi kwa kumhurumia mgonjwa tuangalie pia upande wa pili anaowawakilisha, alipogundua kuwa anaumwa na hawezi kuwahudumia kwa nini hajiuzulu kupisha mwingine, ina maana yeye hawahurumii akina mama wajawazito pale Tengeru wanaosumbuka kupanda bajaji kwa kukosa mwakilishi bungeni?
 
Halisi, asante kwa taarifa hii.
Wana jf wenzangu, hawa hate preachers humu, wasio na ubinaadamu, wataifikisha jf pabaya!.

Kama alivyosisitiza Halisi, utu na ubinaadamu mbele.

Get well soon Mhe. Jerry Solomon!.

Pasco.
 
Japo magamba siwapendi lakini kama binadamu tunamtakia heri apone haraka aje kutekeleza ahadi alizo ahidi kwenye kampeni.

Pipoz power!

Mi mwenyewe NAFSI yangu sitaki hata kuwasikia na ukisema arudi aje atekeleze ahadi zake,hakika itakuwa ngumu! Na kuna tetesi ya kwmb ameachana na mambo ya siasa! Na bila shaka anakula mshahara na hata posho ya Ubunge anachukua!
 
Pasco, utu haupimwi kwa kumhurumia mgonjwa tuangalie pia upande wa pili anaowawakilisha, alipogundua kuwa anaumwa na hawezi kuwahudumia kwa nini hajiuzulu kupisha mwingine, ina maana yeye hawahurumii akina mama wajawazito pale Tengeru wanaosumbuka kupanda bajaji kwa kukosa mwakilishi bungeni?

mkuu umenena
 
Ugua pole Sumari

Pole Brother, nadhani hili jambo lahitaji sana maombi maana linakuwa kama la kifamilia maana mwaka juzi mdogo wake aitwaye Solomon alifariki kwa ugonjwa ufananao na huo. Ee Mungu msaidie, jamani pia apunguziwe majukumu sasa, serikali itisheni uchaguzi mdogo pls
 
Back
Top Bottom