Mbunge Selasini KUBURUZWA Mahakamani

Ya deus ilisukumwa na political si2ation,kama mnataka selasini apandishwe kortini ni lazima familia ya waliokufa watengeneze national dialogue juu ya ajali iyo...waseme kama mbunge alikusuadia kuua..ila hii thrid ipo ktk ushawishi wa magamba zaidi kumpa shida 30
 
Kila ajali ya gari ina uzembe. Mhadhiri wa usalama barabarani wa BP.
 
Sheria mara nyingi inawaumiza wanyonge wakubwa huwa wanapeta sana.Wewe kama mashtaka aliyoshitakiwa iddi simba si ungeoza jela.Mtu mpaka kawadhamini wenzake washukuru iddi wangerudi jela wale masikini wengine
 
Kama unayajua yote hayo kwa nini usiende mahakamani kufungua kesi.
ritz, Mahakama zipi mkuu? kama ni hizi ambazo maamuzi yanotolewa kwa maelekezo ya TIS na Mkulu itakuwa ndoto haki kutendeka.
 
Last edited by a moderator:
parameter, Ni Mimi Msiogope,
Iliwahi kusikika kuwa Dennis ni TIS, na alitumwa kuipunguza nguvu CHADEMA. Pia ilithibitika mahakamani kuwa Dennis hakuwa na leseni.

Tunazungumzia Deus Mallya na siyo Dennis.... Hata hivyo kama alitumwa na TIS kwanini hukwenda Mahakamani kutoa ushahidi?.. Acheni kuropoka vitu msivyovijua! Kunya anye kuku akinya bata kaharisha!
 
Kwani Gamba Chenge, aliyeendesha gari bila bima, akiwa amelewa chakari , akaua watu wawili alihukumiwa kwenda jela miaka mingapi?
 
Ndio maana mm nikasema inategemea taarifa ya polisi make waliokufa ni ndugu zake je ndugu zake watafungua kesi kumuhukum 30 ndugu yao? na pia tusisahau huyu ni Mbunge mwakilishi wa watu, je watu wake watakubali ateseke na wao wateseke ukizingatia alimwangusha jabali gamba mramba kweye ubunge pia sasa ni mremavu,so kuna mambo mengi ya kuitaji consideration?
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limesema litamfikisha mahakamani Mbunge wa Jimbo la Rombo, (Chadema), Joseph Selasini (50), kufuatia ajali ya gari alilokuwa akiendesha kusababisha vifo vya watu wanne.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani Mara, aliieleza hayo NIPASHE Jumamosi, kuhusu hatua zinazofuata baada ya ajali hiyo ambapo mbunge huyo alikuwa dereva wa gari hilo.

Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani, dereva anayesababisha ajali hufikishwa mbele ya chombo cha haki ambacho ni mahakama.

Alisema wanachosubiri ni michoro ya askari aliyepima ajali hiyo, kwani yapo mambo mengi kutokana na ajali hiyo iliyotokea katika barabara kuu ya Moshi Arusha baada ya gurudumu kupasuka.

“Polisi tuna maadili, tunasubiri apone kwani alikuwa mahututi na amefiwa na mama yake mzazi, mkwe na ndugu wengine huku mke wake akiwa bado yu mahututi hospitalini, tutapima ajali na tutachunguza...Sheria lazima ifuate mkondo wake na kesi dhidi yake ipo pale pale,” alisema Mwakyoma.

Aidha, alisema ajali hiyo inahitaji uchunguzi wa kina kwa kuwa inahusisha mambo mengi ikiwemo gurudumu moja kupasuka na kisha gari kwenda kuparamia kalavati, hivyo mara baada ya uchunguzi kukamilika sheria itafuata mkondo wake.
Ajali hiyo ilitokea Mei 24, mwaka huu, majira ya saa 1 usiku, katika eneo la Chuo cha Ufundi Bomang’ombe, barabara ya Moshi Arusha, wakati akitokea kwenye msiba wa padri mkoani Arusha, ambapo watu wawili walifariki papo hapo.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa ni mwendo kasi na kumkwepa mwendesha pikipiki. Gari lilikuwa likiendeshwa na mbunge huyo ni lenye namba za usajili T 441 BRT aina ya Toyota Land Cruiser VXR s/Wagon.

Katika gari hilo, kulikuwa na abiria sita, ambapo wawili walifariki eneo la tukio, mmoja hospitali ya wilaya ya Hai, na mwingine usiku baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge huyo, aliiomba Serikali kufanya ukaguzi wa kina wa bidhaa na vipuri vya magari vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi, kwa kuwa ni siku tatu zilizopita alinunua magurudumu ya gari hilo, ikiwa ni pamoja na elimu kwa waendesha bodaboda na baiskeli.

Hii ni ajali ya pili kwa mbunge huyo, baada ya ajali ya kwanza mwaka juzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo alivunjika mkono wa kulia mara tatu.



Sosi: ippmedia.com
 
askari wetu ni maffaa*** la kweli .. Badala ya kupiga vita ili serikali iache kuingiza bidhaa fake hasa kutokea kenya wanakuja na mashairi ya ajabu ajabu hapa..
Sishangai kuwa wengi wao wana vyeti fake.
 
Huyu mbunge anaonekana ni careless sana haiwezekani ukawa na ajali mbili mpigo, na inasemekana anaendesha kwa fujo sana haya magari ya mkopo.
 
askari wetu ni maffaa*** la kweli .. Badala ya kupiga vita ili serikali iache kuingiza bidhaa fake hasa kutokea kenya wanakuja na mashairi ya ajabu ajabu hapa..
Sishangai kuwa wengi wao wana vyeti fake.

Sasa askali wamekukosea nini hadi uwatusi? huyu jamaa hayuko makini, na polisi wamemstahi sana alitakiwa asomewe mashitaka akiwa kitandani hospitalini.
 
polisi na wenyewe watafuta pa kutokea ionekane wanafanya kazi..
 
Back
Top Bottom