Mbunge Selasini apata ajali mbaya! Akimbizwa hospitali, watatu wafa papo hapo akiwamo mamake

pole mbunge wangu ...lakini hivi kwanini mnapenda kuzurura bana..hivi hamna ipad muwe mnakaa mnasoma vitu na kuplot stratergies za kutatua matatizo ya wananchi ...aghhh

Duh we jamaa ni noumer sa hadi msibani angeshiriki kupitia ipad?
 
MUNGU WETU TUREHEMU SISI TU WAKOSAJI KILA SAA!

Wote walio majeruhi nawatakia kila la Kheri na wapone mapema waendelee na ujenzi wa Taifa.


Na wote waliofariki nasema walale kwa AMANI YAKE BWANA WETU!
 
Ee Mungu tunakuomba kwa ajili ya rehema kwa uliowaita kwako kupitia ajali hiyo, tunakuomba pia kwa ajili ya afya ya Mh. JS. Kwako wewe yote yawezekana. Amen.
 
maisha ndivyo yalivyo

mtu unapanga hiki na mungu nae anapanga lake juu yake na mala nyingi huwa ni siri hakuna ,alikwenda kumchukua baba aliyekuwa hospital amerudi na maiti ya mama aliyekuwa mzima

R.I.P MAMA YETU,NA WOTE

Mungu ampe nguvu Mh MBUNGE KTK WAKATI HUU MGUMU
 
Hivi kwanini sisi watanzania tunaona kufunga mkanda kama ni kuwafurahisha polisi tu?

Mkuu kuna jamaa yangu mtu bila abiria kufunga mkanda haendeshi gari lake!. Unajua mwenye dhamana ya kuhakikisha usalama wa abiria ni dereva, usiondoe gari mpaka wote wafunge mikanda, na uzuri wa magari ya siku hizi ni kwamba kama mtu hajafunga au akifungua unaona kwenye dashboard na alarm inafuatia. Kupanda gari bila kufunga mkanda ni sawa na kufanya mapenzi na stranger bila condom.

Tatizo la polisi wetu wao husisitiza haya kwenye wiki ya nenda kwa usalama baada ya hapo wiki 51 zote zinakuwa nenda kwa hatari huku polisi wakiwinda watu kupatia rushwa. I hope kama abiria wote wa Selasini wengekuwa wamefunga mkanda huenda kungekuwa na minimun casualities.
 
Kutokana na taarifa ya Mh. Makene Tumaini, ni kuwa Mh Selasini alikwenda hospitali kumtoa baba yake baada ya kuwa discharged na kama zilivyo desturi na taratibu zetu alikuwepo mke wa mgonjwa(Marehemu Mama yake Selasini) alikuwepo shangazi(marehemu dada wa mgonjwa) labda na jirani wa karibu rafiki wa Mama au wa Shangazi ambaye nae unfortunately ni marehemu - sasa swali ninalojiuliza ambalo linanifanya nichemke kwa hasira JE IPAD INGEWEZA KUWATOA HOSPITALI KAMA ALIVYOSUGGEST MCHAFUA HALI YA HEWA FULANI???

Mimi nafikiri kabla hatujaamua kuandika ***** basi tuhakikishe at least the few neurons we have are still connected(if ever been connected!!!!) and above all are collaborative otherwise stay away from the keyboard - it's for your own good!!!
 
pole mbunge wangu ...lakini hivi kwanini mnapenda kuzurura bana..hivi hamna ipad muwe mnakaa mnasoma vitu na kuplot stratergies za kutatua matatizo ya wananchi ...aghhh

Kwenda kumtoa baba yake hospitali ni kuzurura? Embu chunga kauli yako kabla hujaitoa au hujaisoma habari?
 
Pole sana Mh. Selasini na Mungu akuponye na akutie nguvu.
Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu wote katika ajali hiyo. Amina
 
pole mbunge wangu ...lakini hivi kwanini mnapenda kuzurura bana..hivi hamna ipad muwe mnakaa mnasoma vitu na kuplot stratergies za kutatua matatizo ya wananchi ...aghhh

alikuwa hazuri kaenda kumtoa baba yake hospitali kamanda
 
Pole sana m4c naamini Mungu atakuponya na utarudi ktk harakati za kuikomboa Tz. R I P kwa wote waliopoteza maisha Mungu awape pumziko la melele na mwanga wa milele uwaangazie amen.
 
Ee Mungu tunakuomba kwa ajili ya rehema kwa uliowaita kwako kupitia ajali hiyo, tunakuomba pia kwa ajili ya afya ya Mh. JS. Kwako wewe yote yawezekana. Amen.

Afya yangu iko murua kabisa ndugu Gobegobe.....:A S angel:......Amen

Pole sana Mhe. Selasini kwa ajali na kwa kupoteza sehemu ya familia yako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Invisible muda mfupi uliopita nimeongea na kamanda wa upelelezi wilaya ya Hai ameniambia Mheshimiwa yuko hospitali ya Wilaya hapo Hai ila mkewe amekimbizwa KCMC hali yake si nzuri ila pia si mbaya sana kwa mujibu wa huyo Kamanda. Kuna mawasiliano tunafanya tupate kujua hali ya mke wa mheshimiwa inaendeleaje huko KCMC
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom