Mbunge sadifa juma khamis (ccm): Nipo tayari kumpiga risasi baba yangu

Kap u ya amebaka
yule bibi vitu maalum kamuoa mjukuu wake,
EL fisadi wa kutupwa,
Mzee wa kucheka cheka anahonga mpaka ofisi za umma(ukuu wa
Wilaya/mikoa),
Pi n då wapigwe tuu amechoka, magufuli kutekeleza sheria anazuiwa,
badala ya kukamata majangili wanateka na kutesa wanavijiji tuuu, mapapa wanapeta,
madawa ya kulevya ni kama pipi tuu,
wanaomba pesa hadharani (bajeti) kukaguliwa matumizi yake kunafanyika gizani,
Huyu mjinga nae unadhani atasema nini? Waacheni watutukane si ndivyo tupendavyo???
Mijitu ina uwezo zaidi ya hawa imekaa tu haifanyi lolote!!!!!! Wacha wajinga watutawale
 
Fikra za ma ccm ni za kikoloni koloni,hawajui kujitawala wanatumia polisi kukandamiza raia
 
MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis (CCM), amesema yupo tayari kumpiga risasi baba yake iwapo atashiriki kwenye maandamano yasiyo na kibali cha polisi. Sadifa alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambapo alisema anaunga mkono polisi kutumia silaha za moto kwenye maandamano. Alisema anapinga michango iliyotolewa na baadhi ya wabunge wenzake ambao walitaka polisi wasiwe wanakwenda kwenye maandamano na silaha za moto. "Jamani mimi nipo tayari kumshoot (kumpiga risasi), baba yangu kama atakuwa amehudhuria maandamano yaliyokataliwa na polisi, nimepitia jeshini, najua ufanyaji kazi wa polisi. "Ni lazima polisi apewe silaha za moto kwenye maandamano maana wengine hapa wanayafanya bila kibali, kama mnataka polisi wasiwapige risasi basi fuateni taratibu za kufanya maandamano," alisema. Awali kabla ya Sadifa kuchangia hotuba hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu, Naomi Kaihula (CHADEMA), alilitaka jeshi hilo kutokwenda na silaha za moto kwenye maandamano mbalimbali. Alisema hivi sasa limekuwa jambo la kawaida kwa askari polisi kwenda katika maandamano wakiwa na silaha za moto ambazo wakati mwingine wamekuwa wakizitumia, jambo linalosababisha vifo na majeruhi kwa waliohudhuria. Kaihula alibainisha kuwa polisi wanapaswa kutambua wajibu na dhamana yao kwa Watanzania kwa kutoegemea upande wa chama chochote katika utendaji wao. "Hali ya sasa inaonyesha matumizi ya nguvu ya polisi ni makubwa, polisi wanaogopwa wanapokamata hata kibaka wanatumia silaha kali za moto, lakini pia kuna tatizo la polisi kujihusisha na siasa, vitu hivi viwili vinapaswa vitengane kwani ni tishio kwa usalama wa nchi," alisema Kaihula. Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao (CHADEMA), aliwatahadharisha polisi kuwa kamwe wasitegemee CCM itaendelea kukaa madarakani milele, kwani ipo siku chama hicho kitang'oka, hivyo ni vema wao wakafanya kazi zao bila upendeleo. Alisema watawala wa kibaguzi nchini Afrika Kusini walikuwa wakivitumia vyombo vya dola kuwaua wandamanaji na wale waliokuwa wakiupinga utawala huo lakini ulipofika mwisho waling'oka madarakani. SOURCE: TANZANIA DAIMA TAREHE: TAREHE 19 JULY, 2012.

Hawa ni wateule wa Mhe Rais Kikwete Mhe Sadif na Mhe Mwigulu, hawatofautiani sanaa kiitikadi ni watu wenye itikadi ya zidumu fikra za mwenyekiti na wako tayari kufanya lolote chini ya mwavuli wa uzalendo.. Bahati mbaya tafsiri ya neno uzalendo, ni yeyote ambaye anaipinga au kutokubaliana na serikali au CCM si mzalendooo.. analosahau maisha ni dynamic na lolote linawezaa tokea hata waliopo CCM hutoke wakapingana na CCM na maaandamano ni haki inayolindwa na katiba ya jamhuri ya muuungano... polisi wapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao... sasa hayoooo ya kushooot yanatokea wapiiiiii....
 
Back
Top Bottom