MBUNGE: POLISI wameshaninyang'anya JIMBO langu...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mbunge wa Morogoro Mjini-CCM,Aziz Abood amekaririwa akisema kuwa vitendo vinavyoendelea kufanywa na Polisi Jimboni mwake,kurindimisha mabomu ya machozi na risasi ni kumpora Jimbo lake.

Taarifa toka kwa Msaidizi wa Mbunge huyo zinadai kuwa vitendo hivyo vya Polisi vinajenga chuki baina ya wananchi na Serikali yao hivyo kuweka jimbo hilo na CCM kwa ujumla mashakani. Ameapa kulalamika kwenye vikao vya Chama. Mwenye maji ampunguzie mwenzie...ngoma inogile!
 
Hiyo danganya toto, inawezekana Abood alijua kabisa kuwa polisi watafanya hujuma hii
 
Mbunge wa Morogoro Mjini-CCM,Aziz Abood amekaririwa akisema kuwa vitendo vinavyoendelea kufanywa na Polisi Jimboni mwake,kurindimisha mabomu ya machozi na risasi ni kumpora Jimbo lake. Taarifa toka kwa Msaidiz4 wa Mbunge huyo zinadai kuwa vitendo hivyo vya Polisi vinajenga chuki baina ya wananchi na Serikali yao hivyo kuweka jimbo hilo na CCM kwa ujumla mashakani. Ameapa kulalamika kwenye vikao vya Chama. Mwenye maji ampunguzie mwenzie...ngoma inogile!

Aliwatuma yeye sasa analalamika nini> POLICCM
 
Hiyo danganya toto, inawezekana Abood alijua kabisa kuwa polisi watafanya hujuma hii


Nakubaliana na wewe, na tangu mwanzo niliamini kuwa huyu Mbunge allikuwa nyuma za 'nguvu' inayotumiwa na polisi. Mambo yameharibika sasa anaanza kujikosha ili aonekane anajali walalahoi. Abood anamaliza watu na mabasi yake sasa anajificha nyuma ya polisi. Haikubaliki.
 
Huyu kwanza si yule aliyekuwa na kashfa ya kuzika wahanga wa ajali la basi lake la ABOOD pale MDAULA kuficha kashfa ya mabasi yake ya ajali dhidi ya mshindani wake HOOD.Atulie
 
Mbunge yuko sahihi. Kila siku serikali inawasaidia Chadema kupata wanachama kurokana na presha zao. Hivi ikiwa watu wanaandama barabarani huku hawana silaha yoyote isipokuwa mabango na wengine wamebeba magazeti kama marehemu comredi Ally alivokutwa, kwa nini kuwazuia hadi kwa kufyatua bunduki.
Kama wangewasaidia ili waandamane vizuri ingekuwa na hasara gani kwao?
Hivi kwa kufyatua bunduki na kuua raia kumewasaidia nini zaidi ya kujenga chuki kwa wapiga kura wa mheshimiwa Abood?.

Ama kweli ukizeeka sana huogopi chochote zaidi ya kifo na kwa bahati mbaya nacho hakikwepeki.
 
Asitafute sababu za kujinawisha mikono. Kama Jimbo kuporwa, lilishaporwa kitambo. Akilaumu chama na serikali kwa ujumla wake.
 
Naona naye ni miongoni mwa walio amuru polisi itumie nguvu, unafiki tu naona unamsumbua.
 
ha ha ha (Vuta Nikuvute hili la mwenye maji ampunguzie mwenzie nalo ni neno). CCM vichwa ngumu sana, yaani siasa uchwara walizomfanyia Mrema mwaka 1995 ndio wanazitekeleza leo 2012? Kweli mkojo wa alfajiri hauzuiliki.
 
Mnamo 2015 CCM kubaki na viti vya ubunge SI ZAIDI YA 78 tu na viti vya ubunge kote nchini.

Nako mkoa wa Morogoro ndio kama hivo CCM kimeamua kuviuza kimoja kwa thamani ya damu ya ALLY hata kabla hajamaliza mfungo wake ule wa siku 6 za ziada zile.

Bai bai CCM kwa mtaji wa unyama kma huu dhidi ya raia wasiokua na hatia.
 
Anazuga tu. Yeye ndie alietoa posho ya askari kulinda maandamano siku zile. Hana lolote anaogopa kesi ya kuua huyo.
 
CCM ina hati miliki na nchi,polisi,na rasililimali
wana uwezo wa kuangamiza chochote kitakachojaribu kuwanyanganya hati miliki yao.
wameshajua kuwa wananchi wako mbioni kuwanyanganya ndio maana wanatumia nguvu badala ya sera na hoja.
 
Back
Top Bottom