Mbunge na madiwani wameiba madawati

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika hali isiyo ya kawaida (Kwa taarifa ya habari ya TBC 1), mbunge aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mathayo Manyinyi, amemtuhumu mbunge wa Musoma mjini kwa tiketi ya CHADEMA Vincent Nyerere pamoja na madiwani kwa kumwibia madawati.Mathayo amesema atawafikisha watuhumiwa mahakamani kwa kumwibia mbunge huyo mstaafu madawati ambayo ni mali ya familia yake.

Binafsi nimeshindwa kuelewa vema sakata hilo. Naomba mwenye taarifa kamili atujuze. Yawezekana pia ikawa ni hasira za kushindwa katika uchaguzi!
 
Ana familia kubwa kiasi gani mpaka amiliki madawati yake mwenyewe? Au ni yale yale ya Mtera ukishindwa unakusanya hata vile ulivyotoa huko nyuma?
 
Aisee hii kali ya mwaka. Hayo madawati ni mangapi na anafamilia kubwa kiasi gani mpaka atengeneze madawati badala ya makochi na viti?
Siasa za maji taka zitatuponza sana!
 
Hii ni kali kwa kweli..
hebu mliopo kwenye maeneo mtujuze zaidi madai ya huyo ndugu aliyeshindwa ubunge akaamua kudai kuibiwa madawati
 
Yani Takataka Broadcasting Chamber wamekosa habari za kureport ama kweli tutaona vioja vingi sana mpaka 2015
 
Katika hali isiyo ya kawaida (Kwa taarifa ya habari ya TBC 1), mbunge aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mathayo Manyinyi, amemtuhumu mbunge wa Musoma mjini kwa tiketi ya CHADEMA Vincent Nyerere pamoja na madiwani kwa kumwibia madawati.Mathayo amesema atawafikisha watuhumiwa mahakamani kwa kumwibia mbunge huyo mstaafu madawati ambayo ni mali ya familia yake.

Binafsi nimeshindwa kuelewa vema sakata hilo. Naomba mwenye taarifa kamili atujuze. Yawezekana pia ikawa ni hasira za kushindwa katika uchaguzi!
pole sana kwa kuibiwa madawati yako pambana mpaka ushinde kesi
 
Huyu sasa naona ashakuwa mwehu.... madawati ya familia?? Yaani ndio walikuwa wanayatumia kama viti au ndo style zile za chama cha magamba za kuondoka kwenye ofisi za wabunge na furniture??
 
Katika hali isiyo ya kawaida (Kwa taarifa ya habari ya TBC 1), mbunge aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mathayo Manyinyi, amemtuhumu mbunge wa Musoma mjini kwa tiketi ya CHADEMA Vincent Nyerere pamoja na madiwani kwa kumwibia madawati.Mathayo amesema atawafikisha watuhumiwa mahakamani kwa kumwibia mbunge huyo mstaafu madawati ambayo ni mali ya familia yake.

Binafsi nimeshindwa kuelewa vema sakata hilo. Naomba mwenye taarifa kamili atujuze. Yawezekana pia ikawa ni hasira za kushindwa katika uchaguzi!

Wale wale,
 
Daah..., jamani siasa za Bongo kwa vituko ni noma,sasa hayo madawati ni ya kukalia nyumbani kwake au..?
 
Huyu sasa naona ashakuwa mwehu.... madawati ya familia?? Yaani ndio walikuwa wanayatumia kama viti au ndo style zile za chama cha magamba za kuondoka kwenye ofisi za wabunge na furniture??
Mkuu kwani kuwa na madawati mengi ndio mwehu? yeye anataka madawati yake msitake kujua ya kazi gani, Mbunge na Diwani wake wafanye haraka kumlipa jamaa madawati yake, kabla kesi aijawa kubwa
 
Mbunge wa zamani (CCM) ametengeneza madawati kwa ajili ya shule ya Mkendo iliyopo mjini Musoma. Alichelewa kuyakabidhi katika kipindi chake na sasa amekosa ubunge. Alipanga kuyakabidhi lakini akawa na shughuli nyingine, hivyo yalibaki yamefungiwa stoo. Madiwani (wa CDM) baada ya kuona msaada unachelewa, wakavunja stoo na kuyakabidhi shule kabla mmiliki hajayakabidhi. Tayari wamefikishwa mahakamani kwa kuvunja na kuiba... nimesikia mwanasheria wa halmashauri amekataa kuwatetea kwa sababu aliwashauri wasubiri mwenyewe ayakabidhi lakini hawakumjali(hili sina hakika ni pipo sei)
 
Mkuu kwani kuwa na madawati mengi ndio mwehu? yeye anataka madawati yake msitake kujua ya kazi gani, Mbunge na Diwani wake wafanye haraka kumlipa jamaa madawati yake, kabla kesi aijawa kubwa

sasa kwa nini aibe mbunge na diwani wala hajasema wenje ndo kaiba? Au siku izi vyeo vya kisiasa vinaiba? Au ndo uendawazimu umetimuliwa ofsini unataka na mali kama Masha? Mwizi anatangazwa mkutanöni au anapelekwa mahakamani? Je ana Report ya polisi?je amejuaje Wenje ni mwizi bila ya kuamliwa na mahakama? Kama ugali unakula na juice waweza tengeneza pombe na ukalewa kwa kuwa hapo kuna glucose na oxygen pamoja na unga. Uyo mgombea mkataliwa kalewa ugali!
 
Katika hali isiyo ya kawaida (Kwa taarifa ya habari ya TBC 1), mbunge aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mathayo Manyinyi, amemtuhumu mbunge wa Musoma mjini kwa tiketi ya CHADEMA Vincent Nyerere pamoja na madiwani kwa kumwibia madawati.Mathayo amesema atawafikisha watuhumiwa mahakamani kwa kumwibia mbunge huyo mstaafu madawati ambayo ni mali ya familia yake.

Binafsi nimeshindwa kuelewa vema sakata hilo. Naomba mwenye taarifa kamili atujuze. Yawezekana pia ikawa ni hasira za kushindwa katika uchaguzi!
Nafikiri kilikuwa kipindi cha VIOJA MAHAKAMANI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom