Mbunge Mussa Khamis Silima afariki Dunia

Bunge lime hailishwa baada ya mmoja wao kuaaga dunia kutokana na ajari iliyo tokea jana .R.I.P. MP wetu!!!!
 
Shughuli za bunge zimeahirishwa, baada ya spika kuwatangazia wabunge kuwa Mbunge Silima amefariki dunia katika hospitali ya muhimbili, alikokuwa amelazwa kutokana na ajali mbaya ya barabarani aliyopata jana asubuhi, ambapo mke wake mwanaheri alifariki dunia palepale. R.I.P. Musa Silima
 
Yule Mbunge aliyefiwa na mkewe juzi na yeye akaletwa Muhimbili...Na yeye amefariki leo hii" Spika Anne Makinda".
 
Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda, ametangaza muda huu kuwa Mh. Mbunge Silima aliyepata ajali mbaya ya gari juzi na kumpoteza mkewe. Amefariki muda mfupi pale Muhimbili. Bunge limeahirishwa mpaka kesho kwa maombolezo. Poleni wanafamili wote na Bunge zima kwa ujumla wake.
 
Na spika wabunge la jamuhuri Anne Makinda ameliahirisha bunge hadi kesho kutokana na kifo hicho!
 
Ni wajimbo gani huyu Jamani? RIP Mh!
RIP Silima

Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi (CCM), Maalim Mussa Silima, amepata ajali na mkewe, Mwanaheri Alli, amefariki dunia baada ya gari walilokuwa wamepanda kugongana na gari ya mizigo eneo la Nzuguni mkoani Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Uzini, Muhammed Seif Khatib, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:00 jioni na marehemu alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Alisema Mbunge huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam akiwa amefuatana na mkewe akiwahi kikao cha Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa kifanyike jana pamoja na kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano.

"Marehemu anatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja," alisema Khatib na kuongeza kuwa Mwakilishi huyo alisafirishwa kwa ndege kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Kitengo cha Mifupa (MOI).

Alisema baada ya kutibiwa katika Hospitali ya Dodoma, madaktari walishauri ahamishiwe MNH kutokana na maumivu aliyoyapata sehemu ya uti wa mgongo na paja.

Alisema gari ya mbunge huyo ilikuwa ikiendeshwa na dereva wake, Chizani Sembonga, alipokuwa akijaribu kuikwepa gari iliyokuwa mbele yake alikutana na gari lingine na kugongana nalo.

"Ujumbe wa wabunge tisa umeteuliwa kuwakilisha Bunge katika mazishi wakiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Dole, Juma Nhunga," alisema Khatib. Mwakilishi huyo alichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa mara ya kwanza baada ya kumuangusha katika kura za maoni aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee.
 
Kwa kweli hili ni pigo kwa wanafamilia, watu wawili kufa katika kipindi kifupi. Poleni sana wafiwa na mungu awarehemu waja wake.

Nadhani huyu Mh Silima ni ndugu wa Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima. very sad.
 
RIP mheshimiwa, nilidhani ni wa huku bara nianze kushangilia jimbo lingine kuwa wazi kwa chadema.
 
Back
Top Bottom