Mbunge Lucy Mayenga apata ajali!

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Mbunge wa CCM kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana, Lucy Mayenga, amepata ajali ya gari usiku wa kumkia leo na kunusurika kifo. Kwa mujibu wa mtoa habari wetu Lucy alipata ajali hiyo akiwa safarini kwenda Dodoma katika eneo la Chalinze, kilomita 40 kabla ya kufika Dodoma mjini. Habari zaidi zinapasha kuwa Lucy ndiye aliyekuwa akiendesha hiyo gari Toyota Landcruiser VX yenye namba T 681 BCV, alipatwa na majereha kiasi na hali yake inaelezwa kuwa siyo mbaya, ingawa anatarajia kwenda hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

1312.jpg


pole dada yetu
 
pole sister,

lakini, hivi hawa wa viti maalum ni wabunge kweli? manake qualifikesheni yao kubwa ni mashine whether used or brand new!

kweli ccm wanafanya madudu!
 
KUna haja ya kufanya utafiti wa kina kujua kuna nini kati ya Gairo (kuanzia maeneo ya Pandambili) had Dodoma kuna nini hasa kinachosababisha ajali mara kwa mara katika maeneo hayo
 
.....Habari zaidi zinapasha kuwa Lucy ndiye aliyekuwa akiendesha hiyo gari Toyota Landcruiser VX yenye namba T 681 BCV.......!
Acheni ubahiri, tunavibaka wengi sana mtaani ambao wanaweza kuwa madereva wazuri tu......toeni ajira kwa vijana!

Anyway.....pole sana!
 
Acheni ubahiri, tunavibaka wengi sana mtaani ambao wanaweza kuwa madereva wazuri tu......toeni ajira kwa vijana!

Anyway.....pole sana!

hana uhakika na ulaji ndani ya jumba lile linalotema fedha.

halafu wewe, vibaka wale wakimbaka je? totz yenyewe si unaona inavyoita?
 
Hivi jamani mahela yote hayo na maposho bwelelee hata kuajiri dereva nayo ishu

any way augue pole
 
Kanusurika na utabiri wa Sheik Yahya!!!

H ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha acheni vituko jamani eheeeeeeee
 
Back
Top Bottom