Mbunge Kigwangalla Afunga Mgodi wa Isungangwanda kwa Nguvu ya Umma!

Nahisi kama Kigwangalla angekuwa CDM hapa angeoneka shujaa... tuacheni cheap politics tuunge mkono linalostahili kuungwa na tuponde lisilostahili. Mikataba ni mikataba, iwe mikubwa au midogo kuivunja inagharama zake. Kwani hatujajifunza mambo ya kukurupuka kwa Dowans?

Tanzania kwanza...
 
WanaJF nimeikuta hii kule Wanabidii,
Naona Mbunge Kigwangalla sasa ameanza kufanya kweli, Resolute nao wakae sawa sasa!

Wananchi wa Kijiji cha Mwabangu ambao wamedhulumiwa haki ya kumiliki mgodi wao maarufu kama 'Isunga Ngwanda' waliokuwa wakiumiliki toka Mwaka 1987 na kila mara wakikata na kulipia leseni mpya. Mkataba wa kwanza ulikuwa baina ya Mmbando and Partners na Kijiji cha Kilabili/Mwabangu, ambao walikiuka masharti na kuacha kulipia ushuru wa kijiji na kijiji kikaamua kuuvunja mkataba huo. Watu hao walijipanga upya na kuamua kwa njia za hila kwenda kubadilisha jina la kampuni na kuchukua leseni yao (PML) kwenye kitalu kile kile kwa njia ya ulaghai na kujiita jina jipya la Rebman Damson Tarimo and partners na kuja kuanzisha mgodi wao na kuwafukuza wachimbaji wadogo wadogo na baadaye kuanza kuwachaji wanakijiji ushuru wa kuingia kuchimba

Mkuu wa Wilaya mwezi wa kwanza aliamua kusitisha uchimbaji katika eneo hili mpaka ufumbuzi utakapopatikana, wananchi walitii agizo hili lakini Rebman na wenzake waliendeleza uchimbaji, hali iliyofanya wanakijiji kukasirika na sasa kuamua kuweka ulinzi wao na kuwaondoa wawekezaji hao

Mbunge wa Nzega Dkt. Kigwangalla, akiambatana na diwani wa kata ya Nata Mhe. Joseph Malongo wameungana na wananchi kwenye eneo hili la mgodi ili kuzuia dhulma hii kwa nguvu za umma!

Wananchi zaidi ya 1500 wamekusanyika hapa na mpaka sasa hivi wameshafanikisha kuzuia uchimbaji kwenye maduara yote matatu!

Ingawa ni kimgodi kidogo cha wawekezaji wa ndani amefanya vizuri. Sasa hatua inayofuata awafuate Resolute ili awawajibishe.
 
Acheni ushabiki wa hivyo hovyo,
Wakati wa hotuba yake alisema atafunga RESOLUTE na sio hao wachimbaji wadogowadogo sie tulikuwepo uwanja wa Parking Nzega na tunafahamu yaliyomkuta na mpaka sasa hajarudi paking kuhutubia ........
 
Ndugu zangu wanaJF,

Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana.

Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!

Mgodi ulioahidi kuufunga ni RESOLUTE. Ulijaribu kuhamasisha wananchi kwenda kuvamia resolute ukaishia kupata aibu.

Kama unajiamini, nenda kafunge mgodi wa resolute uone cha mtema kuni!
 
Mgodi ulioahidi kuufunga ni RESOLUTE. Ulijaribu kuhamasisha wananchi kwenda kuvamia resolute ukaishia kupata aibu.

Kama unajiamini, nenda kafunge mgodi wa resolute uone cha mtema kuni!

Angekuwa Zitto amefunga mgodi ungeongea hivyo? Tuache unafiki huu na tuanze kujifunza kuongea ukweli kwa manufaa ya taifa. Mambo ya kukatisha tamaa viongozi wetu yalishapitwa na wakati ila toa pongezi inapobidi kutoa.
 
Hii safi. Aungwe mkono Sio kubezwa. Tabia za kubeza ndizo hukatisha tamaa viongozi jasiri na kusababisha warudi nyuma.

Mwalimu Kitila,
Kigwangala haitaji kupewa pongezi katika hili.
Aliahidi kwamba akichaguliwa ataufunga mgodi wa resolute. Wananchi wakamchagua sasa ni zamu yake kutekeleza ahadi yake. Haka kamgodi ambako hata kwa ngeleja hakajulikani hawezi kujisifia hata kidogo!

Aliwahi kujaribu kukusanya wananchi kwenda kuufunga huo mgodi wa resolute akaishia kupata aibu. Baada ya muda tukasikia amewapigia magoti. Hapa amekiri kwamba wako mezani kwa mazungumzo. Hadi hapo ni dhahiri kwamba hoja yake imeshindwa na uzingatie kwamba yuko ccm ambacho kinawakumbatia hao waporaji wa rasilimali za nchi.

Ukiwapa mtihani wanafunzi wako na ikatokea mmoja amepata 20% utampa excellent?
 
Angekuwa Zitto amefunga mgodi ungeongea hivyo? Tuache unafiki huu na tuanze kujifunza kuongea ukweli kwa manufaa ya taifa. Mambo ya kukatisha tamaa viongozi wetu yalishapitwa na wakati ila toa pongezi inapobidi kutoa.

Usikurupuke wewe, kama ni unafiki wewe ndio namba moja!

Kigwangala anajikatisha tamaa yeye mwenyewe na mimi sihitaji kumpa sifa za kijinga. Kama unataka kujua ninasemaje kuhusu zito anzisha thread, ama pitia thread zinazomhusu zito, manake we wa jana hujui wengine tuko hapa kitambo na misimamo yetu iko wazi kwa viongozi wanafiki na wabinafsi kama huyu kigwangala.
 
safi sana Mh uliyasema haya humu humu Jf baada ya mimi kuileta ile mada ya kuufunga mgodi huo na sasa umefanya kweli,nadhani ni wakati wa kukupongeza na kukuunga mkono,kwani ni wabunge wachache sana wanaotekeleza kile wakisemacho kwa vitendo

tuzidi kumuunga mkono Mh ili na wengine wafuate mkondo huo hususani ktk yale maeneo ambayo wananchi wamezurumiwa mali zao na mafisadi wenye pesa,

kaza buti MH mda ndio huu na tambuwa kuwa kupanga ni kuchagua

si kila mtu atakuunga mkono lakini hiyo ni tabia za watu zilivyo hubeza kilajambo ila hilo lisikukatishe tamaa,mapambano daima
 
Ndugu zangu wanaJF,

Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana.

Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!

Usikate tamaa Mh,ni mpaka kieleweke tumezurumiwa sana,tumeteswa sana na tumenyonywa sana sasa huu ni wakati wa mabadiliko,chochote kile kinachowezekana wewe fanya ilimradi tu kanuni,sheria na taratibu zifuatwe

Timiza ahadi zako wakati ndio huu,vijana tuliowengi tunamatumaini na wabunge vijana kama nyie,hakika usirudi nyuma

Lakini pia nikushukuru kwa kutambuwa kuwa mwananchi akichoka hakuna awezae mzuia hata uje na jeshi la moto,basi kwa kutambuwa hilo fanyeni yaliyomema ilikuepusha kuwachosha wananchi

mapambano daima,tambua kuwa hutoweza kumridhisha kila mtu ktk hii dunia hususani ktk hili hapa jf utapata maoni ya kila aina cha muhimu ni wewe kufanya kile kitakachowaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla
 
Usikurupuke wewe, kama ni unafiki wewe ndio namba moja!

Kigwangala anajikatisha tamaa yeye mwenyewe na mimi sihitaji kumpa sifa za kijinga. Kama unataka kujua ninasemaje kuhusu zito anzisha thread, ama pitia thread zinazomhusu zito, manake we wa jana hujui wengine tuko hapa kitambo na misimamo yetu iko wazi kwa viongozi wanafiki na wabinafsi kama huyu kigwangala.

Hizi siasa za kiafrika mbaya sana. Kufikiri kwamba kitu kizuri ni kile kilichofanywa na upinzani tu.
 
Back
Top Bottom