Mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU) ataka TRA wamtoze kodi RICK ROSS show ya leo...

Au siyo mkuu? Maharage kwa mahindi wapi kwa wapi? Sugu atuonyeshe alipolipa "kodi kwa taifa letu" kutokana na show zake za Bongo, achilia mbali zile anazodai kufanya Marekani.

S.6(2)ya income tax act 2004..... Non resident anatakiwa akatwe 15% ya kipato chake.
 
Kweli wabunge wengine bwana, eti Sugu khaaaaa! Hivi wanambeya hamkuona watu wooooooote mkaamua Sugu awe mbunge wenu! Wanamwita suguuuu, nani, wanamwita Suguuuuu, waaanamwita Suguu sugu sugu sugu.

Mkuu nadhani wale waliomchagua ''Prof'' wa tunguri Maji Marefu ndo walifanya uamuzi wa busara.
 
Utamtambua mtu kwa maandishi yake!

Kweli wabunge wengine bwana, eti Sugu khaaaaa! Hivi wanambeya hamkuona watu wooooooote mkaamua Sugu awe mbunge wenu! Wanamwita suguuuu, nani, wanamwita Suguuuuu, waaanamwita Suguu sugu sugu sugu.
 
JF wapumbavu tumeanza kuwa wengi. Kwenye hli jukwaa huwa tunajadili issues na sio watu. Hapa la muhimu ni kujadili alichokiongea Sugu. Sasa wengi humu tunazidi kujadili mtu badala ya hoja.
Kuna tangazo la Guinness huwa linasema ''THERE'S A DROP OF GREATNESS IN EVERY MAN''

Nadhani tuanzie hapo na tukumbuke kuwa kila kitu uwa kina mwanzo. na ndo maana wakina Zitto wanakazania hata kazi za wasanii wetu zisambazwe na Posta na ziwekwe sticker za TRA ili mapato ya kodi yapatikane. Sasa mtu akija kulalamika eti kwa nini hawakuanza enzi za wakina Complex na uswahilini matola ntaona kuwa mtizamo wake ni wa kuzimu
 
Sugu ni waziri kivuli wa michezo na burudani..ulitakaje mkuu???wewe ulishaskia Magufuli anazunguzia elimu??yeye ni mabarabara tu kila siku!!umeona eeh!!....yani jinsi ulivyo kitunguu wewe unamjadili Sugu badala ya kujadili alichokisema Sugu.

naunga mkono hoja mkuuuuu
 
mr 2 anataka kujifananisha na rick ross. wakati anafahamu kabisa tofauti iliyopo kati ya concert zake yeye za kwenye vi pub marekani na hela yenyewe inaishia mfukuno na kwenda kununua used car . na rick ross. tena mwenzake serikali inamtambua na inamlinda akija hapa hadi ubalozi wake unapata taarifa. na ana bima . mr 2 acha wivu na chuki kwa clouds waliomleta .
Wewe kweli ni kupe mnyonyaji, hata maandishi yako yameakaa kikupe kupe usije kuwa ndo kibonde wewe
 
Namuunga mkono Sugu. Dah! Inawezekana TRA huwa inajisahau, eh?

Inawezekana hata wakina Chameleone huwa wanajichotea tu pesa za show hapa Tz bila tax
 
sugu hana lolote zaidi ya chuki binafsi tu! na clouds tu!... FIESTA imeanza lini..?! kuna kipindi pia alikuwa anapiga promo za FIESTA na wasanii wa nje walikuwa wakija.. kwanini kipindi kile asiongelee haya mambo anaongelea sasa..sugu ni looser flani mwenye roho ya kwanini hataki maendeleo ya wenzake! ...
wenzake gani hao ambao hatak maendeleo yao, sisi tuataka maendeleo ya taifa? Usifikirie kama njiwa ur a human being
 
Sugu big up kwa kuliona hilo mkuu wamezoea kuja kujichotea mihela na kusepa Nazi fanyakazi yako mkuu .
 
naona uelewa wawengi JF unanitatiza hata kama sungu hawezi jifananisha na Rick Ross lakini eleweni kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake yeye kama msanii wa kimataifa inabidi alipe kama kodi na wala sio kuupuzia huu wito wa Mheshimiwa Sungu
 
Kweli wabunge wengine bwana, eti Sugu khaaaaa! Hivi wanambeya hamkuona watu wooooooote mkaamua Sugu awe mbunge wenu! Wanamwita suguuuu, nani, wanamwita Suguuuuu, waaanamwita Suguu sugu sugu sugu.


hapa ni sawa na umeaandika jina kwa kinyesi.
 
vilaza kama nyie mnapaswa muelimishwe kuhusu entertainment business...taifa linapoteza mapato mengi sana sababu ya watu wanaochukulia poa hii bizness kama wewe.

Mkuu TRA wanawakamata wauza maji mitaani kwenye ma boza na kuwapandia sijui kodi gani lakini leo huo sijui Rose anapeta ? Hii ni Nchi ya ajabu sana maana walisema kila Petrol station iwe na risiti za TRA hakika sioni kama kuna kitu kama hicho nashangaa tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Sugu achana na Ross, vinega wapo wapi? Tunataka show bana.......anti-virus imekuwa outdated
......nasikitika kuona we mpaka sasa bado unashindwa kujitambua, show ni kitu gani bwana zaidi ya pato la taifa: Sugu ametukumbuka tunaka kuona kiasi atakacho katwa Rick Ross kama Kodi kwa kufanya biashara/kazi nchini.
 
Hapa ni sawa na ku-compare maembe na machungwa. Tanzania siyo Marekani. Halafu usishangae Rick Ross keshalipwa in full mshiko wake kabla hajatia mguu Bongo kupitia transactions za benki za Marekani.

Isitoshe bila shaka Rick Ross atalipa kodi ya mapato ya Marekani kutokana na hii concert, jee Sugu alishawahi kulipa "kodi ya taifa letu" baada ya kufanya show Marekani?

Hata office ikiajiri mtaalama mshauri (Consultant) kutoka nje lazima akatwe KODI kwani ndiyo utaratibu huo ndiyo maana wengi huwa wanafuatilia Kiasi cha Kodi hiku ndiyo wanaweka Bei zao ili wasipate hasara. Kiseheria ROSS anatakiwa kulipa KODI kwa KIPATO alichopata kwenye nchi yetu ni jambo la kawaida kabisaa na SHERIA inasema hivyo wala hakuna haja ya USHABIKI hapa.
 
Hapa ni sawa na ku-compare maembe na machungwa. Tanzania siyo Marekani. Halafu usishangae Rick Ross keshalipwa in full mshiko wake kabla hajatia mguu Bongo kupitia transactions za benki za Marekani.

Isitoshe bila shaka Rick Ross atalipa kodi ya mapato ya Marekani kutokana na hii concert, jee Sugu alishawahi kulipa "kodi ya taifa letu" baada ya kufanya show Marekani?

Ni kweli kabisa nkuu, namipia najiuliza maswali zaidi, msanii wa kibongo anapopiga show yake kenya au uganda au hata hapa TZ akilipwa anatozwa kodi? Hiyo mosi, pili nina uhakika Sugu anatakiwa atumie nafasi yake kikatiba kukomalia hii, na skuandika tu kwenye wall yake ya Facebook na kukaa kimya, hii ni sawasawa na kutupotezea muda wetu tu!
 
Rick Ross ni nani asilipe kodi hata awe juu ya sheria ya nchi yetu? Ikiwa hatalipa basi ni udhaifu kwa serikali iliyopo au chama tawala kimechukua cha juu ili jamaa asilipe kodi ya mapato kwa serikali. Ninyi mnaotetea asilipe ni wazi kuwa mmelisaliti Taifa hata kukosa uzalendo na kujali maslahi binafsi zaidi.
 
Hivyo sugu ni ni chuki binafsi na kutolipa kodi ni upendo wa kitaifa amah?!!!!!!!!!!!






sugu hana lolote zaidi ya chuki binafsi tu! na clouds tu!... FIESTA imeanza lini..?! kuna kipindi pia alikuwa anapiga promo za FIESTA na wasanii wa nje walikuwa wakija.. kwanini kipindi kile asiongelee haya mambo anaongelea sasa..

sugu ni looser flani mwenye roho ya kwanini hataki maendeleo ya wenzake! ...
 
Back
Top Bottom