Mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU) ataka TRA wamtoze kodi RICK ROSS show ya leo...

Hawezi kukatwa kodi huyo, Mbona wawekezaji kibao migodini,kwenye mahoteli i.e Sheraton-Royal Palm-Kempisk ,,TRA hawawachaji? Riki Rosi nae ni mwekezaji tayari utamaduni wetu ni wa kuogopa hawa wawe......zaji
 
KATIBA MPYA IGUSIE SWALA HILI. Ukitaka uwe muelewa penda kusikiliza hoja na sio kuangalia ni nani aliyesema hiyo HOJA.
 
Kwani yeye sugu si mbunge , why asingepeleke bungeni silo suala tena ki oficial na si facebook.
 
mr 2 anataka kujifananisha na rick ross. wakati anafahamu kabisa tofauti iliyopo kati ya concert zake yeye za kwenye vi pub marekani na hela yenyewe inaishia mfukuno na kwenda kununua used car . na rick ross. tena mwenzake serikali inamtambua na inamlinda akija hapa hadi ubalozi wake unapata taarifa. na ana bima . mr 2 acha wivu na chuki kwa clouds waliomleta .

mabwege yapo mengi sana nchi hii
 
MWANAMUZIKI nguli wa Hip hop Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi amewapa mwongozo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu ziara ya mwanamuziki nyota wa Hip hop Marekani, William Leonard Roberts II anayetambulika kama Rick Ross au The Boss, kwamba anastahili kulipa kodi kutokana na pato atakalaolingiza katika shoo yake ya leo.
Rick Ross atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo linaandaliwa na Prime Time Promotions nakudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Mbunge Mbilinyi ambaye anajulikana kwa majina ya kimuziki kama Mr II au Sugu, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook;
"RICKY ROSS ANAKUJA, SAWA HAINA SHIDA, ILA TUNATAKA KUJUA AMELIPWA KIASI GANI NA ATAKATWA KIASI GANI KIBAKI KWENYE KODI YA TAIFA LETU KAMA AMBAVYO MIMI NIKIENDA KUFANYA SHOW/CONCERT MAREKANI NAKATWA KODI NA SERIKALI YAO"
Source:http://daresalaam-yetu.blogspot.com/2012/10/mbunge-sugu-ataka-tra-wamtoze-kodi-rick.html#.

****Nawasilisha****
 
Labda hadi pale TRA itakapoondoka kwenye mikono ya hawa manyang'au ndipo tutakuwa serious na ukusanyaji wa mapato, lakini kwa hali ya sasahivi ni kwamba ze boss anakunja mkwanja mzima mzima na kusepa.
 
Kweli ndivyo inavyo takiwa hila kwa nchi kama tanzania wanavyo penda kubembeleza wamarekani hiyo kitu ni ngumu!

Kama wasanii wetu wakienda marekani wana katwa kodi ni haki yetu pia kupata mapato kupitia hiyo shoo!

Lakini kwa nchi inayoongoza kuwa na maajabu mengi that won't happen.
 
Yes nisahihi huyo ross akatwe kodi kwenye pato lake la leo. Sio aje achume na kuondoka wakati walim mshahara 469000 kwa mwezi nakatwa kodi. yeye kwa cku ni zaidi ya milion 100 halafu akatwi kodi. So tra ikate kodi hapo. Kama tz ina mkataba na usa kuhusu double taxation, sisi tukate huku atasamehewa kwao huko.
 
Hapa si swala la clouds kulipa on behalf, RICK ROSS ana takiwa aambiwe kuwa utalipwa kiasi kadhaa na kodi utakatwa asilimia kadhaa na kiasi utakacho ondoka nacho ni Tsh kadhaa, hii ndio inayo takiwa.

Kwa sababu tunategemea kodi ilipwe kulingana na atakacho pewa!

clouds ndo inabidi walipe withholding Tax on his behalf
 
Kwanza hawa jamaa ukute wana lipwa pesa nyingi tu na bado hawakatwi kodi. Tusitegemee wa america wanaweza kukuacha usilipe kodi.
 
Hapa si swala la clouds kulipa on behalf, RICK ROSS ana takiwa aambiwe kuwa utalipwa kiasi kadhaa na kodi utakatwa asilimia kadhaa na kiasi utakacho ondoka nacho ni Tsh kadhaa, hii ndio inayo takiwa.

Kwa sababu tunategemea kodi ilipwe kulingana na atakacho pewa!

Kawaida Withholding TAX inabidi alipe mtoa huduma kama Rick Rozz ndo inabidi alipe kodi
kwasababu amatoa service tofauti na nchi yake au CLOUDS wanaweza kusema watamlipia
wenyewe kwa kugross up ile amount ili ionekane mwenyewe ndo kalipa

Lakini kwasababu CLOUDS FM ni CCM usitegemee haya mambo ya kulipa KODI

Nakala kwa, Mwita25, Teamo, tarmo, Nnauye Jr
 
Last edited by a moderator:
Hili la Ross mie halininyimi usingizi iwapo matapeli wanatumia madhehebu ya dini kukwepa kodi ukiachi ambali wahindi kuja na kujichotea utajiri huku tunaona. Tatizo ni watanzania wenyewe. Tumeridhika na umaskini wetu na ushamba la bibi wa taifa letu huku tukitawaliwa na vilaza na wasanii. Sugu umenena ingawa hakuna atakayekuelewa hasa wahusika.
 
Hii iwe inafanyika kwenye mechi za mpira pia kama ilikuwa haifanyiki.Brazil kabla ya kwenda SA kwenye kombe la dunia,waligema pesa nyingi sana ambazo nahisi hata kodi hawakulipa!
 
Kwanza hawa jamaa ukute wana lipwa pesa nyingi tu na bado hawakatwi kodi. Tusitegemee wa america wanaweza kukuacha usilipe kodi.

atafanya sho ya dakika 45..analipwa za kitanzania milioni mia mbili na ushee,then atuachii ata shilingi kumi.
 
Back
Top Bottom