Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,566
Ubunge ni dili kubwa sana kwa huyu jamaa. Nakumbuka 1995 alishinda kwenye kura ya maoni, lakini ccm ilimpiga chini kwa madai kuwa hajakomaa kisiasa. Tokea hapo ilibidi aanze kugawa chakula kwa wananchi, na pia akajitolea kujenga jengo la ofisi ya ccm mkoa wa Singida kwa gharama yake. Hapo utagundua aliutafuta ubunge kama kinga ya baadhi ya biashara zake zisizofuata utaratibu. Pia utagundua kuwa siyo kwamba anatumia posho za kibunge kuwasaidia wapiga kura wake, kwasababu alikuwa akifanya hivyo hata kabla hajawa mbunge. Msaada anaoutoa ni mdogo sana kulinganisha na anavyowaibia wananchi.