Mbunge Godfrey Lema Atishiwa Kuuwawa....

Nimelisikia juu juu asubuhi kupitia tanzania daima,mwenye niuz kamili atuwekee kwani nipo meru huku valesca,HAWA JAMAA WANAONA KUWA Lema ana comsng power ya kutisha.magamba bwana

kumbe na wewe umesikia juu juu.

hata me nilisikia juujuu tu

Jamani tupeni taarifa iliyoshiba,sasa kila mmoja akija na taarifa nusu nusu namna hii sidhani kama itakuwa ni afya kwa jukwaa letu...kama una taarifa kaa kimya ili wenye taarifa watujuze.Sasa kila mmoja akiwa anasema hata mimi nimesikia juu juu,si itakuwa ni kituko?
 
kitendo cha kutishia kuua hilo ni kosa kwa mujibu wa katiba ya JMT...na la kushangaza zaidi informer wa habari hizi ni mwanasheria Tendwa....
 
Hivyo vizee vinnatishia kuua wakati muda wao wa kuishi umeisha, Tendwa anapaswa kutumia hbr hizo kuwashtaki hao wazee haki ya Lema kuishi iko wapi? na polisi wanachukua hatua gani kwa hao wazee? au ndio mambo ya DCI Manumba kuja na ushahidi wa ofisini?
 
Hivyo vizee vinnatishia kuua wakati muda wao wa kuishi umeisha, Tendwa anapaswa kutumia hbr hizo kuwashtaki hao wazee haki ya Lema kuishi iko wapi? na polisi wanachukua hatua gani kwa hao wazee? au ndio mambo ya DCI Manumba kuja na ushahidi wa ofisini?

Nasikitika sana mmoja wa wazee hawa ni CDF wetu wa zamani the right and most retired Gen Mirisho Sarakikya......used to be an icon in my opnion but not anymore......
 
Politics propganda....LEMA amekuwa mwiba kwa magamba.ivi sasa lema akiuawa tendwa si atakuwa anawajua wauaji.TENDWA ACHA KUTUMIKA,KUNA SIKU UTAWAJIBIKA KWA YOTE HAYO
 
Nasikitika sana mmoja wa wazee hawa ni CDF wetu wa zamani the right and most retired Gen Mirisho Sarakikya......used to be an icon in my opnion but not anymore......

Ni ajabu sana kama kweli Sarakikya naye anaweza kutumiwa na ccm kufanya siasa za majitaka. Kwa hali kama hii naanza kuamini kwamba hawa maCDF wanakuwa na kadi za jembe na nyundo mifukoni mwao wakati wakiwa ndani ya utumishi wa jeshi.
Kwani huu ni muendelezo tu, baada ya kumshuhudia CDF mstaafu mwingine Robert Mboma akijitosa kuwania ubunge Mbeya Vijiji mwaka juzi baada ya kifo cha Richard Nyaulawa, na hii ilikuwa si muda mrefu tangu astafu jeshi.
 
Ni Hivi!

Nenda kamwambie huyo Nape aliyekutuma kuwa Godbless Lema ndiye atakaye ongoza kampeni za CDM Arumeru Mashariki!

Tangu juzi unaleta uzi huu huu ukiwa na heading tofauti tofauti, sijui wamekulipa shilling ngapi? tena naona wamagamba mmeisha anza kuweweseka kimtindo na bado safari hii tunawamaliza
 
Ndo siasa hata abroad zipo!Cha msing ka ni kwel busara ifwate mkondo wke!Tz ni nchi ya matajir na maskin,wny haki na waso haki,makabila na dini zote!Wajinga na werevu, Mungu ijalie nchi yetu!
 
Hawa wazee wa mafisadi ni nini haswa G. Lema aliwaambia hawa wazee?

Ama ni mazito mpk hayafai kuwekwa hapa?

Hayo maneno yawekwe kwenye jukwaa lengwa!
 
huyu zubeda mchuz,umekosa ugali nn?mbna unaandika mboyoyo?ningekuwa na nguvu za mod ningekuweka ban,cz unapotosha jamii.na unachochea vurugu
 
mkuu meru bado upo sana .

Hawa wazee wa kikabila wameanza lini kuwepo mbona ndo mara ya kwanza nawasikia na kama wana influence mbona hata hawana wafuasi zaidi ya ndugu zao wachache tu? Nafikiri tendwa angewaleta mbele ya screen ya TV tuwaone. Kama kuna wazee wa mila waliokuwa na nguvu basi ni kule Sirte Libya alikojificha Gaddafi na jeuri yao haikusaidia kumficha Gaddafi. Hawa wazee wa Arumeru ni wa kuchonga kwani ni sawa utishie eti kule Hai, Rombo au Vunjo mbunge hawezi pita bila wazee kuamua; huu ni uhuni wa mchana ambao sikutegemea ntu kama Tendwa kujihusisha nao.
 
Ni Hivi!

Nenda kamwambie huyo Nape aliyekutuma kuwa Godbless Lema ndiye atakaye ongoza kampeni za CDM Arumeru Mashariki!

Tangu juzi unaleta uzi huu huu ukiwa na heading tofauti tofauti, sijui wamekulipa shilling ngapi? tena naona wamagamba mmeisha anza kuweweseka kimtindo na bado safari hii tunawamaliza
Acha bange wewe...waandikie email hbr leo
 
UKWELI KUHUSU LEMA PALE ARUMERU NI HUU;

Lema alikoroga ARUMERU.
Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema kuwa mbunge wa arusha mjini Godbless Lema CHADEMA ametia dosari kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la arumeru mashariki
amesema kitendo chake cha kufanya vurugu wakati wa mazishi ya marehemu SUMARI kimetia dosari siasa za jimbo hilo hivyo,yeye Lema pamoja na chama chake wanapaswa kuomba radhi kabla kampeni hazijaanza.
zaidi soma magazeti ya leo na ilitoka kwenye taarifa za habari usiku wa jana na leo asubuhi.
 
we hata jina la mbunge hulijui utaweza kutuletea habari ya maana wewe. mbunge anaitwa Godbless LEMA sio geofrey.unaishi wapi wewe
 
TENDWA; LEMA AOMBE RADHI ARUMERU

Imeandikwa na Waandishi Wetu; Tarehe: 22nd February 2012


MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri' vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

''Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema," alisema Tendwa.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

''Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi," alisema.

Msajili alisema; ''ujambazi wa siasa'' hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi nao wanapaswa kuziepuka.

Ushindi wa Siyoi Wakati huohuo, Katibu wa Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, amesema utaratibu wa kuteua mgombea aliyepata asimilia 51
ya kura za maoni bado haujaanza kutumika rasmi CCM.

Alifafanua kuwa bado chama hicho kina nia ya kufanya mabadiliko katika mfumo wake wa kura za maoni, ili kifike mahali mgombea anayetoka chama hicho, awe amechaguliwa kwa asilimia 51 ya kura zote.

Alisema hayo alipohojiwa na gazeti hili kuhusu ushindi wa kura za maoni katika jimbo hilo kwa Siyoi Sumari ambaye idadi ya kura zake ni pungufu ya asilimia 50 ya kura zote.

Katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika juzi Arumeru kwa ajili ya kupatikana mgombea wa CCM, Siyoi (30) aliibuka na ushindi kwa kura 361 kati ya kura 1,034 za wajumbe wa chama hicho.

Wagombea wengine walikuwa William Sarakikya (259), Elirehema Kaaya (205), Elishiria
Kaaya (176), Anthony Msani (22) na Rishiankira Urio aliyeambulia kura 11.

Akizungumzia taarifa hizo, Nape alisema hakuna
ushahidi wowote unaothibitisha taarifa hizo,
hivyo hawezi kuisemea hali hiyo ina athari gani
kichama katika uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa
kufanyika Aprili mosi.
Uchaguzi huo unatokana na kifo cha aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari (CCM)
aliyefariki dunia mwezi uliopita.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom